Mrema ataka kupewa wizara yake ya mambo ya ndani,adai ana uzoefu nayo

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Mrema ataka apewe "ile Wizara yake" chap chap! 04/11/2010
0 Comment(s)


Baada kutangazwa mshindi wa Ubunge kwa jimbo la Vunjo, mbunge mteule kwa tiketi ya Chama Cha Tanzania Labour Party, TLP, Augustine Lyatonga Mrema, ameibuka na kumuomba Rais atakayeingia madarakani asisahau kumpa nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuwa anaimudu vilivyo.​
9768155.jpg
Augustine Lyatonga Mrema/Mb - Vunjo​
Akizungumza na gazeti la DarLeo, Mrema amesema amepokea kwa furaha matokeo kwa kuwa wapiga kura wake wana imani naye na wanafahamu fika kuna baadhi ya mambo ambayo tangu yeye aondoke madarakani hayajatekelezwa.

Amesema anaamini kuwa nafasi ya Waziri mwenye dhamana aliyokuwa akiishika yeye hapo awali imekuwa ikipwaya kwa muda mrefu hivyo ni vyema akarejeshewa ili afanye kazi yenye maslahi kwa wananchi na Taifa.

“CCM wakubali wakatae mimi tangu niachie ngazi kwenye ile nafasi ya UWaziri wa Mambo ya Ndani ilikuwa imepwaya sana, sasa umefika muda muafaka wa kunirejeshea nafasi hiyo ili niendeleze na kutekeleza yale niliyoyafanya hapo awali,” amesema Mrema.

Ameongeza kuwa aliwahi kuongoza Jimbo la Vunjo miaka 20 iliyopita lakini hadi leo ana mvuto wa kisiasa na wananchi wanamkubali kutokana na utendaji wake na ndiyo maana wamempa kura nyingi na kumuomba arejee nafasi yake ya awali.

“Sio kama najipigia debe. Haya ni maombi ya wapiga kura wangu. Wameona kabisa kuwa ile nafasi inanifaa hivyo wamenishauri kama nitaipata niitumikie kwa kuwa kipindi kile niliimudu na tangu nimeondoka imeonekana kupwaya,” amesema Mrema.

Nafasi ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani ilikuwa ikishikiliwa na Lawrance Masha, ambaye alikuwa mgombea wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza ambaye alikuwa akitetea nafasi yake lakini hata hivyo, ameangushwa na jimbo hilo kushikiliwa na Ezekia Wenje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Awali Wenje alienguliwa baada ya Masha kumuwekea pingamizi, lakini NEC ilimrejesha baada ya Masha kushindwa kuthibitisha tuhuma za Wenje kuwa si raia.



from: Mrema ataka apewe "ile Wizara yake" chap chap! -
 
mrema ataka apewe "ile wizara yake" chap chap! 04/11/2010
0 comment(s)


baada kutangazwa mshindi wa ubunge kwa jimbo la vunjo, mbunge mteule kwa tiketi ya chama cha tanzania labour party, tlp, augustine lyatonga mrema, ameibuka na kumuomba rais atakayeingia madarakani asisahau kumpa nafasi ya waziri wa mambo ya ndani kwa kuwa anaimudu vilivyo.​

9768155.jpg
augustine lyatonga mrema/mb - vunjo​

akizungumza na gazeti la darleo, mrema amesema amepokea kwa furaha matokeo kwa kuwa wapiga kura wake wana imani naye na wanafahamu fika kuna baadhi ya mambo ambayo tangu yeye aondoke madarakani hayajatekelezwa.

Amesema anaamini kuwa nafasi ya waziri mwenye dhamana aliyokuwa akiishika yeye hapo awali imekuwa ikipwaya kwa muda mrefu hivyo ni vyema akarejeshewa ili afanye kazi yenye maslahi kwa wananchi na taifa.

“ccm wakubali wakatae mimi tangu niachie ngazi kwenye ile nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani ilikuwa imepwaya sana, sasa umefika muda muafaka wa kunirejeshea nafasi hiyo ili niendeleze na kutekeleza yale niliyoyafanya hapo awali,” amesema mrema.

Ameongeza kuwa aliwahi kuongoza jimbo la vunjo miaka 20 iliyopita lakini hadi leo ana mvuto wa kisiasa na wananchi wanamkubali kutokana na utendaji wake na ndiyo maana wamempa kura nyingi na kumuomba arejee nafasi yake ya awali.

“sio kama najipigia debe. Haya ni maombi ya wapiga kura wangu. Wameona kabisa kuwa ile nafasi inanifaa hivyo wamenishauri kama nitaipata niitumikie kwa kuwa kipindi kile niliimudu na tangu nimeondoka imeonekana kupwaya,” amesema mrema.

Nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani ilikuwa ikishikiliwa na lawrance masha, ambaye alikuwa mgombea wa jimbo la nyamagana mkoani mwanza ambaye alikuwa akitetea nafasi yake lakini hata hivyo, ameangushwa na jimbo hilo kushikiliwa na ezekia wenje wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema).

Awali wenje alienguliwa baada ya masha kumuwekea pingamizi, lakini nec ilimrejesha baada ya masha kushindwa kuthibitisha tuhuma za wenje kuwa si raia.



From: mrema ataka apewe "ile wizara yake" chap chap! -
he sijamwelewa mrema kwani kunampango wa serikali ya mseto tz ?
 
he sijamwelewa mrema kwani kunampango wa serikali ya mseto tz ?

Mseto gani? kwani Mrema ni mpinzani? ama amewahi kuwa mpinzani? Kazi aliyotumwa mwaka 1995 ameimaliza na ccm wamemfanyia namna akapata Vunjo ili ale pension
 
mseto gani? Kwani mrema ni mpinzani? Ama amewahi kuwa mpinzani? Kazi aliyotumwa mwaka 1995 ameimaliza na ccm wamemfanyia namna akapata vunjo ili ale pension

but chama alichoingia nacho sidhani kama kitawezesha hilo!
 
Kwa jinsi alivyochoka sidhani kama anaweza hiyo kazi,wakati akiwa Waziri changamoto hazikuwa nyingi kamailivyo sasa na mambo mengi yamebadilika.
Asitegemee CCM kukubali kumteua yeye kama Waziri,hizo ndoto zimewezekana Zanzibar tu na haiwezi kutokea bara
 
wachaga mpo hapo? kilo ya kahawa itafika tena tsh 2400/=?:peace:
 
Back
Top Bottom