Mrema alazwa KCMC

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Tunamuombea apone haraka ili aendelee na shughuli zake za kila siku.

Mrema alazwa KCMC

na Charles Ndagulla, Moshi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi akisumbuliwa na homa ya mapafu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye wodi namba 15 ya hospitali hiyo, Mrema alisema kuwa, amelazwa hapo tangu Jumanne wiki hii na kukanusha uvumi ulioenea mjini hapa kuwa yuko mahututi.

“Ngoja niamke kitandani ili muelewe kwamba mimi siko mahututi, maana mnaweza mkaondoka hapa na kwenda kuandika ‘Mrema yuko taabani’, si kweli, hata watoto wangu nimewaeleza naendelea vizuri, naomba msiwatie hofu wanachama wangu,” alisema Mrema huku akiinuka kitandani kuthibitisha maneno yake.

Alisema kuwa, hali yake imeimarika sana tangu alazwe, na iwapo itaendelea hivyo, ana uhakika kuwa, anaweza kuruhusiwa wakati wowote kuanzia sasa na kusisitiza lazima amalize dawa alizopewa na madaktari wanaomtibu.

Kwa siku tatu mfululizo kumekuwepo na uvumi kuwa, Mrema ambaye yupo mkoani Kilimanjaro kwa takribani wiki tatu sasa, amelazwa katika hospitali hiyo akiwa hajitambui, madai ambayo amesisitiza kuwa si ya kweli.

Katika hatua nyingine, Mrema ameiomba serikali kuisadia Hospitali hiyo ya Rufaa ya KCMC, inayoendeshwa na Shirika la Msamaria Mwema (GSF), ili kukabiliana na uhaba wa dawa pamoja na msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaolazwa hapo.

Alisema kuwa, katika kipindi alicholazwa hapo, amebaini kuwa, muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 35, huku msongamano wa wagonjwa ukiwa mkubwa kutokana na wingi wa wagonjwa.

Aliiomba serikali kuzitumia fedha zinazorejeshwa na watu wanaodaiwa kufuja mabilioni ya fedha za wavuja jasho katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kusaidia wagonjwa walioko hospitalini, wakiwamo hao wa KCMC na kwingineko.

Alishangazwa na wimbi la viongozi waandamizi wa serikali na wa chama tawala (CCM) kukimbilia nje ya nchi kwa ajili ya kuchunguzwa afya zao na kuacha kuzitupia macho hospitali zilizopo hapa nchini, ambazo alisema zina uhaba mkubwa wa dawa, vitendea kazi na watumishi.

“Hii ndiyo India yetu, acha hao wanaokimbilia nje kwenda kuangalia afya zao na kuacha kuzisaidia hospitali kama hizi ambazo ni mkombozi wetu mkubwa, wangeweza kutumia fedha zilizorejeshwa na mafisadi wa EPA kusadia hospitali hizi, matatizo kama haya ya mrundikano wa wagonjwa yangepungua,” alisisitiza.

Mrema yupo mkoani Kilimanjaro akifuatilia mwenendo wa kesi yake ya madai ya fidia ya sh milioni 500 aliyoifungua dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Jeshi la Polisi nchini, ambayo ipo Mahakama Kuu Kanda ya Kilimanjaro.

Kesi hiyo inatokana na kufutwa kwa kesi namba 1545/99 ya uchochezi aliyofunguliwa na Jeshi la Polisi mwaka 1999, baada ya Mrema kukamatwa kwa madai ya uchochezi pamoja na wenzake sita, akiwamo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti TLP Zanzibar, Farahan Mzee Farahan.

Wengine walioshitakiwa pamoja na Mrema ni Getrude Pwila, ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Kitengo cha Wanawake, Kalisti Njau aliyekuwa dereva wa Mrema na Festo Vidonge, ambaye kwa sasa ni msadizi wa mbunge wa Jimbo la Vunjo Alocye Kimaro (CCM).

Akiwa na wenzake, Mrema alikamatwa na polisi mwaka 1999 eneo la Marangu wilayani Moshi Vijijini, akituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kwamba, mke wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mama Anna Mkapa, alichota sh milioni 497 kutoka Benki ya NBC.

