Mrisho mpoto

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Huu wimbo wa mpoto CHOCHEA KUNI mashairi yake yana ujumbe gani? "...chochea kuni .... muwaite mamluki...wakija wasubiri" "..mtu anatapika nyongo yake anarudia tena kuila mnamwangalia?" "...utawaulizaje watu magongo ya nini akati ulisema kuna nyoka? Mjomba wewe si uliwapaka wanja ngoja wao wakupake pilipili afu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga" " "....nisiwe ka wanasiasa hawaoneki hadi kuwe na janga, utawasikia natoa katon 20 za sabun ya unga nani ka kuambia wale ni wachafu?"

Nyimbo zake nyingi huwa zina mafumbo sana mpaka inakuwa ni shida sasa huyu jamaa kueleweka na hadhira yake na hii katika tasnia ya fasihi msanii anakuwa ameshindwa kuitendea haki tasnia
 
Mie kwa kuwa simpendi, hata nyimbo zake sinaga muda wa kuzisikiliza.
 
Aliposhirikishwa kwa mara ya kwanza na Irene Sanga ktk wimbo wa Salaam kwa mjomba nikajua jamaa ni mwanamapinduzi type ya kina Chico, Brenda, na Chakachaka kumbe wapi! Jamaa kiukweli mnafiki sana.
 
haaha mvuto ka wa Omy dimpoz au sukari ya warembo

me ndo naijua definition ya huo mvuto ambao amekosa so hao kina sukar ni wenu. Mwanaume mbaya ka utando wa uji wa ulezi uliolala, tifutifu ka furushi la magimbi loh na huo unakfi wake bhaaassss ful kinyaa
 
Ana njaaaa hana lolote, na kujifanya anaumia na hali ya tanzania. Wakat yeye kama yeye n mnafiki, mkubwa. Mwili mkubwa anatumika na wattooto kama rugeii
 
achape lapa mbele yaani yule afai ata kidogo mzandiki mkubwa.
 
ni kweli kabisa....mafumbo yanapokua mazito mno, panakua na udhaifu wa mwandishi japo amefanya kazi nzuri!
Lakini pia Shaaban Robert alikua na mafumbo mengi na mazito japo miongoni mwake, yaling'amuliwa na hadhira yake.

"Mjomba wewe si uliwapaka wanja ngoja wao wakupake pilipili afu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga"

hapo kwenye RED nimeelewa kwamba, Kiongozi Mkuu amekua akiwalea lea watu fulani, ilhali watu hao si wema. Matokeo yake sasa wao huenda wakaja kumsababishia matatizo katika uongozi wake kiasi cha kumfanya ashindwe kumwona adui, anayetaka kumharibia...kwa maana ya kombolela unapozinga unapaswa kumzuia adui asibutue!
 
''Akuambiae usikombe mboga anakutakia ushibe! By Mrisho Mpoto jamaa namkubali sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom