Mrema: Ubunge mtamu, siuachii ng’oo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Wednesday, 29 February 2012 08:32

Pamela Chilongola na Keneth Goliama

MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour Part (TLP ) Augustino Mrema amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuwa na uvumilivu na kiwango cha mshahara wa wabunge wanachokipata.Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake jana, Mrema alisema wabunge wanatakiwa kuogopa kutawaliwa na tamaa ya fedha katika kuongoza wananchi.

Mrema alisema wabunge hawahitaji kuwa mamilionea katika kuwasaidia wananchi bali kuna miradi mbalimbali kama mfuko wa jimbo na kufungua miradi ya maana katioka kuinua uchumi wa wananchi.

"Ni kweli fedha tunazolipwa hazitoshi lakini tunatakiwa kuvumilia na kuendelea kuongoza maana hata ukipewa Sh10 milioni haziwezi kutosha iwapo mbunge hatakuwa na matumizi ya mipango thabiti," alisema.
Mrema alisema kinachoongelewa na Spika Makinda ni kweli lakini mbunge anatakiwa kuweka bajeti katika kuendesha jimbo lake.

Alisema kama wabunge wanataka kuondoka kwa ajili ya kukosa posho na mishahara waende lakini kwa yeye hawezi kuondoka kutokana na kiwango hicho kumtosha sana.

"Nimekaa zaidi ya miaka 20 bila kupata chochote, niliweza kuwasaidia wananchi wangu licha ya kujiuzulu uwaziri wangu, sasa kwanini leo niachie hata hiki kidogo siwezi kukiachia ng'oo! Haachii ngazi mtu hapa," alisema mrema.
Alisema hakuna mbunge ambaye ataweza kuachia ngazi kwa ajili ya mshahara kuwa mdogo kutokana na kwamba kazi ya ubunge sio fedha bali ni kujituma kwa wananchi.

Marema alisema Spika Makinda hatakiwi kulaumiwa kutokana na wabunge wachache waliongia bungeni kwa ajili ya kutafuta fedha humfuata na kumueleza matatizo yao."Spika makinda ni halalali kueleza kutokana yeye kuwa mama wa wabunge wote wa kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi," alisema.

Uteuzi wa mgombea Arumeru Wakatai huo huo chama cha TLP kimetangaza kusimamisha mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru mashariki.

Mrema alisema chama kimempitisha Abraham Mhoza Chipaka kupeperusha Bendera ya TLP . Alisema kamati ya halmashauri ya wilaya ya chama hicho ilimpitisha Mgombea huyo kwa kuona nafaa kukiwakilisha chama.
"TLP tumejipanga kugombea Arumeru Mashariki tutaenda kugombea na sio kusindikiza kama wanavyofikilia"alisema na kuongeza:

"Tumemsimamisha Abrahamu Chipaka ambaye ni mjasiliamali amepitishwa na kamati ya Halmashauri ya Wilaya Taifa"alisema Mrema. Mrema alisema anafurahishwa na migogoro inayoendelea ndani ya chama cha CUF na NCCR mageuzi kwa kile alichodai kuwa aliambiwa yeye ni dikteta na kufukuza viongozi katika chama alichokuwa akikiongoza.

"Uongozi ni mgumu wanatakiwa wajifunze kupitia vyama vingine wasibaki kushabikia na kuniona mimi ni dikteta kazi yangu ni kuwafukuza wanachama wenzangu,sasa kikowapi leo hii yamewageukia wao"alisema Mrema. Alisema suala la watu kumnyemelea ili kumuondoa uenyekiti hakubaliani nao kwa kuwa huyo anayetaka kuchukua nafasi hiyo anasifa yeyote kuwa mbunge.


 
Inatisha kweli, ubepari umemuingia utamu wake ameuona hauachii...

Inatisha kweli, Hadi Mrema hajali uongozi tena anayajali marupurupu ya Uongozi...
 
WAMEM MWAKYEMBE MEKU PolE SANA ,WEWE HAWAKUPELEKI APOLO KAMA ZITTO???​
 
Back
Top Bottom