AMARIDONG
JF-Expert Member
- Jun 24, 2010
- 2,501
- 183
MWENYEKITI wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Agustine Mrema (TLP), amemvua madaraka Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyala, Kata ya Marangu Magharibi, Agustino Fabiani kwa madai ya unywaji wa pombe haramu ya gongo.
Mrema ametoa uamuzi huo wakati wakiwa katika operesheni maalumu ya Ulinzi Shirikishi kwa lengo la kukabiliana na uhalifu na ujambazi katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Mwanasiasa huyo ni Mbunge wa jimbo hilo. Katika operesheni hiyo ambayo ilifanywa kwa ushirikiano na Polisi, timu hiyo ya viongozi ilipita katika baadhi ya vijiji katika jimbo hilo na inadaiwa ilimkuta Mwenyekiti huyo wa Kijiji akiwa amelewa.
Mrema alidai kuwa, pamoja na kwamba Mwenyekiti huyo alikuwa mwanachama wa TLP, lakini yeye hawezi kulea viongozi aliodai hawana maadili kwa kuwa watazorotesha maendeleo ya wananchi.
Mbunge huyo alidai kuwa, taarifa za wanakijiji alizonazo zilieleza kuwa Mwenyekiti huyo alikuwa akisikika akiwahamasisha wananchi wanywe pombe hiyo kwa kuwa haina madhara kwa madai ni sawa na bia zilizopimwa kitaalamu.
Mimi ni Mbunge wa wananchi wote wakiwemo wasio na vyama..nikimtetea huyu Mwenyekiti, wananchi hawatapata maendeleo, nimemvua madaraka yake ili iwe mfano kwa viongozi wengine wasio na maadili, alisema.
Wakati wa operesheni hiyo ilibainika kwamba Kijiji cha Nganjoni ni kitovu cha utengenezaji wa pombe hiyo baada ya kukutwa kwa mitambo ya utengenezaji pombe hiyo huku wananchi wa eneo hilo wakihama makazi yao kwa hofu ya kutiwa mbaroni.
Mrema alisema, Jimbo la Vunjo limeathiriwa na vitendo vya uhalifu kutokana na kukithiri kwa uzalishaji wa pombe hiyo pamoja na unywaji wake na uvutaji wa bangi, hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa huku baadhi ya ndoa zikivunjika na wazazi kuacha kupeleka watoto shule.