Pia walidaiwa kutoa maneno ya uchochezi kwamba, Mkapa wakati huo akiwa rais, naye alichota mamilioni ya fedha kutoka NBC na kuzificha kwenye moja ya benki nchini Uswisi.
 
Mrema alazwa KCMC

Alisema kuwa, katika kipindi alicholazwa hapo, amebaini kuwa, muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 35, huku msongamano wa wagonjwa ukiwa mkubwa kutokana na wingi wa wagonjwa.

“Hii ndiyo India yetu, acha hao wanaokimbilia nje kwenda kuangalia afya zao na kuacha kuzisaidia hospitali kama hizi ambazo ni mkombozi wetu mkubwa, wangeweza kutumia fedha zilizorejeshwa na mafisadi wa EPA kusadia hospitali hizi, matatizo kama haya ya mrundikano wa wagonjwa yangepungua,” alisisitiza.

Hii itawauma sana Viongozi. Bonge la statement...
 
Hii itawauma sana Viongozi. Bonge la statement...

...thubutuuuu!!!

Kuhani Mkuu ushasahau mwezi February George Bush alipokuja hospitali ya Amana pale Ilala ilivyokuwa?

kila mgonjwa na kitanda chake, tena kuna vitanda vilikuwa vitupu! hospitali ilipakwa rangi, ilipigwa deki, na wagonjwa hao wachache waliolazwa hapo "bila msongamano" walibahatika kunywa chai na mayai... kama ulibahatika kuangalia luninga, chumba cha madawa kilikuwa kimejaa madawa ya aina mbali mbali!...

yale yaleeee ya 'UJINGA WA MWAFRIKA!'...

sasa angalia huyu mkuu wa TAMISEMI naye alivyoripotiwa miezi mitatu tu baadae...


2008-05-06 16:05:07
Na Haji Mbaruku, Amana

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Stephen Wassira, ameitaka Hospitali ya Amana kujenga vituo vingine vya afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo...

...Kwani kulikuwa na ubaya gani "Joji Kichaka" akijionea mwenyewe 3rd world hospital ilivyo, yaani msongamano wa wagonjwa, hospitali chakavu, hamna madawa nk? si ndio misaada ingemwaga ya kutosha?

Viongozi wetu hawana haya wala hawaoni vibaya!
 
hivi hUyu si ndio alikuwa kinara wa kuvuruga upinzani mwaka 1995 na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa? natamani wanasiasa wetu wa Tanzania wangekuw
na upeo wa ziada hasa kuhusiana na malengo na maamuzi yao.

tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu upone na kuwa na nguvu kama zamani ili tuendelee kuiweka serikali katika mkondo stahimilifu!

mpaka Kieleweke.
 
pole Mrema MUNGU akupe wepesi katika kupona kwako!Get well soon!Naibu waziri mkuu mstaafu!
 
Tunakuombea heri na afya njema mapema iwezekanavyo.
Uje tuendeleze vita kuikomboa tanzania
 
Tunakuombea kwa MUngu upone haraka sana kwani bado unamchango mkubwa sana katika jamii wa kufichua wala nchi.Bila wewe vituo vidogo vya POLICE visingekuwepo leo hii uswazi licha ya vingine kuwa vimesha jifia na kuezuliwa kabisa.
Utapona tu tupo nyuma yako tukikuombea.
 
Tunakuombea kwa MUngu upone haraka sana kwani bado unamchango mkubwa sana katika jamii wa kufichua wala nchi.Bila wewe vituo vidogo vya POLICE visingekuwepo leo hii uswazi licha ya vingine kuwa vimesha jifia na kuezuliwa kabisa.
Utapona tu tupo nyuma yako tukikuombea.

Inasikitisha kuona kuwa vile vituo vilivyokufa ndio vinahusishwa na mrema, lakini vilivyo msaada hawamkumbuki, jamani Tanzania tuna ugonjwa mbaya!!!

Of all the leaders, ninaowakumbuka, waliofanya vitu vya kuonekana.
Ni mrema,
na Mwaibula alivyochora mistari daladala na kuzipangia ruti. Japo wanamnyamazisha
 
Inasikitisha kuona kuwa vile vituo vilivyokufa ndio vinahusishwa na mrema, lakini vilivyo msaada hawamkumbuki, jamani Tanzania tuna ugonjwa mbaya!!!

