Mrema: Afe kipa, afe beki Magufuli Rais 2020

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Picha zikimuonyesha Mwenyekiti Wa Tanzania labour party (TLP) akiongoza Mkutano Mkuu wa Taifa Wa kumpitisha Rais john pombe Magufuli kuwa mgombea pekee Wa urais anayeungwa mkono na tlp kwa mwaka 2020

Akiongoza kikao hicho Mrema amesema kwamba wajumbe Wa mkutano mkuu kutoka Tanzania bara na Visiwani zaidi 95 wameridhia kwa pamoja kumuunga mkono Mh Rais kurejea tena katika awamu nyingine kugombea urais 2020

Katika Mkutano Mkuu huo Mrema aliwaalika viongozi mbalimbali kutoka vyama vingine. Chama cha Mapinduzi kiliwakilishwa na Katibu Wa itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Pole Pole, David Saudi Mwaijojele Mwenyekiti Wa taifa Wa CCK pamoja na Msajili Msaidizi Wa vyama vya siasa nchini Sisty Nyahoza

Akimwakilisha Katibu mkuu Wa CCM, Humphrey Pole pole Amesema CCM inakubaliana na mkutano mkuu wa TLP kwa kumpitisha Mhe. Rais Magufuli kwani utendaji wake umewafuraisha watanzania wakiwemo wanachama Wa TLP.

IMG_20200509_114553_5.jpg
IMG_20200509_103252_6.jpg
IMG_20200509_121402_2.jpg
IMG_20200509_120331_9.jpg
IMG_20200509_102621_2CS.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua kuna kipindi mtu unaangalia siasa za Tanzania unaishiwa kabisa hata comments. Yaani unakwama kabisa, unazungusha akili na maarifa yako yote unakwama kabisa.

Enyi wapendwa mliosomea political sciences kwa kada mbali mbali hamuoni sasa ni kipindi muafaka kugundua other models za siasa duniani? Kwanini msianzishe utafiti kwa hadhi ya PHD au hata thesis za masters kuweza kuijua hii model ya siasa za Tanzania?
 
Wangesikia Kamanda wa Anga jemedari asiye yumba ama ukitaka muite Mwamba Mbowe anaongea na waandishi wa Habari kuhusu Mapapai na Mafenesi kuwa na corona ungeona maporisi wamjejaa kuzuia mkutano. Ila wakiongea mawakala wenu ccm, wapinzani hewa wanaandaliwa hadi eneo la kuongelea na kuwapa ulinzi. Hii Chadema ipogo tuu hata mukimbie ikulu zooteee mtaikuta tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkutano Mkuu wa Taifa Wa kumpitisha Rais john pombe Magufuli kuwa mgombea pekee Wa urais anayeungwa mkono na tlp kwa mwaka 2020

Katika Mkutano Mkuu huo Mrema aliwaalika Chama cha Mapinduzi na Katibu Wa itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Pole pole Amesema CCM inakubaliana na mkutano mkuu wa TLP kwa kumpitisha Mhe. Rais Magufuli kwani utendaji wake umewafuraisha watanzania
Hizi ndizo siasa za kisasa kama nilivyoshauri hapa

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums

Kwa jinsi TLP ilivyo hoi kiuchumi, haina mbunge hata mmoja wala diwani, na haipati ruzuku yoyote serikalini hivyo kitendo cha kupata uwezo wa ghafla wa kuitisha mkutano Mkuu na hadi kuvalia fulana na kofia!, it's not a joke!. Naomba kusijitokeze mwandishi wa habari za uchunguzi akachunguza TLP imepata wapi fedha za kuitisha mkutano huo, wakati chama hakina hata senti 5 ya uendeshaji!.

P
 
Hizi ndizo siasa za kisasa kama nilivyoshauri hapa

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums

Kwa jinsi TLP ilivyo hoi kiuchumi, haina mbunge hata mmoja wala diwani, na haipati ruzuku yoyote serikalini hivyo kitendo cha kupata uwezo wa ghafla wa kuitisha mkutano Mkuu na hadi kuvalia fulana na kofia!, it's not a joke!. Naomba kusijitokeze mwandishi wa habari za uchunguzi akachunguza TLP imepata wapi fedha za kuitisha mkutano huo, wakati chama hakina hata senti 5 ya uendeshaji!.

P
Haujamuona hapo Mr. "SLOW SLOW" inaonekana yeye ndio katoa FUNGU.
 
Namwona kamanda wangu POLEPOLE,nzuri Sana iyo CCM HOYEEEEEEEE

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Back
Top Bottom