Mrema umeanza na kasi ambayo sio yenyewe,ungewachia wahusika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrema umeanza na kasi ambayo sio yenyewe,ungewachia wahusika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibona Dickson, Mar 8, 2011.

 1. Kibona Dickson

  Kibona Dickson Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Augustino Lyatonga Mrema,Mbunge wa jimbo la Vunjo na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali ya mitaa,ameanza kwa kishindo ambacho sio chenyewe na kudhihirisha jinsi asivyojua mipaka ya wajibu wa kamati ya bunge anayoiongoza.
  Magazeti kadhaa nchini yameripoti juu ya kile kilichojiri katika halimashauri ya wilaya ya same wakati Mrema na kamati yake wakikagua hesabu
  Kwa mjibu vyanzo vya habari,Mrema na kamati yake walikagua hesabu za halmashauri ya same kama kawaida "walikutana na madudu ya hesabu yaliyokuwa yanawasilishwa na DED" kitabu cha Taarifa alichokuwa anakisoma DED ni tofauti kabisa na yaliyomo ndani kitabu cha CAG,jambo ambalo liliashilia si tu kukosa umakini kwenye za umma na uzembe, bali harufu uwizi na ubadhirifu.
  Nimpongeze bwana Mrema na kamati yake nzima kwa uchungu, hali kadharika kwa umakini waliounyesha katika kulinda mali za wananchi,umakini na moyo huu viendelezwe hata katika maeneo mengine.
  Lakini wakati Kamati ya hesabu za serikali za mitaa ikianza kwa kuonyesha makali yake na kutoa salamu kwa mabingwa wa kuchakachua hesabu nitoe angalizo.
  Huko same Mrema na kamati wameagiza "DED na wenzake wakatwe mishahara asilimia kumi na tano kuziba kile kiasi kinachopungua kwenye.
  Nakiri kwamba wahusika katika hesabu za halmashauri ya Same wanastahili adhabu.Wasiwasi wangu ni uhalali wa Mrema na kamati yake kukata mishahara ya watumishi.Mshahara wa mtumishi unaweza kukatwa na mwajiri
  Mwajiri wa DED na wenzake sio mrema wala kamati ya bunge.Mrema na kamati yake wangependekeza adhabu na utekelezaji wake wangewaachia wahusika,au kwa hatua zaidi wangewaachia wahusika."MREMA NA WENZAKO KILA LA HERI, LAKINI NI VEMA MKAZINGATIA MIPAKA YA WAJIBU WENU"
   
 2. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwa jinsi nchi inavyopelekwa kipumbavu mimi naona wakatwe mishahara tu. Hana adabu hawa mafisadi. Mimi niko tayari kushirikiana na watu wanaotetea maslahi ya wananchi bila kujali itikadi na historia yao.
   
 3. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hiyo adhabu ni sahihi ila nani anastahili kuitoa ndio tatizo. I am sure hiyo siyo kazi ya kamati ya bunge. Wao walitakiwa wa propose adhabu then TAMISEMI ndo wangeitoa.

  Nadhani wabunge hawajapata semina ya kutosha wakiwa kwenye kamati zao
   
 4. Kibona Dickson

  Kibona Dickson Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na wewe.
   
 5. Kibona Dickson

  Kibona Dickson Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na hoja yako
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,899
  Trophy Points: 280
  Nadhani kila mtu anakubaliana na watumishi kama hao kupewa adhabu,ila hoja ni kuwa kamati ya Bunge inastahili kutoa au kupendekeza adhabu?
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  atakuwa na hasira na babu wa loliondo
   
 8. p

  police Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mrema uko juu. mbona wakati dr. slaa anaongoza kamati hii kulikuwa kimya. mrema mwezi tu tumesikia same na rombo. court system yetu inatetea mafisadi, wakatwe mishahara tu.
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Assumung Mhe Mrema na kamati yake wanaruhusiwa kuchukua nafasi ya mahakimu, hivi, iwapo mtu kajichotea mapesa katika halimashauri, jee kukatwa mshahara ni adhabu tosha?
   
 10. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  HOJA YAKO IMEELEWEKA SANA.:ranger:
   
 11. LD

  LD JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Good Mrema!!!
   
 12. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hoja hapa ni kuwa kamati ya bunge inamamlaka ya kukata mishahara ya watendaji wa serikali? Sio unasupport kila kitu kisa kimefanywa na mtu ambaye hamuungimkono mpinzani wako DKT SLAA, unajua kuwa mshahara ni haki ya mtumishi na ili mtumishi akatwe mshahara wake ni hadi sheria ibainishe wazi kuwa kosa alilolifanya adhabu yake ni kukatwa mshahara. Tunarudi kulekule watumishi wa umma wakishutumiwa kutenda kosa wanapewa siku saba za kumuona DKT MREMA tena kwao kiraracha wakiwa na utetezi wao. Mambo yamebadilika sana miaka ya leo nchi inaongozwa kwa misingi ya sheria msije kesho mkamcheka baada TAMISEMI kutotekeleza agizo hilo na kamati yake ikakosa la kufanya.
   
 13. e

  emalau JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kama mishahara inaweza kutosheleza malipo hayo definitely pesa iliyoliwa ni kiduchu, kama ni mamilioni hiyo mishaharai tatosha nini kama sio tone baharini. For great thinkers that is not the right move, according to the rule of law, governing is divided into executive, parliament and judicially,In this regard Mrema has crossed the red line, the duty of sanctioning punishment should be left to its respective branch of governing which is judicially.
   
 14. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  mrema baba waonyeshe kazi. daktari wa wakatoliki alikuwa anachukua posho na kuiba siri ili arushe mabomu ccm hakutaka kutatua tatizo.

  baba songa mbele nyuma twakusukuma. mrema uko juu asilimia 28 ya kura rekodi yako inapeta. daktari wa kwalesma anaisikia redioni.
   
 15. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Tatizo lako hukubahatika kujua jinsi Dr. Slaa alivyokuwa kauzu kwenye LAAC. Kama kuna kitu wakurugenzi, Wakuu wa idara na watendaji mbalimbali wa serikali za mitaa walishangilia katika maisha yao ya utumishi ni Pale waliposikia Dr. Slaa hagombei ubunge. Tuulize sisi tuliowahi kuingia kwenye hiyo Kamati kipindi ambacho Dr. Slaa alikuwa Chair, wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali walivyokuwa wanahaha utadhani wanaingia kwenye mtihani, na wakiingia ndani walikuwa wanatetemeka sio mchezo Dr. alikuwa very critical kwenye kuhoji na ukijichanganya tu unakatwa mshahara, au kushushwa cheo. Na waliofanya vizuri katika kujibu walikuwa wanapewa promotion
   
 16. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ugomvi wako na DKT SLAA unayemuita wa kwaresima mimi haunihusu, cha msingi ninacho kushauri usishangilie pale DKT MREMA anapoongoza kamati yake na kufanya uvunjifu wa sheria ya utumishi wa umma ya 2002 na sheria ya kazi 2004 kwa kukata mishahara ya watumishi bila kuzingatia sheria hizo. Kumbuka mshahara ni hakiyao ya msingi kama wamechakachua sheria zipo, polisi na takukuru wapo wafanye kazi yao, tabia hizi za kutoa adhabu za papo kwa papo kinyume cha sheria kitalivunjia bunge hadhi yake na serikali kama itatekelaza maana wajiandae kwenda mahakamani ktk masuala ya haki za wafanyakazi na raia si sehemu ya kujitengenezea umaarufu wa kisiasa
   
 17. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wakubwa kilichotokea Same ni hiki: Kwanza taarifa ya LAAC iliyopelekwa kwa CAG ilikua na mapungufu ya fuatayo - Kiasi cha fedha cha miradi katika muhtasari kilikua kidogo ukilinganisha na michanganuo ya matumizi. Yaani matumizi yalionekama makubwa kuliko fedha zilizopokelewa. Pili kiasi cha fedha zilizooneshwa kupokelewa kwenye muhtasari wa taarifa ya LAAC kilionekana kuwa kidogo ukilinganisha na kiasi kilichooneshwa kwenye final accounts. Kwa hiyo tatizo kubwa lilikua ni uandaaji mbovu wa taarifa. Lakini kinachonishangaza, moja ya kazi muhimu za kamati hiyo ni kuangalia value for money ambayo wajumbe wa kamati hawakuifanya wakati wa ukaguzi wao. Wao baada ya kukutana na taarifa mbovu ya LAAC waliamua kuconclude kunaubadhilifu. Mimi naamini value for money haiangaliwi kwenye vitabu. Taarifa inaweza kuwa nzuri na miradi ikawa hoyo kabisa!!! Vilevile uandaaji mbaya wa taarifa hauna maana hakuna value for money katika miradi. Inaweza ikawa ni uzembe tu katika uandaaji wa taarifa. Value for money inajulikana kwa kukagua miradi physically, kitu ambacho Mrema na wenzake hawakukifanya!! Kwa upande wangu mimi naona hawakutenda haki wala kuwajibika ipasavyo! Watumishi wa Same wanastahili adhabu kwa uzembe wa kuandaa taarifa mbovu. Kamati inastahili adhabu gani kwa kutokukagua value for money ya miradi ya maendeleo?? Vipi kama huko kwenye miradi kunauozo zaidi ya huo waliouona??? Kwa kifupi utendaji wa kamati hii kama ndo utakua hivi, mimi hauniridhishi hata kidogo!!! Huo ni mtazamo wangu tu wakubwa.
   
Loading...