Elections 2010 Mrisho mpoto na uchaguzi

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,831
8,621
Wana JF,
kwanza poleni kwa usumbufu mnaopata kutokana na ujumbe wa simu unaoendelea kusambazwa na hili GENGE LA MAHARAMIA WANAOONGOZWA NA TEJA LAO MIRAJI.

Dhumuni langu kubwa hapa nataka nielezee elimu inayoendelea kutolewa na msanii maarufu hapa nchini Mrisho Mpoto.

Kati ya matangazo yake mengi yanayosambazwa kwenye vituo mbalimbali vya TV, lililonigusa zaidi ni lenye ujumbe ufuatao; nanukuu; “………………..UKIONA UMEKULA UJUE UMELIWA”.

Kutokana na ujumbe huo labda niwaambie marafiki zangu kina MALARIA SUGU, QUIENIN, MAGGID, KUDADEKI na wengineo wengi wanaoendelea kutetea utawala wa kifisadi kutokana labda kulipwa au kufaidika kwa namna moja au nyingine na mfumo wa serikali inayoondoka madarakani hivi karibuni kuwa, KAMA WAMEKULA BASI WAJUE WAMELIWA PIA hasa ukizingatia kauli za rais anayestaafu hivi karibuni kwenye moja ya hotuba zake alipowaambia wananchi kuwa, nanukuu; “…….UKITAKA KULA NA WEWE LAZIMA ULIWE KIDOGO…”
Historia itawahukumu hasa pale atakapoinuka mtawala mwingine ambae hamjui mtoto wa MAGGID, SHIMBO, TENDWA, MKUU WA REDET na wengine wenye kutaka kupora haki ya wanyonge kwa kutumia kalamu au vyeo na dhamana walizokabidhiwa.

Ninachowaambia ni kuwa UKIONA UMEKULA UJUE UMELIWA.
 
Wana JF,
kwanza poleni kwa usumbufu mnaopata kutokana na ujumbe wa simu unaoendelea kusambazwa na hili GENGE LA MAHARAMIA WANAOONGOZWA NA TEJA LAO MIRAJI.

Dhumuni langu kubwa hapa nataka nielezee elimu inayoendelea kutolewa na msanii maarufu hapa nchini Mrisho Mpoto.

Kati ya matangazo yake mengi yanayosambazwa kwenye vituo mbalimbali vya TV, lililonigusa zaidi ni lenye ujumbe ufuatao; nanukuu; "………………..UKIONA UMEKULA UJUE UMELIWA".

Kutokana na ujumbe huo labda niwaambie marafiki zangu kina MALARIA SUGU, QUIENIN, MAGGID, KUDADEKI na wengineo wengi wanaoendelea kutetea utawala wa kifisadi kutokana labda kulipwa au kufaidika kwa namna moja au nyingine na mfumo wa serikali inayoondoka madarakani hivi karibuni kuwa, KAMA WAMEKULA BASI WAJUE WAMELIWA PIA hasa ukizingatia kauli za rais anayestaafu hivi karibuni kwenye moja ya hotuba zake alipowaambia wananchi kuwa, nanukuu; "…….UKITAKA KULA NA WEWE LAZIMA ULIWE KIDOGO…"

nadhani ujumbe umefika kwa:llama::llama::llama:
 
Please huyo muondoe katika kundi hilo. Hayumo kabisa. Ni ndugu yangu na namfahamu. Tena muombe radhi.
 
namuomba radhi mkuu, lile jina la malaria sugu lilinichanganya na hii dawa ya quinin, kumbe QUININ ni dawa ya huyu malaria!!! vvery sorry.
 
huwa watz tunaridhika na vitu vidogo, kama kupigiwa makofi na kupewa sifa, huku tukiweka rehani mustakabali wa Taifa letu
 
jana nimemuona akichana kuhusu uchaguzi mkuu kwenye kipindi cha asubuhi star tv. serikali ingekuwa inasikiliza mashairi yake wangejua kuwa wanalengwa wao, ila wanajifanya hawasikii tena watamualika huyo huyo anaewachana ahudhurie matamasha yao, duh, kweli.......
 
Chura anapenda maji lakini sii ya moto, kuingiza roho za watu kwenye siasa ni hatari, ni baadhi ya mafumbo ya bwana Mpoto nayapenda saaaaana
 
Nachojuiliza, je ujumbe wake wanauelewa au wanapata buradani tu? Maana ujumbe wake unamgusa sana mjomba na bado hajibu wala hashituki, lkn walicho nishangaza walimwalika kwenye sherehe za kuzima mwenge Kigoma. Ila nahisi alipoanza kumwaga message walimkatiza.
 
Sijaelewa ina maaana sasa CCM baada ya kutula na sie twawala??????????????????????? haya ngoja nijipanguse mie
 
hapo anamaanisha wale wanaopokea vizawadi kutoka kwa wagombea wasijidai kuwa wameula, wajue ndo wanaliwa.
 
imekaa vizuri sana , kweli ukiona umekula kumbe umeliwa

mimi napinga si lazima ukila na wewe umeliwa, ila ngoma nzito uchaguzi wa mwaka huu, chadema kiwewe, ccm kiwewe, huko zanzibar in mshikishike
 
huyu jamaa namkubari kwa jinsi anavyotoa ujumbe mzuri wa kwa jamii, mbali na kutumiwa kwenye matangazo baada ya kuonekana anakubalika kwa jamii pia nyimbo zake kwenda kwa mjomba ni nzuri sana na zina ujumbe mzito. na hisi baadhi ya viongozi serikalini na mafisadi hawampendi sababu ya ujumbe unaokuwa kwenye nyimbo zake
 
Halafu ujumbe umejaa falsafa kali kweli kweli. watawala wanajitahidi kumweka kwenye kwapa zao lakini jamaa anafurukuta big time.
I know this dude kwa kupenda kuongea na kusimamia ukweli.

Ataghani, watamshangilia lakini kawachoma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom