Mrema: CCJ ni matokeo ya kongamano la kina Butiku

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Na Waandishi Wetu

MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema amesema Chama Cha Jamii (CCJ) kimeanzishwa ikiwa ni matokeo ya kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere inayoongozwa na Joseph Butiku, ambaye ameyaelezea madai hayo kuwa "upuuzi".

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mrema alisema vigogo wa CCM waliozungumza kwenye kongamano hilo na kutamka wazi kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kufanya maamuzi magumu, ndiyo waanzilishi wa CCJ.

CCJ ni chama kipya cha kisiasa ambacho kuanzishwa kwake kunahusishwa na mkakati wa vigogo na baadhi ya wabunge wa CCM ambao hata hivyo hadi leo hawajajitokeza hadharani.

Mrema, ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kabla ya kutofautiana na mawaziri wenzake mwaka 1995 na kujiunga na chama pinzani cha NCCR Mageuzi, alidai kuwa ametumia mbinu zake za usalama wa taifa kuwatambua vigogo hao.

Bila kuwataja kwa majina, Mrema alisema vigogo hao wanatumia mwamvuli wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuandaa makongamano kwa nia ya ya kumtukana na kumhujumu Rais Kikwete.

"Wanatumia mwavuli huo kumtukana rais kwamba anazungukwa na wezi na kwamba hana maamuzi magumu wakati wenyewe hawana maamuzi hayo," alisema Mrema.

"Ni aibu kwa vigogo hao wa CCM tena wanaojifanya kuwa wapo chini ya mwamvuli wa Tasisi ya Baba wa Taifa kuandaa makongamano ya kumtukana rais wetu hadharani wakati wenyewe pia hawana mamuzi magumu na kama wanayo basi wajitangaze hadharani kuwa wao ndiyo CCJ," alisema Mrema.

Mrema, ambaye alikuwa nchini India kwa matibabu na ambaye alikanusha kuwa safari yake ilidhaminiwa na Kikwete, alisema: "Kumwambia rais maneno makali kama hayo tena hadharani ni kutaka wananchi wamdharau na kumwona mwizi pia na kimsingi huu ni uhaini.

"Nimetumia uzoefu wa taaluma yangu ya Usalama wa Taifa na kubaini machafu yanayofanywa na vigogo... simtetei Kikwete bali natetea rais yeyote wa taifa hili siyo Kikwete tu kama wanavyosema nipo kwenye mtandao wa Kikwete na wengine kudai kuwa nimenunuliwa.

"Kikwete hawezi kuninunua; mimi ni mtu wa gharama sinunuliki, ila kwenye ukweli panastahili kuzungumzwa; natumia taaluma yangu kutetea taifa, siwezi kuona taifa linayumba halafu nikae kimya; mimi na mkurugenzi mstaafu wa Usalama wa Taifa bwana."

Hata hivyo, hakueleza alikuwa mkurugenzi wa kitengo gani cha Usalama wa Taifa.

Mrema aliongeza kusema: "Siingii jikoni kupika, lakini nina utaalamu wa kupika. Ninataka wale vigogo wanaomhujumu rais kwa maneno ya kijeli, kama wana uwezo na kujiamini wajitokeze hadharani wasema wao ndiyo wenye CCJ."

Hata hivyo mwenyekiti wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alipuuza madai hayo ya Mrema akisema hawezi kuzungumzia upuuzi.

"Sitaki kuulizwa maswali yasiyo na maana; nenda kamuulize aliyekwambia upuuzi huo," alisema Butiku.

Katika hatua nyingine wakati Mrema akitoa tuhuma hizo nzito, CCJ imeanza mapambano kupigania usajili wake kwa kumhoji Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa sababu za kushindwa kuwapa usajili wa muda.

Tamko hilo la CCJ kwa Tendwa limekuja katika kipindi ambacho Msajili amekuwa akisisitiza kuwa uwezekano wa chama hicho kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 haupo kwa sababu muda hautoshi kwa chama hicho kukamilisha taratibu zote ili kipate usajili wa kudumu.

Usajili wa muda, ambao unahusisha chama kipya kitafuta angalau wanachama 200 kutoka mikoa 10 au zaidi, huchukua miezi sita ambayo hufuatiwa na uhakiki unaofanywa na Msajili kabla ya kupata usajili wa kudumu.

Tendwa alisema hata kama chama kipya kitakamilisha sharti hilo la kwanza katika muda mfupi, sheria ya miezi sita inabakia kama ilivyo.

Ndani ya kipindi hicho cha usajili wa muda na uhakiki, Tume ya Uchaguzi itakuwa imeshaanza taratibu za uchaguzi kwa kuruhusu wagombea waliopitishwa na vyama vyao kuanza kuchukua fomu.

Lakini uvumilivu uliwashinda CCJ ambao jana walimshukia Tendwa wakidai kuwa anadhofiisha mipango hiyo ya kukipa chama usajili wa muda kwa malengo anayojua mwenyewe.

Renatus Muabhi, ambaye ni katibu mkuu wa CCJ, alitoa tamko linalosema: "Hali iliyopo sasa imesababisha viongozi pamoja na wanachama watarajiwa wa CCJ kuwa katika hali ya utata na kuhofia mustakabali mzima wa upatikanaji wa usajili wa muda wa CCJ.

"Tunapata taarifa za maelezo ya msajili wa vyama vya siasa nchini yanayokinzana na wajibu wake kupitia vyombo vya habari pasipo sisi kuwa na taarifa yoyote inayoonyesha hatua ipi imefikiwa juu ya usajili wa CCJ.

"Kwa mfano, tarehe 26/01/2010 siku ya Jumanne gazeti la Daily News lilichapisha maneno ya msajili ambayo kwetu sisi yanatuingiza katika utata na hofu juu ya usajili wa chama chetu."

Tamko hilo linaendelea kueleza kuwa Tendwa anakwenda kinyume na taratibu pamoja na dhamana aliyopewa na kuhakikisha kwa vitendo ya kwamba nchi ya Tanzania ni ya kidemokrasia na inayofuata mfumo wa vyama vingi, badala ya kuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu kuunda na kujiunga katika vyama vya siasa ili kuleta demokrasia ya kweli.

Linamtuhumu Tendwa kuwa anakatisha tamaa na kuwavunja moyo Watanzania kuhusu tafsiri ya kuanzishwa kwa CCJ hasa pale anaposema chama hicho ni sawa na vyama vingine vilivyopo.

Habari hii imeandaliwa na Ramadhan Semtawa, Mussa Mkama na Minael Msuya.

SOURCE: Mwananchi
 
Na bado mpaka Chiligati afe kwa presha au kisukari
 
Waandishi Wetu

.... siwezi kuona taifa linayumba halafu nikae kimya; mimi na mkurugenzi mstaafu wa Usalama wa Taifa bwana." ...

Hata hivyo mwenyekiti wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alipuuza madai hayo ya Mrema akisema hawezi kuzungumzia upuuzi.
"Sitaki kuulizwa maswali yasiyo na maana; nenda kamuulize aliyekwambia upuuzi huo," alisema Butiku.

.

SOURCE: Mwananchi

Jamaa anazeeka vibaya.... kwa hiyo taifa linayumba kwa sababu ya kongamano la Taasisi ya mwalimu nyerere na ujio wa CCJ? huyu mzee vp?

Naona jibu la Butiku ni zuri sana - big up.
 
....Mmmmmmmh huu upinzani wa Mrema ni very questionable???
Tangu lini Mrema akawa mpinzani...sasa anajiibua mwenyewe kuwa ni pandikizi na boya la kuwaraghai watanzania. Hatujasahau kuwa enzi za utawala wa Mobutu kule Zaire alipandikiza makumi ya vyama feki vya upinzania!!!
 
Jamaa anazeeka vibaya.... kwa hiyo taifa linayumba kwa sababu ya kongamano la Taasisi ya mwalimu nyerere na ujio wa CCJ? huyu mzee vp?

Naona jibu la Butiku ni zuri sana - big up.

Msameheni mrema hajui Kiswahili taifa linayumba, wengine wanaona huo ndio mwelekeo unaotakiwa.
 
Tangu lini Mrema akawa mpinzani...sasa anajiibua mwenyewe kuwa ni pandikizi na boya la kuwaraghai watanzania. Hatujasahau kuwa enzi za utawala wa Mobutu kule Zaire alipandikiza makumi ya vyama feki vya upinzania!!!

Dr Nguza Karl-I-Bond ndio alikuwa 'Mrema' wake Mobutu
 
Mrema as a person is not credible at all.

Hapa ametumiwa kujaribu kuwadanganya watanzania.

