Mrema aungwe mkono kukomesha halmashauri zilizokubuhu ubadhirifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrema aungwe mkono kukomesha halmashauri zilizokubuhu ubadhirifu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jenifa, Mar 13, 2011.

 1. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Mrema aungwe mkono kukomesha halmashauri zilizokubuhu ubadhirifu
  Na Mhariri (Nipashe)  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema(mbunge wa Vunjo-TLP), wiki hii imeendeleza makali yake kupambana na halmashauri zinazolegalega katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayogharimiwa na serikali.
  Kamati hii katika hali inayoonyesha kutoridhika na utendaji kazi wa watendaji katika halmashauri ilizotembelea kukagua miradi inayofadhiliwa na serikali, imefikia hatua ya kutoa adhabu ya kukatwa mishahara ya watumishi hao bila huruma.
  Agizo la aina hiyo limeiangukia Halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini ambako watendaji wake watakatwa asilimia 15 ya mishahara yao. Wamo pia Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Annah Mwahalende, mweka hazina, wakuu wa idara na maofisa wanaosimamia miradi ya maendeleo.
  Hatua hiyo imetokana na kitendo cha watendaji hao kushindwa kuandika ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo. Adhabu kama hiyo imetolewa kwa watendaji wa halmashauri ya Same, akiwemo Mkurugenzi, Joseph Mkude.
  Kamati hiyo pia imeagizwa kusimamishwa kazi kwa watendaji 12 wa halmashauri ya wilaya ya Rombo, kisha wakamatwe kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa mamilioni ya fedha. Aidha, imeeleza masikitiko yake kuhusu ubovu uliojitokeza katika kuandaa na kuwasilisha ripoti za halmashauri hizo na kuagiza ziandaliwe upya na kuwasilishwa kabla ya Aprili 11, mwaka huu na kwamba vitabu vya ripoti vikabidhiwe kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
  Tuchukue nafasi hii kupongeza kazi nzuri iliyoanza kufanywa na kamati hii ya Bunge katika kufuatilia matumizi ya fedha za serikali zinazomwagwa kwenye hamlshauri nchini kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
  Serikali kila mwaka imekuwa ikitoa fedha nyingi sana kwa halmashauri nchini kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini katika baadhi ya hamlshauri fedha hizo zimekuwa zikifujwa ikiwa ni pamoja na kuzielekeza kwenye miradi ambayo haikupangiwa kinyume na utaratibu.
  Ufujaji mwingine ambao umekuwa ukitajwa ni pamoja na miradi kujengwa chini ya viwango, mfano barabara, na fedha zake kutiwa mifukoni mwa wajanja, vikao vya ujanja ujanja na kujilipa posho na zingine wizi wa kalamu unaofanywa na wanaosimamia fedha hizo na ujanja mwingine.
  Matokeo yake ndio kujikanyaga kanyanga wakati wa kuandaa ripoti ya mapato na matumizi ya fedha hizo kama ambavyo tayari imejitokeza kwenye baadhi ya halmashauri zilizotembelewa na kamati hiyo ya Bunge. Kasoro hizo zimo kwenye halmashauiri kibao na inawezekana zilibweteka hasa kwa kuamini kuwa serikali haiwezi kuweka utaratibu wa kuzifuatilia.
  Hivi sasa zoezi hilo la ufuatiliaji wa fedha za serikali kwenye halmashauri hizo limepata wenyewe na tunaamini kamati hii ya Mrema itaibua mengi jinsi fedha hizo za serikali zinavyofujwa au kutafunwa na watendaji wasio waaminifu japo wamepewa dhamana kubwa na serikali.
  Usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo katika halmashauri zetu, ndio umechangia kwa kiasi kikubwa manungÂ’uniko ya wananchi kwamba serikali haiwajali, kumbe watendaji wasio waaminifu ndio sumu inayokwamisha mipango mizuri ya serikali iliyolenga kuiletea nchi yetu maendeleo.
  Uoza kwenye halmashauri nyingi umekuwa ukibainishwa kila mwaka kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Kwa mtindo wa kamati hii ya Bunge wa kutoa adhabu papo kwa papo, tunaamini wakorofi kwenye halmashauri zetu watabainika. Na kinachofuatwa ni kamati hii ya bunge kuungwa mkono na vyombo vyote vinavyohusika ikiwa ni pamoja na jeshi la polisi ili kusafisha watendaji wabovu kwenye halmashauri zetu.
  Hakuna sababu ya kuwafumbia macho watu ambao wanaipaka matope serikali kwamba haiwajali wananchi wakati taratibu zipo, fedha zinatolewa kila mwaka lakini waliopewa dhamana kusimamia wanageuka mchwa na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi. Kasi iliyoanza nayo Kamati hii ya Bunge ya fedha za serikali isirudi nyuma hadi kieleweke. Hata kama ni kufilisiwa. watakaobainika kufuja fedha za maendeleo wasionewe huruma.
   
 2. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  kamati iliongozwa na dr slaa 2006 - 2010. mrema kaikamata tayari kumekucha. baba daktari mrema sogeza gurudumu mbele wewe ni dume la mbegu nakufagilia
   
 3. p

  police Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi wakati dr. slaa anaongoza kamati hii palikuwa kimya? alikuwa anapokea za pembeni? mrema mwezi tu tumesikia rombo na same. hawa ndio viongozi tuwataka. hongesa mrema kwa kazi nzuri..
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Kweli A L Mrema kaanza na makali ila sijui kama ataendelea nayo hadi mwisho.

  Kila mtu ana namna yake ya kufanya kazi Dr Slaa na Dr Mrema watu wawili tofauti kabisa.
   
 5. M

  Magirito New Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa naelewa ni kwa nini wana-vunjo "hawadanganyiki" juu ya propaganda chafu dhidi ya Dr Mrema. Huwa hana mzaha na kazi zake. Akiahidi anatekeleza, ni mfano wa kuigwa... Mnyonge mnyongeni jamani..

  Tutegemee mapinduzi makubwa kwenye halmashauri zetu, I believe he wont leave any stone unturned!!

  Big up Dr Mrema for "walking the talk". Keep it up!!!
   
 6. semmy samson

  semmy samson Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ebwanaeee kumbe Mrema ni Dr.????????!!!!!!!!!!!!

  ila mheshiwa anajua kazi kumbukaeni yule ni mkungwe halaf kaja na nguvu mpya. nasikia kanywa kikombe cha babu loliondo.......kamua baba
   
Loading...