Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 45
Mrema apinga serikali ya mseto Kigoma
na Jacob Ruvilo
na Jacob Ruvilo
MGOGORO wa serikali ya mseto katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma-Ujiji, mkoani Kigoma, umeingia katika sura mpya kutokana na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, kupinga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukabidhi madaraka kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa madai kuwa wananchi wa manispaa hiyo hawakushirikishwa kutoa maoni kuhusu serikali hiyo.
Akihutubia mkutano wa hadhara mkoani hapa mwishoni mwa wiki, Mrema alisema kutokana na hali hiyo seriklali ya mseto katika manispaa hiyo si halali.
Alisema CCM ilikubali mfumo wa serikali ya mseto Kigoma kutokana na kuona kuwa watanufaika.
Aliongeza kuwa kama wangekuwa waungwana, suala la serikali ya mseto Zanzibar lisingesubiri maoni ya wananchi.
Mrema alisema kama suala la serikali ya mseto visiwani Zanzibar linasubiri maoni ya wananchi, basi suala al serikali ya mseto katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoima-Ujiji lingesubiri pia maoni ya wananchi.
Kutokana na utata huo, Mrema ametaka kuvujwa kwa serikali ya mseto katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji, ili kusubiri maoni ya wananchi au kuruhusu serikali ya mseto Zanzibar bila kungoja maoni ya wananchi kama ilivyoundwa serikali ya mseto Kigoma.
Mrema alimtahadharisha Rais Jakaya Kikwete na serikali yake kuwa makini na maamuzi ya ubabaishaji kwa sababu hali hiyo inaweza kusababisha vurugu kama zilizotolea nchini jirani ya Kenya.
Wananchi waliohudhuria mkutano huo, walionekana kuunga mkono kauli hiyo ya Mrema kwa kushangilia mara kwa mara.
Kwa kauli moja wananchi wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji wameitaka Chadema kutoachia madaraka hadi maamuzi ya seikali ya mseto yatakapokuwa sawa katika pande zote mbili za Zanzibar na Kigoma