Mrembo wa Tanzania Aolewa na Kibabu cha Kiingereza, Anusurika Kukatwa Mikono Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrembo wa Tanzania Aolewa na Kibabu cha Kiingereza, Anusurika Kukatwa Mikono Yake

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Dec 21, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG]
  Saluni ya urembo inayomilikiwa na William Porter[/TD]
  [TD]Sunday, December 04, 2011 7:58 PM
  Mwanamke mrembo wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 25 tu amekiona cha moto baada ya kukubali kuolewa na babu wa Uingereza mwenye umri wa miaka 69 na matokeo yake kujeruhiwa kwa kisu alipolalamika pafomansi mbovu ya babu kitandani.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mwanamke wa Kitanzania aliyejulikana kwa jina la Saada Mwiazimu mwenye umri wa miaka 25 amenusurika maisha yake baada ya kujeruhiwa kwa kisu na mumewe mfanyabiashara wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 69 anayejulikana kwa jina la William Porter.

  William anamiliki saluni maarufu ya masuala ya urembo inayojulikana kwa jina la Tan Express iliyopo kwenye mji wa Scarborough, kaskazini mwa Uingereza.

  Kasheshe la Saada kujeruhiwa kwa kisu lilitokea mwezi juni mwaka jana wakati Saada na mumewe walipokuwa kitandani wakiangalia DVD.

  Mazungumzo yao yalipelekea Saada kuzungumzia pafomansi mbovu ya William kwenye malavi davi na kupelekea William kukasirika sana.

  William alimdondosha chini Saada na baadae kumjeruhi kwa kisu mikononi huku akitishia kuikata mikono ya mke wake huyo aliyemleta toka Tanzania.

  Kesi ya William kumjeruhi Saada ilifikishwa mahakamani na wiki iliyopita ndiyo hukumu ilitolewa ambapo William alipatikana na hatia ya kufanya shambulio la kudhuru mwili na kuhukumiwa kwenda jela miezi 15.

  Mwanzo wa yote ilikuwa mwaka 2009 wakati William aliposafiri kuja Tanzania kuonana na Saada ambaye alimjua kupitia dada yake ambaye yupo Uingereza na kuanza kuwasiliana naye kwa kutumia email.

  Kukutana kwao kulipelekea kuanza kwa uhusiano wa mapenzi ambapo William alimualika Saada Uingereza ili pia aje akutane na dada yake. Ujio huo haukudumu muda mrefu kwani Saada alikamatwa akiishi Uingereza akiwa amepitiliza muda wake wa kuruhusiwa kuishi Uingereza. Alirudishwa Tanzania na maafisa wa uhamiaji wa Uingereza.

  William aliamua kutumia njia ya kumuoa Saada ili waweze kuishi pamoja Uingereza. William kwa mara nyingine alikuja Tanzania na kumuoa Saada mwezi januari mwaka jana na kuanza mikakati ya kumtafutia viza ili aruhusiwe kuishi Uingereza. Baada ya vipingamizi vya hapa na pale hatimaye Saada alipewa viza na kuwasili Uingereza mwezi mei mwaka jana.

  Saada aliishi pamoja na William kwenye nyumba ya juu katika ghorofa linalomilikiwa William ambapo mke wa zamani wa William alikuwa akiishi nyumba ya chini.

  Hatimaye mwezi mmoja baada ya kuhamia kwenye nyumba hiyo ndipo sakata hilo lilipotokea na kupelekea Saada abaki na makovu kwenye mikono yake.

  Akijitetea kabla ya kuhukumiwa kwenda jela miezi 15, William aliiambia mahakama kuwa kesi hii ilipangwa na mkewe ili aweze kumkimbia aendelee kuishi Uingereza.

  Mahakama ya York Crown Court ilimuona William ana hatia ya kumshambulia mkewe kwa kisu cha urefu wa inchi 12 na kumhukumu kwenda jela.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3, align: center"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [/TR]
  [/TABLE]
  chanzo: Mrembo wa Tanzania Aolewa na Kibabu cha Kiingereza, Anusurika Kukatwa Mikono Yake
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  daaahhh
  hii inatisha.
   
 3. Kyaratu

  Kyaratu Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mmmmmmmh
   
 4. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  hajalipwa huyo dada? ...nao wamezidi kutaka utajiri wa haraka haraka ...nyambaafu
   
 5. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  pole zake tamaa mbele
   
 6. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Babu na pafomansi mbovu kitandani lakini pafomansi ya ubabe imekaa njema, duh!...
   
 7. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Angekatwa 2 maana mabinti wa sasa wanapenda mkwanja sana m2 wangu kuliko hata penzi lenyewe.
   
 8. h

  happy robert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hellow!duuh bonge la noma jaman njaa hizi ni probleeem
   
 9. dazipozi

  dazipozi JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 1,143
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hahahahaha makubwa ila yote njaaa
   
Loading...