Mruhusu bosi aseme mwanzo

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,816
0
Bosi mmoja na wafanyakazi wake walikuwa wanaenda kujipatia kinywaji na kupumzika kidogo baada ya kufanyakazi saa bila kupumzika. Njiani walikutana na Aladini akawapa ofa ya kila mmoja kuomba chochote anachotaka na kingetekelezwa. Ugomvi ukawa nani aanze kuomba, hatimaye akaanza mdogo kabisa:
MFANYAKAZI MDOGO: Mimi naomba likizo la mwezi mmoja, niende Australia na kulipiwa gharama zote - Ombi lake lilikubaliwa na hapo hapo akajikuta yuko Australia.
WA KATI: Mimi naomba likizo la mwaka mzima niende Brazili na gharama zote kulipiwa - Ombi lake naye lilikubaliwa ghafla akajikuta yuko Brazil.
ALADINI: Na wewe unaomba nini?
BOSI: Ninawataka hawa wapuuzi wawili ofisini sasa hivi tuendelee na kazi.

Wote wakiwa ofisini wakalalamika - laitani tungelimwachia bosi yeye kwanza kuomba.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom