BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,845
Tunamuombea apone haraka ili aendelee na shughuli zake za kila siku.
Mrema alazwa KCMC
na Charles Ndagulla, Moshi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi akisumbuliwa na homa ya mapafu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye wodi namba 15 ya hospitali hiyo, Mrema alisema kuwa, amelazwa hapo tangu Jumanne wiki hii na kukanusha uvumi ulioenea mjini hapa kuwa yuko mahututi.
Ngoja niamke kitandani ili muelewe kwamba mimi siko mahututi, maana mnaweza mkaondoka hapa na kwenda kuandika Mrema yuko taabani, si kweli, hata watoto wangu nimewaeleza naendelea vizuri, naomba msiwatie hofu wanachama wangu, alisema Mrema huku akiinuka kitandani kuthibitisha maneno yake.
Alisema kuwa, hali yake imeimarika sana tangu alazwe, na iwapo itaendelea hivyo, ana uhakika kuwa, anaweza kuruhusiwa wakati wowote kuanzia sasa na kusisitiza lazima amalize dawa alizopewa na madaktari wanaomtibu.
Kwa siku tatu mfululizo kumekuwepo na uvumi kuwa, Mrema ambaye yupo mkoani Kilimanjaro kwa takribani wiki tatu sasa, amelazwa katika hospitali hiyo akiwa hajitambui, madai ambayo amesisitiza kuwa si ya kweli.
Katika hatua nyingine, Mrema ameiomba serikali kuisadia Hospitali hiyo ya Rufaa ya KCMC, inayoendeshwa na Shirika la Msamaria Mwema (GSF), ili kukabiliana na uhaba wa dawa pamoja na msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaolazwa hapo.
Alisema kuwa, katika kipindi alicholazwa hapo, amebaini kuwa, muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 35, huku msongamano wa wagonjwa ukiwa mkubwa kutokana na wingi wa wagonjwa.
Aliiomba serikali kuzitumia fedha zinazorejeshwa na watu wanaodaiwa kufuja mabilioni ya fedha za wavuja jasho katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kusaidia wagonjwa walioko hospitalini, wakiwamo hao wa KCMC na kwingineko.
Alishangazwa na wimbi la viongozi waandamizi wa serikali na wa chama tawala (CCM) kukimbilia nje ya nchi kwa ajili ya kuchunguzwa afya zao na kuacha kuzitupia macho hospitali zilizopo hapa nchini, ambazo alisema zina uhaba mkubwa wa dawa, vitendea kazi na watumishi.
Hii ndiyo India yetu, acha hao wanaokimbilia nje kwenda kuangalia afya zao na kuacha kuzisaidia hospitali kama hizi ambazo ni mkombozi wetu mkubwa, wangeweza kutumia fedha zilizorejeshwa na mafisadi wa EPA kusadia hospitali hizi, matatizo kama haya ya mrundikano wa wagonjwa yangepungua, alisisitiza.
Mrema yupo mkoani Kilimanjaro akifuatilia mwenendo wa kesi yake ya madai ya fidia ya sh milioni 500 aliyoifungua dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Jeshi la Polisi nchini, ambayo ipo Mahakama Kuu Kanda ya Kilimanjaro.
Kesi hiyo inatokana na kufutwa kwa kesi namba 1545/99 ya uchochezi aliyofunguliwa na Jeshi la Polisi mwaka 1999, baada ya Mrema kukamatwa kwa madai ya uchochezi pamoja na wenzake sita, akiwamo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti TLP Zanzibar, Farahan Mzee Farahan.
Wengine walioshitakiwa pamoja na Mrema ni Getrude Pwila, ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Kitengo cha Wanawake, Kalisti Njau aliyekuwa dereva wa Mrema na Festo Vidonge, ambaye kwa sasa ni msadizi wa mbunge wa Jimbo la Vunjo Alocye Kimaro (CCM).
Akiwa na wenzake, Mrema alikamatwa na polisi mwaka 1999 eneo la Marangu wilayani Moshi Vijijini, akituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kwamba, mke wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mama Anna Mkapa, alichota sh milioni 497 kutoka Benki ya NBC.
Pia walidaiwa kutoa maneno ya uchochezi kwamba, Mkapa wakati huo akiwa rais, naye alichota mamilioni ya fedha kutoka NBC na kuzificha kwenye moja ya benki nchini Uswisi.