Mrisho Gambo: Sisi mpinzani wetu siyo vyama vya siasa ni changamoto za Watanzania

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
“Sisi Mpinzani wetu sio Vyama vya Siasa, Mpinzani wetu ni changamoto za Watanzania leo ukizungumza Watumiwhi wana manung’uniko kuhusu mishahara yao, wana manung’uniko kuhusu kupanda madaraja kwa miaka mitano hawajapanda madaraja, leo ukizungumza kuhusu bodi ya mikopo unaona sheria ilikuwa inasema asilimia 8 baadae imekwenda asilimia 15 lakini hayo mambo yamepitishwa ndani ya Bunge hili" Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini.

"Lakini ukiangalia tuna changamoto kwenye bima ya afya, tuna changamoto kwenye ajira, manung’uniko ni makubwa. Kazi ya Bunge hili ni kurekebisha sheria, kutoa mapendekezo na ushauri ambao Serikali ikifanyia kazi matumaini yataendelea kudumu kule kwa Watanzania" Mrisho Gambo.

 
Huyo aendelee kupeta mchele jikoni ! Waliwekwa hapo na Jiwe !

Ndio maana jiwe alijisahau akasema "wengine hamkuchaguliwa na wananchi" ndio kama kina Gambo hao
2525477_120041101_3360033017421700_256927606636531134_o-1-650x450.jpg
 
Kwa kweli hapo Mrisho Gambo umenena. Shughulikieni changamoto za wananchi. Hiyo Minyukano ya Kundi la Mwendazake na la Samia haitusaidii. CCM haina mwelekeo wa kuisaidia nchi. Angalia sasa hicho chama hakina mwenyekiti, katibu wala katibu mwenezi. Ni chama kinachoningínia mahali fulani hewani tu.
 
“Sisi Mpinzani wetu sio Vyama vya Siasa, Mpinzani wetu ni changamoto za Watanzania leo ukizungumza Watumiwhi wana manung’uniko kuhusu mishahara yao, wana manung’uniko kuhusu kupanda madaraja kwa miaka mitano hawajapanda madaraja, leo ukizungumza kuhusu bodi ya mikopo unaona sheria ilikuwa inasema asilimia 8 baadae imekwenda asilimia 15 lakini hayo mambo yamepitishwa ndani ya Bunge hili" Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini

"Lakini ukiangalia tuna changamoto kwenye bima ya afya, tuna changamoto kwenye ajira, manung’uniko ni makubwa. Kazi ya Bunge hili ni kurekebisha sheria, kutoa mapendekezo na ushauri ambao Serikali ikifanyia kazi matumaini yataendelea kudumu kule kwa Watanzania" Mrisho Gambo

View attachment 1751705
Naona ule mgando kichwani umeanza kuyeyuka wanaanza kupata akili sa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom