Uchaguzi 2020 Mrisho Gambo, Arusha unapwaya. Lema awasikilizisha Wananchi Audio ya Magufuli akieleza sababu za kutenguea uteuzi wa Gambo

Administer

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
678
1,000
Nimehudhuria mkutano wa Mgombea Ubunge Arusha Mjini kupiti CHADEMA, Godbless Lema leo, amekuchafua sana, amemwambia DJ aweke sauti ya Rais Magufuli akieleza sababu za kutengua uteuzi wa Gambo

Baadae tukamsikia Bashiru wote wamekuuleza wewe kama mtu mchonganishi na hufai kuwa kiongozi.

Lema akauliza umati ule, kama Gambo yuko hivi atawezaje kuongoza Jimbo la Arusha mjini ilihali viongozi wake wamemuelezea sifa zake? Ninaona Lema kawekewa mpinzani ambaye hauziki.

netein

Senior Member
Sep 20, 2019
156
250
Nimehudhuria mkutano wa Lema leo,amekuchafua sana,amemwambia DJ aweke sauti ya Magu akikufukuza kazi,baadae tukamsikia Bashiru wote wamekuuleza wewe kama mtu mchonganishi na hufai kuwa kiongozi.Lema akauliza umati ule ,kama Gambo yuko hivi atawezaje kuongoza jimbo la Arusha mjini ilihali viongozi wake wamemuelezea sifa zake?Ninaona Lema kawekewa mpinzani ambaye hauziki
Gambo hana chembe ya sifa ya kugombea jimbo gumu kama Arusha, CCM pale walifeli.
 
jo mose

JF-Expert Member
Aug 5, 2020
3,489
2,000
Nimehudhuria mkutano wa Lema leo, amekuchafua sana, amemwambia DJ aweke sauti ya Magufuli akikufukuza kazi, baadae tukamsikia Bashiru wote wamekuuleza wewe kama mtu mchonganishi na hufai kuwa kiongozi. Lema akauliza umati ule, kama Gambo yuko hivi atawezaje kuongoza jimbo la Arusha mjini ilihali viongozi wake wamemuelezea sifa zake? Ninaona Lema kawekewa mpinzani ambaye hauziki.
Gambo Akatafute kazi zingine
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
29,393
2,000
Gambo hana chembe ya sifa ya kugombea jimbo gumu kama Arusha, CCM pale walifeli.
Jimbo la Arusha limechangamka Sana Kama limetiwa ndimu...kwahyo na mgombea anatakiwa awe hivyo hivyo.mtoto wa mjini. ..kichaa Fulani...sasa unatuletea Gambo 'msabato' huyo wapi na wapi..hili Jimbo linataja mtu mwenye fitna. Na Lema ndo ana sifa hizi ..Gambo fungua kampuni yaulinzi unafit huko...🤸🦸
 
Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
1,908
2,000
Wiki iliyopita nilitoa ushauri kwa CHADEMA kutumia kauli tata za Magufuli alizowahi kutamka nyakati tofauti ili kuwakumbusha wananchi maneno yake ya kiburi,kejeli na ya kuudhi dhidi yao,audio hizi zitumike wakati wa mikutano ya kampeni.

Nimesiki Gobless Lemma akitumia audio ya magufuli kumfukuza Gambo ukuu wa mkoa kuwakumbusha Arusha kuwa Gambo siyo mstaafu bali alifukuzwa kazi

Ushauri mujarabu kwa CHADEMA kuhusu kutumia mapungufu/ makosa katika kuongea kwa Mgombea wa CCM
Uchaguzi 2020 - Ushauri mujarabu kwa CHADEMA kuhusu kutumia mapungufu/ makosa katika kuongea kwa Mgombea wa CCM

Mkutano wa Lemma huu hapaHuu ndio ubunifu
 
Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
1,941
2,000
CCM ni genge la wahuni waliojitwalia mamlaka kwa njia za ajabu.
Nimeamini kuwa siasa ni techniques
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
2,173
2,000
Mkuu Swali Langu Ni Hili;

Kwa kuwa Tume Ya Uchaguzi Imetoa Mwongozo Kuhusu Kampeni Zenye Lugha za kuudhi na Matusi pamoja na uchochezi;Je Hauoni Kama AUDIO hizo,zinaweza kumharibia mh.Lema Kupelekea kupata adhabu iliyotajwa na Dr.Mahela?!!!
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
2,278
2,000
Jana nimesikia maeneo ya Kawe Chadema wanatumia kauli ya Gwajima kwenye gari yao matangazo alivyodai Uaskofu ni kazi kubwa zaidi ya Uwaziri na Urais.

Haya mambo yapo ni ya kweli, huyo Mwenyekiti wa Tume aache kuwatisha watu.
 
Uoga sio kitu kizuri, kauli zao walizitoa wenyewe leo wanasema zinawaudhi, sasa walitaka wafurahishwe au?
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,402
2,000
Jana nimesikia maeneo ya Kawe Chadema wanatumia kauli ya Gwajima kwenye gari yao matangazo alivyodai Uaskofu ni kazi kubwa zaidi ya Uwaziri na Urais.

Haya mambo yapo ni ya kweli, huyo Mwenyekiti wa Tume aache kuwatisha watu.

Walisha jimiminia Mafuta wenyewe Mkuu ,kazi yetu ni moja tu kutia kiberiti na kuwa kaanga..
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
7,591
2,000
Gambo hana chembe ya sifa ya kugombea jimbo gumu kama Arusha, CCM pale walifeli.
CCM hawajafeli wao hawategemei kura zenu wao wanategemea tume ya uchaguzi itakapomtangaza saa tisa za usiku kuwa Gambo mshindi na nyie mtabakia kuokota porini masanduku ya kura.
 
mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
6,195
2,000
Mkuu Swali Langu Ni Hili;

Kwa kuwa Tume Ya Uchaguzi Imetoa Mwongozo Kuhusu Kampeni Zenye Lugha za kuudhi na Matusi pamoja na uchochezi;Je Hauoni Kama AUDIO hizo,zinaweza kumharibia mh.Lema Kupelekea kupata adhabu iliyotajwa na Dr.Mahela?!!!
Aliyetoa hizo ndio wa kulaumiwa sio lema
 
mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
6,195
2,000
CCM hawajafeli wao hawategemei kura zenu wao wanategemea tume ya uchaguzi itakapomtangaza saa tisa za usiku kuwa Gambo mshindi na nyie mtabakia kuokota porini masanduku ya kura.
Kuna majimbo ya makondoo ila sio arusha,mbeya mjini na iringa mjini ,ukitamka vinginevyo watu wanaingia barabarani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom