PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 877
- 952
Mstanii wa Mashairi Mrisho Mpoto (Mjomba) amesaini Mkataba wa makubaliano ya pamoja na Shirika la Posta Tanzania kuwa Balozi wa Shirika hilo. Shirika la Posta Tanzania limeingia Makubaliano na Msanii huyo ili kulitangaza Shirika pamoja shughuli zote za Shirika hilo ikiwemo Huduma Pamoja, Duka Mtandao, EMS, Post Cargo, Pcum pamoja na Posta kiganjani Ndani na Nje ya Nchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Postamasta Mkuu Bwa. Macrice Daniel Mbodo amesema kuwa Shirika la Posta kwasasa lipo kwenye mageuzi makubwa ya kiutendaji hivyo Shirika limeona vyema kushirikiana na Mrisho Mpoto kulitangaza Shirika hilo.
"Kwasasa Shirika la Posta lipo kwenye Mageuzi Makubwa ya Kiutendaji pamoja na Maboresho ya Huduma zetu, kama Shirika limemteuwa Bwa Mrisho Mpoto (Mjomba) kuwa Balozi wa Shirika la Posta ili kulitangaza Shirika pamoja na shughuli zote zinazofanywa na Shirika la Posta Tanzania " Macrice Mbodo
Kaimu Postamasta Mkuu aliendelea kwa kusema Wananchi wanafahumu Huduma moja tu inayotolewa na Shirika la hilo,
"Wananchi wanafahamu Huduma moja tu inayotolewa na Shirika la Posta, Huduma ya kutuma na kupokea barua lakini kwasasa kupitia Ofisi zetu za Shirika la Posta unaweza kupata Huduma ya NIDA, RITA, Pasi ya kusafiria pamoja Huduma za Kibenki, Imani yetu kama Shirika kupitia Mrisho Mpoto atazitangaza Huduma hizi kwa Wananchi " Macrice Mbodo
Aidha kwa upande wa Mrisho Mpoto amelishukuru Shirika la Posta Tanzania kwa kumuamini na kumtekuwa kuwa Balozi wa Shirika hilo.
"Nilishukuru sana Shirika la Posta Tanzania kwa kuniamini na kuniteuwa kuwa Balozi hii ni heshima kubwa kwangu nitakwenda kulitangaza Shirika pamoja na Shughuli zote za Shirika la Posta Tanzania kama Balozi wa Shirika hili" Mrisho Mpoto