Elections 2010 Mrema ataka apewe "ile Wizara yake" chap chap!

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Baada kutangazwa mshindi wa Ubunge kwa jimbo la Vunjo, mbunge mteule kwa tiketi ya Chama Cha Tanzania Labour Party, TLP, Augustine Lyatonga Mrema, ameibuka na kumuomba Rais atakayeingia madarakani asisahau kumpa nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuwa anaimudu vilivyo.​
9768155.jpg

Augustine Lyatonga Mrema/Mb - Vunjo​

Akizungumza na gazeti la DarLeo, Mrema amesema amepokea kwa furaha matokeo kwa kuwa wapiga kura wake wana imani naye na wanafahamu fika kuna baadhi ya mambo ambayo tangu yeye aondoke madarakani hayajatekelezwa.

Amesema anaamini kuwa nafasi ya Waziri mwenye dhamana aliyokuwa akiishika yeye hapo awali imekuwa ikipwaya kwa muda mrefu hivyo ni vyema akarejeshewa ili afanye kazi yenye maslahi kwa wananchi na Taifa.

“CCM wakubali wakatae mimi tangu niachie ngazi kwenye ile nafasi ya UWaziri wa Mambo ya Ndani ilikuwa imepwaya sana, sasa umefika muda muafaka wa kunirejeshea nafasi hiyo ili niendeleze na kutekeleza yale niliyoyafanya hapo awali,” amesema Mrema.

Ameongeza kuwa aliwahi kuongoza Jimbo la Vunjo miaka 20 iliyopita lakini hadi leo ana mvuto wa kisiasa na wananchi wanamkubali kutokana na utendaji wake na ndiyo maana wamempa kura nyingi na kumuomba arejee nafasi yake ya awali.

“Sio kama najipigia debe. Haya ni maombi ya wapiga kura wangu. Wameona kabisa kuwa ile nafasi inanifaa hivyo wamenishauri kama nitaipata niitumikie kwa kuwa kipindi kile niliimudu na tangu nimeondoka imeonekana kupwaya,” amesema Mrema.

Nafasi ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani ilikuwa ikishikiliwa na Lawrance Masha, ambaye alikuwa mgombea wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza ambaye alikuwa akitetea nafasi yake lakini hata hivyo, ameangushwa na jimbo hilo kushikiliwa na Ezekia Wenje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Awali Wenje alienguliwa baada ya Masha kumuwekea pingamizi, lakini NEC ilimrejesha baada ya Masha kushindwa kuthibitisha tuhuma za Wenje kuwa si raia.


from: - Habari
 
Nadhani atakuwa amefurai Masha kupigwa chini
Hajui kuwa kuna 10 chances za Raisi na ili mradi wa ID uendelee lazima Masha arudi Mrema ataaribu
 
Mimi binafsi sina imani na Mrema. Kuhamahama kwake hasa kunanitia wasiwasi tangu zamani. Mtu ambaye amewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani bila shaka anajua vizuri kabisa siri za nchi. Wale waliotoka CCM wakiwa na siri za ndani kabisa mwisho wao tumeuona (tumeusikia); nina mashaka kama Mrema amewahi kutoka CCM. Akili hainiruhusu kumfikiria Mrema nje ya "system".
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom