Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,762
Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amefunguka na kuzungumzia kitu alichojifunza kutoka kwa msanii Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anatajwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wenye mafanikio makubwa barani Africa.
Mrisho Mpoto akiwa na Diamond
Mtunzi huyo wa mashairi ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Sizonje’ ameiambia Bongo5 kuwa Diamond ndiye msanii aliyemshauri mambo mengi kuhusu muziki pamoja na kuingia katika mitandao ya kijamii.
“Diamond ndiyo mtu ambaye alinifuata na kuniambia Mjomba ingia Instagram, huku unapost picha na kuandika maneno machache, nikamwambia hapana mimi sitaki kuingia huko lakini baadae nikakaa na kuamua kuingia lakini yeye ndiye aliyenishtua kwa mara ya kwanza,” alisema Mrisho Mpoto.
Aliongeza, “Nakumbuka kuna maneno ambayo aliniambia Diamond mpaka leo siwezi kuyasahau, aliniambia Mpoto ukipata mia tano kwenye muziki wako, usitumie yote, tumia mia mbili na mia tatu wekeza kwenye muziki wako utafika mbali. Hii kauli imenisaidia sana, muziki au kazi ya sanaa hauwezi kuifanya peke yako, lazima ufanye kazi na watu ili uweze kwenda mbele,”
Mpoto amedai Diamond ni mmoja kati ya wasanii ambao wanatakiwa kuigwa kutokana na juhudi zao katika muziki.