Of all the leaders, ninaowakumbuka, waliofanya vitu vya kuonekana.
Ni mrema,
na Mwaibula alivyochora mistari daladala na kuzipangia ruti. Japo wanamnyamazisha

Tatizo la watawala wetu iwa wanaweka kila kitu kisiasa maana wamemchukia na wanaona kama havina msaada vingi siku hizi vimekuwa magofu.Unajua huyu jamaa alikuwa makini sana kwenye swala la usalama kila mtu analijua hilo kwani majambazi walijisalimisha walisalimisha bunduki.Ni kiongozi wa kuigwa sana leo.
 
Tatizo la watawala wetu iwa wanaweka kila kitu kisiasa maana wamemchukia na wanaona kama havina msaada vingi siku hizi vimekuwa magofu.Unajua huyu jamaa alikuwa makini sana kwenye swala la usalama kila mtu analijua hilo kwani majambazi walijisalimisha walisalimisha bunduki.Ni kiongozi wa kuigwa sana leo.

hasa hili suala la sasa ambapo jambazi asema yeye ndo alokwiba na kuwakana akina Zombe nimemkumbuka sana Mrema...!
 
Posted Date::6/10/2008
Mwanasiasa asifia madaktari KCMC baada ya kupata afueni
Na Ally Sonda, Moshi
Mwananchi

AFYA ya Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP) Augustine Mrema,ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya KCMC,mjini hapa inaendelea kuimarika zaidi.

Mrema ambaye alilazwa tangu Juni 3 mwaka huu, jana alisema kuwa, homa kali na maumivu ya kifua alivyokuwa nayo wakati analazwa hivi sasa yametoweka na kumshukuru Mungu, madaktari na wauguzi wa KCMC.

Mrema amerejea kauli yake aliyoitoa wiki iliyopita kuwa, kutokana na jinsi alivyohudumiwa vizuri KCMC, amejiona hana tofauti na kigogo wa serikali au wa chama fulani aliyelazwa kwenye Hospitali nchini India.

"Sijui niwape zawadi gani madaktari wazuri wa KCMC na wauguzi wao, yaani wamenipa huduma nzuri sana ya matibabu, mimi na waliokwenda India kutibiwa ngoma droo(tuko sawa), " alisema Mrema.

Kwa upande mwingine, aliwaonya baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), wanaotumia mikutano ya hadhara kumkejeli kuacha mara moja.

Alisema viongozi hao wa CCM wanapaswa kumfariji kwa kuwa yeye ndiye muasisi wa vita dhidi ya mafisadi nchini,vita ambavyo serikali ya Rais Jakaya Kikwete inapambana navyo.

"CCM wanapaswa kunifariji mimi,siyo kunikejeli, mimi ndiye muasisi wa vita dhidi ya mafisadi, mimi ndiye kiongozi wa kwanza kusema hadharani vigogo wa nchi wamegawana Sh900 milioni, nikashitakiwa mahakamani na kisha nikashinda kesi,CCM wasione wivu kunisifu kwa hilo, "alitamba.

Kuhusu madai yaliyotolewa na kiongozi mmoja wa CCM mkoani Kilimanjaro, kuwa Mrema hana mamlaka ya kutetea maslahi ya watumishi wa KCMC, alidai kiongozi huyo hana tofauti na mama wa kambo anayewanyanyasa watoto wa mke mwenza marehemu.

Alisema ataendelea kuiomba serikali iwasaidie watumishi wa KCMC wakiwamo Madaktari bingwa kupata maslahi bora ili waweze kufaidika na kuboresha maisha yao kama wasomi wengine.

" Mimi ndiye mgonjwa,nimetibiwa vizuri nimepona,sina zawadi ya kuwapa wauguzi na madaktari wangu isipokuwa kuwaombea maslahi mazuri serikalini...sasa huyo kigogo mmoja wa CCM wa mkoa anawashwa na nini? "Alihoji Mrema.
 
Back
Top Bottom