Mrema, Lipumba, Slaa, Lowassa na mustakabhari wa vyama vingi;

dux limit

Senior Member
Jul 28, 2015
143
55
Ilikuwa ni mwaka 1993 ndipo kwa mara ya kwanza nilipohudhuria mkutano wa kiongozi wa chama cha upinzani, ulikuwa ni mkutano wa Chama cha UMD, kipindi kile umri wangu nilikuwa bado ni kijana mdg na kila mtu tulipokuwa tunarudi majumbani alikuwa anamsifia kiongozi wa UMD kutokana na jinsi alivyohutubia. Baadae nilibahatika kuudhuria mkutano mwingine, huu ulikuwa ni mkutano wa CHADEMA hapa namkumbuka kiongozi wa chama alikuwa ni Edwin Mtei, akiwa na BOB Nyange Makani wakiwa na kijana mmoja naye ni Freeman Mbowe, Mtei alieleza mambo mengi sana na mimi nilijaribu kufatilia mkutano ule kwa umakini lkn ilikuwa ni vigumu kuelewa nini hasa kilikuwa kinatafutwa kwani sikujua utofauti wa CCM na vyama vile kutokana na umri wangu kuwa mdogo! Baada ya hapo kikafuata NCCR-Mageuzi, kikiwa na viongozi kama Mabere Nyaundo Marando, Dr. Lamwai nk. Baadae alikuja James Mapalala ambae alikuwa kiongozi mkuu wa CUF.

Lakini kwa kipindi kile chama kilichokuwa na nguvu hadi 1994 kilikuwa ni UMD, lkn upepo ulikuja kubadirika ghafla pindi Agustino Lyatonga Mrema alipohama toka CCM na kujiunga na upinzani ktk chama cha NCCR-Mageuzi. Kipindi hicho ilikuwa ni vigumu sana kuweza kuudhibiti upepo wa Mrema kwa kutegemea nguvu ya hoja ama sera za chama fulani, nakumbuka kipindi hicho uwanja wa Sokoine mjini mbeya ulishindwa kuhimili wingi wa watu na kulazimisha mkutano kufanyika nje ya uwanja.
Hii hali ndio inayonifanya nimpongeze sana Kamanda Freeman Mbowe kwa kubadiri gear kwani yeye akiwa ni mmoja wa vijana walioshuhudia nguvu ya Mrema ilivyovipoteza vyama km UMD na kuifanya NCCR kuwa na nguvu zaidi kutokana na Mrema. Lkn kuna baadhi ya watu huwa wanapuuza maamuzi ya mbowe ambayo yalikuwa ni sahihi na yataendelea kuwa sahihi na yenye tija na manufaa kwa CDM.
Hivi mbowe angegoma kumpokea Lowassa na hivyo Lowassa angejiunga na chama kingine cha upinzani mfano ACT, hivi chadema ingekuwa na nguvu km iliyokuwa nayo ktk uchaguzi 2015 ? Kumbuka kwamba ACT ya kipindi kile adui yake mkubwa alikuwa ni CHADEMA na si CCM! Hlf ongeza na hasira za Lowassa juu ya kuchafuliwa mda mrefu na viongozi wa upinzani? Ni wazi kabisa CDM isingeweza kupata idai kubwa ya viti na kufikisha kura mil 6.07 ktk nafasi ya urais kulinganisha na maamuzi ya mbowe kwa Lowassa.
Kumbuka kwamba Dr. Slaa hakuwai kuwa chaguo la CHADEMA ktk nafasi ya urais hata mwaka 2010 aliteuliwa yeye baada ya Samwel Sitta kuitosa CHADEMA ktk hatua za mwisho kama tetezi zilivyokuwa zinasikika, kwa hiyo ni kwamba Dr. Slaa hakuwai kuwa chaguo la CDM ktk nafasi ya urais, bali aliwekwa baada ya kumkosa mtu sahihi na si kwamba alikuwa na sifa....! Hii ni km ilivyotokea kwa Mama Anna Mgwira yeye pia hawezi jipambanua kuwa alikuwa mtu sahihi ndani ya ACT kwa nafasi ya urais.
Hivi kati ya Mrema, Lipumba, Slaa na Lowassa ni nani aliye leta changamoto na mtikisiko mkubwa ndani ya CCM baada na kabla ya uchaguzi? Kwani Mrema, Lowassa na Slaa wote wamehama toka CCM, na ni kwamba Mrema na Lowassa walihama wakiwa na nguvu kitaifa lkn Slaa alihama akiwa ananguvu ya jimbo.

Linapokuja suala la maslahi mapana ya chama cha CHADEMA siku zote Mbowe ni mtu muhimu na sahihi sana na ktk hili ata ukimfata Mzee Wassira ama Yusuph makamba watakueleza.
 
Back
Top Bottom