Mrisho Ngassa na Canavaro Waihenyesha Yanga: Jeuri ya fedha ya Azam Yawa Mwiba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrisho Ngassa na Canavaro Waihenyesha Yanga: Jeuri ya fedha ya Azam Yawa Mwiba.

Discussion in 'Sports' started by Junius, May 19, 2010.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ule wakati wa Klabu kubwa maarufu za Tanzania, Yanga na Simba, ambazo ni wababe wa soka la nyumbani huku zikiwa urojo katika medani za kimataifa unakaribia kufikia hatima.
  Hatua hiyo inakuja baada ya timu ya Yanga kujikuta ikizidiwa ubavu wa kifedha na timu ya Azam FC,inayopigana kwa jeuri ya fedha kuwan'goa jangwani wachezaji wa kutumainiwa wa Yanga, Mrisho Ngassa na libero hodari wa timu hiyo,mtoto wa Kipemba, Nadir Haroub "Cannavaro".
  Viongozi wa klabu hiyo kongwe katika medani ya soka la bongo wamekiri wazi kuwa hawana ubavu wa kuwazuia wachezaji hao kwa vile Azam FC, imetangaza kuwapa dau kubwa zaidi ambalo Yanga licha ya kuwa na matajiri na washabiki wengi nchini hawana uwezo nalo.
  Huku hali hiyo ikionekana kuwanchanganya viongozi wa Yanga tayari Mrisho Ngasa amenukuliwa akisema kinaga ubaga kuwa hayupo tayari kubaki Yanga kwa mshahara wa 400,000, wakati Azam wametangaza kumlipa zaidi ya mara tatu ya kiasi hicho.
  Habari zaidi bofya hapa.Dullonet Tanzania | Just Call it Real Solution for News and Information
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hii imenikumbusha mchezaji mmoja wa zamani wa Yanga na Simba, Bakari Malima "Jembe Ulaya", wakati akihama Yanga kwenda Simba alisema,mpira sasa ni maslahi tu,ule wakati wa kusema kuwa unachezea timu kwakuwa uliipenda tokea utotoni umepitwa na wakati.
  Namuunga mkono Ngassa na Cannavaro, kwakuwa ni mda wa kujikomboa na manyanyaso na dhuluma wanazofanyiwa na viongozi wao, wanaopendelea wachezaji wa kigeni na kuwalipa mishahara mikubwa huku uwezo wao ukiwa wa kawaida au mdogo kulingana na baadhi ya wachezaji wazawa.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hatima ya Ngassa itakuwa leo usiku kwa mujibu wa msemaji wao Louis Sendeu, wakati watapokutana na Azam FC kwa ajili ya mazungumzo juu ya uhamisho wake. Wakati huo huo Sendeu amedai kuwa suala la Canavaro kutaka kuhamia Azam hawalijuwi kabisaaaa.
   
Loading...