Elections 2010 Mrema, CUF ni CCM!

skeleton

Member
Aug 17, 2010
60
3
Jamani mmeskia jinsi mh. Mrema anavyomfagilia JK kuwa matokeo ni ya halali na hivyo Dr Slaa hana budi kuyakubali na wapinzani wasiyabeze matokeo hayo. Anasema JK amewaacha kwa mbali wapinzani wake na hivyo ni rais halali!

Hivi kweli kichwani zipo au hamnazo? Ni bora hata Mrema asingejiuzulu uwaziri enzi zake, maana anaitamani CCM, kurudi anaona aibu! Na Lipumba nae hivyohivyo anajibaraguza kwa JK hadi kumpa ilani yake ya uchaguzi.

Kinachonikera na kinachonifanya niwaone TLP na CUF na vyama vingine (ukiondoa CHADEMA) ni wasaliti ni kumkubali mchakachuaji. Sasa je, Tanzania hii kuna upinzani au wapinzani wanaingia kwenye vyama vya siasa kwa lengo la kuganga njaa? Sasa chama pekee cha upinzani kwangu mimi ni CHADEMA peke yake.

Eh Mungu naomba usimfanye na Dr Slaa nae akabadilika hapo badae na kuwa kama CUF, TLP, n.k kwani sisi wanyonge tutakuwa hatuna kimbilio na tutakuwa tumekwisha!
 
Vyama vya upinzani vyote vilivyobaki ukiondoa Chadema ni CCM huo ndo ukweli ingawa unauma
 
Vyama vya upinzani vyote vilivyobaki ukiondoa Chadema ni CCM huo ndo ukweli ingawa unauma

Mimi nina mawazo tofauti kidogo. Nionavyo mimi vyama vyote vya upinzani ni vya upinzani isipokuwa CHADEMA hawa ni CCM tu..ndio maana viongozi wake waandamizi walipokwenda CCM walipewa ahsante kubwa tu..start with Amani Kaburu..........
 
Jamani mmeskia jinsi mh. Mrema anavyomfagilia JK kuwa matokeo ni ya halali na hivyo Dr Slaa hana budi kuyakubali na wapinzani wasiyabeze matokeo hayo. Anasema JK amewaacha kwa mbali wapinzani wake na hivyo ni rais halali!

Hivi kweli kichwani zipo au hamnazo? Ni bora hata Mrema asingejiuzulu uwaziri enzi zake, maana anaitamani CCM, kurudi anaona aibu! Na Lipumba nae hivyohivyo anajibaraguza kwa JK hadi kumpa ilani yake ya uchaguzi.

Kinachonikera na kinachonifanya niwaone TLP na CUF na vyama vingine (ukiondoa CHADEMA) ni wasaliti ni kumkubali mchakachuaji. Sasa je, Tanzania hii kuna upinzani au wapinzani wanaingia kwenye vyama vya siasa kwa lengo la kuganga njaa? Sasa chama pekee cha upinzani kwangu mimi ni CHADEMA peke yake.

Eh Mungu naomba usimfanye na Dr Slaa nae akabadilika hapo badae na kuwa kama CUF, TLP, n.k kwani sisi wanyonge tutakuwa hatuna kimbilio na tutakuwa tumekwisha!

Nadhani kuna PICHA watanzania HATUTAKI KUIANGALIA:
VYAMA NA WAPINZANI WOTE NCHI HII WANAFANANA WANACHOTOFAUTIANA NI TAREHE TU, TUACHE MAPENZI YALIYOPITILIZA KWA BAADHI YA VYAMA NA VIONGOZI KWA SABABU KILA MMOJA ANAJIJUA MWENYEWE NAFSI YAKE.
UNAPASWA KUJIAMINI MWENYEWE NA SI KUMUAMINI MWINGINE YEYOTE:

NINAKUNUKULIA TENA HAPA HABARI HII JAPO INAUMIZA MOYO:smile-big::

2005:

Mgombea
Chama
Kura
Asilimia
Anna Senkoro
PPT Maendeleo
18783
0.17%
Augustine Mrema
Tanzania Labour Party
668756
0.75 %
Christopher Mtikila
Democratic Party
31083
0.27%
Emmanuel Makaidi
National League for Democracy
21574
0.19%
Freeman Mbowe
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
668756
5.8%
Ibrahim Lipumba
Chama cha Wananchi
1,327125
11.68%
Jakaya Kikwete
Chama Cha Mapinduzi
9,102,951
80.28%
Dr.Sengondo Mvungi
NCCR-Magaeuzi
55819
0.43%
Prof. Leonard Shayo
Demokrasia Makini
17070
0.15%
Henry Kyara
Sauti ya Umma
16414
0.14%
Kura Zilizoharibika
Tanzania Daima:

Mbowe: Sijashindwa

Na Mwandishi Wetu
Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Desemba 14, Watanzania walimchagua Jakaya Kikwete wa CCM kuwa rais wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Mbowe alisisitiza kwamba mageuzi yanayotafutwa, na ambayo yeye na wenzake walikuwa wakiyapigania wakati wa kampeni za kugombea urais, si ya kubadili sura za viongozi, bali mfumo.
Akizungumzia hatua yake ya kukubali matokeo ya uchaguzi, na hata kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Kikwete wakati wapinzani wengine wamesusa, Mbowe alisema kususa si mbinu yake ya kisiasa.
Alitoa mfano wa baadhi ya wanasiasa wa upinzani ambao wamekuwa wakisusia na kukataa matokeo ya uchaguzi tangu mwaka 1995, akasema mbinu hiyo haikuwawezesha kuidhoofisha CCM.
Alisema wakati wapinzani wameendelea kusema hawamtambui Rais Benjamin Mkapa (aliyestaafu wiki hii) hawakuweza kumzuia kuwaongoza kwa miaka 10.
Kwa sababu hiyo, alisema yeye na chama chake wameona ni vema kufanya siasa za kisasa, za kistaarabu na kiungwana kwa kuwa hata walipokuwa wanaingia kwenye ushindani, walijua kuwa kuna kushinda na kushindwa.
Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za nchi, hata kama mshindi kapatikana kwa njia zisizo sahihi, akishatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hakuna anayeweza kuhoji mahali popote.
Mbowe alikuwa wa tatu nyuma ya Profesa Lipumba wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Jakaya Kikwete wa CCM aliyeapishwa kuwa rais wiki hii.
Mbowe amekuwa mmoja wa viongozi wachache wa upinzani waliokubali kushindwa na walioshiriki sherehe za kuapishwa kwa rais mpya katika Uwanja wa Taifa wiki hii, huku baadhi ya wanajamii wakimsifu kwa ujasiri na ukomavu aliouonyesha wakati vyama vingine vya upinzani vikisusa.
Wengine waliojiunga na Mbowe katika hilo ni Paul Kyara wa Sauti ya Umma (SAU) na Anna Senkoro wa PPT-Maendeleo.
Gazeti-Tanzania Daima
ISSN 0856-9762
Tarehe: Jumapili Desemba 25, 2005
 
Unafiki mwingine wa wapinzani. Halafu mnazungumzia kuungana! Kuungana kwa lipi? Kwa kuwa wote mko upinzani au? Upuuzi mtupu.. CHADEMA kaza mwendo!
 
Back
Top Bottom