Mrema aunguruma Star TV, atoboa siri nzito uteuzi wake Parole!!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,903
2,884
Ndugu Agustine Lyatonga Mrema amesema kazi ya parole alishaanza kuifanya akiwa waziri wa mambo ya ndani ambapo aliwahi kuwaendea wafungwa majambazi na kuwaahidi ikiwa watamwonyesha mtandao wa ujambazi atawaombea msamaha kwa rais jambo walilolifurahia na kumfanya afanikiwe sana kwenye vita yake dhidi ya maovu mbalimbali hivyo ameteuliwa kihalali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Augustine Mrema ataka wananchi wapime utendaji wake ndani ya siku 100. Aahidi kubadilisha tabia za wahalifu.
 
Kwani wananchi ndio walio mteua hadi wapime utendaji wake ndani ya siku 100!?
Hii ni dalili ya kulewa madaraka bado mapema.
 
Jamani mwacheni na yeye awe na uhakika wa mlo kwa miaka hii mitatu, haya maisha ni magumu, vijana tu tunadata ndio sembuse wazee?

Magufuli ametenda vyema kumpa kibarua huyu mzee.
mbavu zangu , Awe na uhakika na mlo wake e? Huyu jamaa kama kufa angekufa zamani, wamwache tu umri ushaenda
 
Hajajibu swali aliloulizwa na mtangazaji kama ana sifa za kuwa mwenyekiti wa bodi ya Parole na badala yake anaeleza historia ya utendaji wake.Tena mtangazaji katanguliza kuwa mwenyekiti aliemaliza muda wake alikuwa jaji.

mrema hawezagi kujibu maswali

Team kuropoka...!

Duuuh njaa mbaya sana, huyu ndiye alitaka kuwa Raisi wa Tanzania 1995, tungeisoma namba

Kwani wananchi ndio walio mteua hadi wapime utendaji wake ndani ya siku 100!?
Hii ni dalili ya kulewa madaraka bado mapema.
Hata wapinzani mnatoleana macho??
 
Ndugu Agustine Lyatonga Mrema amesema kazi ya parole alishaanza kuifanya akiwa waziri wa mambo ya ndani ambapo aliwahi kuwaendea wafungwa majambazi na kuwaahidi ikiwa watamwonyesha mtandao wa ujambazi atawaombea msamaha kwa rais jambo walilolifurahia na kumfanya afanikiwe sana kwenye vita yake dhidi ya maovu mbalimbali hivyo ameteuliwa kihalali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Augustine Mrema ataka wananchi wapime utendaji wake ndani ya siku 100. Aahidi kubadilisha tabia za wahalifu.
Mwenyekiti wa Bodi atakuwa mtendaji.... nafikiri apewe clearly majukumu yake na mipaka yake, vinginevyo itakuwa taabu na huyu mzee
 
Mrema aliomba kazi kapewa kazi mwacheni afanye kaz
MRE.jpg
 
Sasa atabadilishaje tabia ya wahalifu wakati yeye no mwenyekiti wa parole tu....kwani mwenyekiti wa parole ni Mtendaji???inawezekana hajui mipaka yake . anatakiwa kupata semina elekezi huyu la sivo unaweza ukamkuta akilazimisha kufanya kazi za wakuu wa magereza au kamishina wa magereza..
 
Jamani mwacheni na yeye awe na uhakika wa mlo kwa miaka hii mitatu, haya maisha ni magumu, vijana tu tunadata ndio sembuse wazee?

Magufuli ametenda vyema kumpa kibarua huyu mzee.
Kapewa shavu!meli ilishaanza kuzamaa
 
Jamani mwacheni na yeye awe na uhakika wa mlo kwa miaka hii mitatu, haya maisha ni magumu, vijana tu tunadata ndio sembuse wazee?

Magufuli ametenda vyema kumpa kibarua huyu mzee.
matola unaumiza mbavu zangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom