BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Ni kweli ni rahisi kumuita mnafiki lakini kweli hoja anazojenga mjengoni zina mashiko sana na Watanzania wengi tunaziunga mkono kwani Watanzania wengi wamedhulumiwa sana na yule mwendazake na Serikali yake. Ukweli ni lazima ubaki ukweli. Je, atapewa onyo kwamba apunguze maneno makali mjengoni au atakuwa mbunge wa awamu moja? Tusubiri.
Hakika mkuu, huyu jamaa alijijengea taswira mbaya sana machoni pa wengi hasa akiwa RC Arusha. Tangu aingie mjengoni ni kama vile kabatizwa ubatizo wa maji mengi - anajenga hoja zenye mashiko sana. Hata kama atapigwa mawe na wengi kwamba alikuwa sehemu ya udhalimu wa awamu iliypopita lakini ukweli utabakia kuwa ukweli tu kwamba anajenga hoja vizuri. Wahenga walisema: "Ukweli utabakia kuwa ukweli hata kama ungetoka kinywani mwa shetani"!!!