Inafahamika kuwa Mrema anatumiwa na wanamtandao ili kuwasema vibaya wote wale ambao wana wasiwasi na utendaji wa Serikali ya Kikwete tangu iingie madarakani.

Kila binadamu, akiwemo Rais anaweza kukosolewa. Rais si malaika asikosee, na katiba inatoa uhuru wa kusema. Na wananchi wanatakiwa kuendelea kuyasema mazuri na mabaya pia.

Eti Mrema naye alitaka kuwa Rais!.. Duh!

Chama chochote kinapoanziswa kinahitaji kupata wanachama wengi iwezekanavyo, hivyo kinatakiwa kijitangaze na pia kutangaza viongozi waanzilishi wake, na kama wapo wanaofahamika zaidi basi inakuwa rahisi zaidi kupata wanachama wa kusaidia kufikiwa kwa idadi ya wanachama wanaotakiwa ili kuweza kukifanya kipate usajili wa kudumu.

Kuna sources zinasema kuwa CCJ ni creation ya Rostam, ni 'red herring' ili kuwafanya watanzania kuacha kufuatilia mambo muhimu yaliyopo kwa sasa kama Utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu mkataba wa kifisadi wa Richmond.
 
Kuna sources zinasema kuwa CCJ ni creation ya Rostam, ni 'red herring' ili kuwafanya watanzania kuacha kufuatilia mambo muhimu yaliyopo kwa sasa kama Utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu mkataba wa kifisadi wa Richmond.


I dont think so
 
Watanzania hatuhitaji kujua nani mwenye kuanzisha chama gani.Tunachohitaji uongozi bora utakaowapeleka watanzania kwenye maisha bora ya kugawana rasilimali za nchi kwa pamoja badala ya kuongeza gap ya tajiri na masikini. aje yeyote na Chama chochote lakini atupeleke tunakotaka kufika.
 
Maskini JK, yaani wenzake wamemchoka kiasi hiki hadi kumlazimu kuwatumia akina Mrema na Yahya kumsafisha?

Poor Mr. President..!
 
Mrema alisema vigogo hao wanatumia mwamvuli wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuandaa makongamano kwa nia ya ya kumtukana na kumhujumu Rais Kikwete.

"Wanatumia mwavuli huo kumtukana rais kwamba anazungukwa na wezi na kwamba hana maamuzi magumu wakati wenyewe hawana maamuzi hayo," alisema Mrema.

"Ni aibu kwa vigogo hao wa CCM tena wanaojifanya kuwa wapo chini ya mwamvuli wa Tasisi ya Baba wa Taifa kuandaa makongamano ya kumtukana rais wetu hadharani wakati wenyewe pia hawana mamuzi magumu na kama wanayo basi wajitangaze hadharani kuwa wao ndiyo CCJ," alisema Mrema.

Ama kweli nyani haoni kundule, yeye Mrema alipokuwa anamtukana Mkapa aliona ni sawa tu au Mkapa hakuwa rais wa nchi?

Kama kuna watu wanaoongoza kwa kuwatukana viongozi hasa rais hapa TZ, mrema is among the top.
 
Maskini JK, yaani wenzake wamemchoka kiasi hiki hadi kumlazimu kuwatumia akina Mrema na Yahya kumsafisha?

Poor Mr. President..!

Ikifikia kiongozi wa nchi kusafishwa na watu bogus kama Mrema na yule mpiga ramli Yahya basi ni dalili tosha kwamba Kiongozi huyo hafai kuwa madarakani.
 
karudi kutoka india alikopelekwa na JK lini?
naoana analipa fadhira wakati bado wa motomoto,
 
Mrema kama kweli kasema hivyo bila unafiki ana uhuru wa kutoa maoni yake

Lakini kama analipa fadhila atakua ametukosea watanzania,hatuhitaji wema wa namna hiyo.Kwani CCJ ikianzishwa na vigogo wa CCM ni kosa?kuamua kujitokeza leo au baadae ni uamuzi wao,kila chama/kundi lina mkakati wake.kelele za nini? i like the way Butiku alivyojibu
 
Tanzania ni huru na kila mtu yu huru mradi havunji sheria na katiba, mbona CCJ ni kitu ya kawaida tu na mkisikia ni chama cha bwana mkubwa mwenyewe anataka fanya ya mutharika mtasemaje?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom