Mrema wa TANROADS bado aendelea na majukumu

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
6,591
6,471
Mrema wa TANROADS bado aendelea na majukumu


na Mwandishi wetu


amka2.gif
WAFANYAKAZI wa Wakala wa Barabara Nchini wamestushwa na kitendo cha Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Ephraim Mrema, kuamua kutangaza nafasi mbalimbali za kazi huku akijua kuwa jukumu hilo si lake.
Licha ya kutangaza nafasi hizo, wafanyakazi hao wanashangazwa na taarifa ya serikali kukiukwa. Taarifa hiyo ilimtaka Mrema kukabidhi majukumu ya ofisi hiyo Novemba 2, mwaka huu, kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wakala huo (jina linahifadhiwa).
Hata hivyo siku chache baada ya taarifa hiyo, serikali ilitangaza nafasi ya kazi iliyokuwa ikishikiliwa na Mrema ambapo hadi sasa haijaeleweka mchakato wake uliishia wapi huku wafanyakazi hao wakifananisha na mchezo wa kuigiza.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake kwa sharti la kutotajwa jina, mfanyakazi huyo alisema kuwa kuna kitu kinachomfanya mkurugenzi huyo aendelee kujiamini ndiyo maana amefikia uamuzi wa kutangaza nafasi hizo za kazi bila wizara kufahamu.
Alisema tangazo la kazi lililotolewa na Mrema Novemba 25 mwaka lilitangaza nafasi mbalimbali za kazi zikiwemo za mameneja wote wa mikoa na wakuu wa idara nyeti wa makao makuu.
Alisema nafasi za mameneja ni za mikoa 25, mkaguzi wa ndani, mwanasheria, wakurugenzi watano wa mipango, miradi, matengenezo, manunuzi na biashara.
“Miezi michache Mrema aliwahi kutangaza nafasi za kazi lakini kulitokea msuguano katika ofisi zote za Tanroad nchini lakini sasa amerudia tena …yaani hatujui nguvu hii anapewa na nani,” alihoji.
Katika taarifa ya notisi ya barua ambayo Mrema alipewa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, ilibainisha kuwa Mrema anapaswa kukamilisha taratibu za kukabidhi ofisi mapema ili kutoathiri shughuli za uendeshaji wa wakala huyo.
Kwa mujibu wa barua yake ya uteuzi ya Mrema ambaye tangu aingie madarakani amekuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali, alitakiwa kutumikia nafasi hiyo hadi Juni 3 mwaka huu.
Hata hivyo, katika mazingira ya kutatanisha zaidi, Mrema alisaini kutumikia nafasi hiyo kwa miaka mitano hadi Juni 3, 2012 na mkataba wake ulisainiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu, Enock Bukuku.
Katika kipindi cha uongozi wake, Mrema amekuwa akilalamikiwa kukiuka maagizo ya wakubwa zake, akiwemo aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, huku akidaiwa kutumia jina la Rais Jakaya Kikwete vibaya kwamba anamkingia kifua asifukuzwe.
Anadaiwa kukiuka majukumu yake kwa kuteua mameneja wa mikoa na wilaya bila kuthibitishwa na bodi na kupuuza maagizo na ushauri wa Waziri wa Miundombinu kuacha kufanya hivyo, huku akidai kuwa amepewa idhini ya kufanya hivyo na Rais Kikwete. source: TANZANIA DAIMA

SEKTA YA UJENZI INA HALI NGUMU.....niliwahi sema kuwa hatafanywa chochote
 
Back
Top Bottom