Mrema: Maalim Seif anafanya uhaini yafaa achukuliwe hatua haraka

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Vunjo Augustino Lyatonga Mrema amesema katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF anafanya uhaini

amesema anataka kuingia madarakani kinyume na taratibu za nchi na jambo hili watu wasilichukulie kama jambo dogo na anaongea kwa uzoefu wake kama waziri wa mambo ya ndani wa zamani
Amesema pia ni mbinafsi na anataka kuingia madarakani kwa gharama zozote na watanzania wacha mungu hawakubaliani na hatua lazima zichukuliwe

 
Aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Vunjo Augustino Lyatonga Mrema amesema katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF anafanya uhaini

amesema anataka kuingia madarakani kinyume na taratibu za nchi na jambo hili watu wasilichukulie kama jambo dogo na anaongea kwa uzoefu wake kama waziri wa mambo ya ndani wa zamani
Amesema pia ni mbinafsi na anataka kuingia madarakani kwa gharama zozote na watanzania wacha mungu hawakubaliani na hatua lazima zichukuliwe


ahahaha,shikamoo mbatia!
 
Mrema karibu Dar vipi wapiga kura wako wa Vunjo hawajambo? Habari za hapo JOGOO HOUSE Magomeni?
 
Mrema yupo sawa kabisa huyu Maalim Seif mahaba ya waZnz yanafanya wasione uhalifu anaofanya.. Huyu anakufa na CUF maana CUF wamemgeuza mungu wao hakifa na wao kwa heri.
Sasa kosa la Maalim Seif liko wapi hapo, hadi kuitwa mhaini?
Wahaini ni hao wanaojifanya kujipendekeza wabaki kwenye siasa huku dhamira yao ikiwa tofauti
 
Huyu mzee njaa tu zinamsumbua,uhaini uliofanywa na ccm zanzibar hakuuona?
Huyo Mrema anajipendekeza kwa CCM ili Magu amkumbuke kumpa ubunge wa viti maalum katika zile nafasi zake 10.

Si mnakumbuka mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu, Magu alipopita kule Vunjo alimpigia kampeni Mrema badala ya kumpigia debe mgombea wake wa CCM?!

Hivi kweli Mrema hamwogopi Mungu kwa kutambua ukweli kuwa anayestahili kushitakiwa kwa uhaini ni Jecha 'aliyepindua' matokeo halali ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 na si Maalim Seif, ambaye anaeleza ukweli mtupu kuwa Shein yupo madarakani kwa kuwekwa na vyombo vya usalama na siyo kwa ridhaa ya wananchi wa Zenji?
 
Maalim Seif ni mhaini soon atachukuliwa hatua!
Wewe kada wa CCM, wakati mwingine jaribu kumwogopa Mungu na kuutambua ukweli.

Hivi kiuhalisia ni nani hasa anastahili kushitakiwa kwa makosa ya uhaini kati ya wale vijana wenu wa UVCCM waliopita na mabango yao ya ubaguzi wa kutisha, yaliyosomeka CHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI YA WAAFRIKA PEKEE na Maalim Seif anayesema ukweli mtupu kuwa Jecha 'aliagizwa' na viongozi wahafidhina wa CCM kuyafuta matokeo halali ya uchaguzi huru uliofanyika tarehe 25/10/2015, baada ya kubaini kuwa Shein ameangukia pua?
 
Huwa ninabaki kinywa wazi kwa mtu aliyekaa madarakani muda wote na kupata marupurupu makubwa kushindwa kuendeleza maisha yake kwa kipato chake alichopata bali kutaka kuendelea kusubiri nafasi za uteuzi tu ili ale kwa ulaini. Hii inaonyesha pindi unapopata nafasi ya kula katika nchi hii ni kama unashikiwa akili na uwezo wa kujiamini katika kujitegemea hivyo namna pekee ni kujipendekeza tu.
 
Mzee pumzika ulee wajukuu,wakati matokeo yanafutwa kimizengwe mbona hukuongea?Asante Mbatia
 
mrema angekuwa kama pinda tu, siasa huku analima, siasa zikikutema bado una kitega uchumi chako, mzee amebaki kuishi kweye past glories tu, eti waziri wa mambo ya ndani niliyepita
 
Back
Top Bottom