Mrembo Maarufu wa Mavazi ya Kike Kumbe ni Mwanaume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrembo Maarufu wa Mavazi ya Kike Kumbe ni Mwanaume

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 14, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Ukimwona akiwa katika maonyesho ya vivazi vya ndani vya wanawake unaweza usiamini kuwa huyu mwanamke unayemuona sasa miaka 10 iliyopita alikuwa ni mwanaume kamili. Hata mpenzi wake wa kiume alikuwa hajui mwanamke aliyekuwa akijivinjari naye alikuwa ni mwanaume kamili miaka 10 iliyopita. Mrembo wa maonyesho ya vivazi vya ndani vya wanawake wa Uingereza, Lisa Du Preez mwenye umri wa miaka 35 ametoboa siri yake kwamba miaka 10 iliyopita alikuwa ni mwanaume kabla ya kufanya upasuaji wa kubadilisha jinsia yake.

  "Nilitaka watu waamini kuwa mimi nilizaliwa kama mwanamke ili niweze kuwavutia wanaume wengi na kutembea nao. Lakini hivi sasa nipo tayari kusema ukweli watu wajue hali yangu halisi" alisema Lisa akiongea na gazeti la News of The World la Uingereza.

  Kwa jinsi anavyovutia akiwa katika viguo vya ndani vya kike na matiti yake saizi 34DD makampuni mengi ya matangazo yamekuwa yakimwajiri kwenye matangazo yao bila kujua kuwa mwanamke huyo zamani alikuwa ni mwanaume aliyejulikana kwa jina la Louis.

  Kwa jinsi operesheni yake ya kubadilisha jinsia ilivyofanyika kwa mafanikio hata mpenzi wake ambaye ni fundi umeme alikuwa hajui kuwa mwanamke anayetembea naye alikuwa ni mwanaume miaka 10 iliyopita hadi siku mwanamke-mwanaume huyo alipompigia simu na kumwambia ukweli.

  Lisa alianza kuwa na tabia na kujiremba kama mwanamke alipokuwa na umri wa miaka saba baada ya kuvutiwa na vipodozi vya dada yake.

  Lisa alianza kupenda kujiremba kama mwanamke wakati huo na alikuwa akipenda aonekane kama mwanamke na kupelekea wenzake shuleni wamzomee na kufikia hata wanafunzi wenzake wa kiume kuogopa kubadilisha nguo zao mbele yake.

  Alipofikisha umri wa miaka 22 alianza kutumia madawa na kudungwa sindano za kuongeza homoni za kike. Na wakati huo alianza kujiunga na klabu za mashoga.

  Mwaka 1999 alifanya operesheni ya kubadilisha jinsia na kuzibadilisha nyeti zake ili aweze kufanya mapenzi kama mwanamke.

  "Wakati nilipokutana na mchumba wangu John Ward mwaka uliopita kwenye baa tulipendana ghafla lakini sikumwambia chochote kuhusiana na operesheni yangu niliyofanya" alisema Lisa.

  "Tulitongozana kwa wiki kadhaa, tukibusiana na kukumbatiana lakini baadae nilipoona uhusiano wetu umekuwa mkubwa sana niliona kuwa inanibidi nimwambie ukweli".

  "Niliona njia rahisi ni kumpigia simu na kumwambia ukweli" alisema Lisa.

  John kwa upande wake alisema kuwa awali baada ya kuambiwa ukweli huo alibaki ameduwaa asijue la kusema lakini baadae aliamua kumkubali Lisa kama alivyo.

  "Tunapendana na tunategemea kufunga ndoa hivi karibuni" alisema John.

  "Najua kuwa siwezi kupata mimba wala kuzaa watoto lakini sijutii uamuzi wangu" alimalizia kusema Lisa.

  picha yake huyo Mrembo bonyeza hapa http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2495798&&Cat=7
   
 2. M

  MalaikaMweupe Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  du eh bwana eh!
   
 3. T

  Tolu Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
Loading...