Mrema Achezewa Rafu kijijini kwake Mkuu Wa Mkoa kikwazo

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
TANZANIA LABOUR PARTY
JIMBO LA VUNJO
Office: Njia Panda, HIMO
Tel: 0754 741 017/ 0710 645 473


Kumb. Na:TLP/UCHAGUZI VIJIJI/VITONGOJI/002 Tarehe: 04/11/2019

MKUU WA MKOA
KILIMANJARO

YAH: NJAMA ZA KUVURUGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VITONGOJI NA VIJIJI JIMBO LA VUNJO.

Naomba kukuarifu kuna njama zilizofanywa na baadhi ya viongozi wasiompenda Rais wetu na jitihada zake anazofanya za kutuletea maendeleo ili aonekane hatoshi kwa kuonyesha kwamba ameshindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji katika jimbo la Vunjo.

Kwa makusudi bila sababu za msingi vituo vya kuchukua na kurejesha fomu za wagombea katika jimbo la Vunjo havijafunguliwa toka tarehe 1.11.2019 mpaka leo tarehe 4.11.2019 siku ya kurejesha fomu.

Vituo ambavyo hazikufunguliwa ni:

MWIKA KASKAZINI
Vijiji:
Mrimbo uuo
Maring’a
Lole
Msae nganyeni
Msae Kinyanvuo
MWIKA KUSINI
Vijiji:
Kimangaro
Kirumeni
Kondeni
Mawanjeni
Matala
KILEMA KASKAZINI
Vijiji:
Kyou
Ruwa
Makame Juu
Makame Chini


KILEMA CHINI
Vijiji:
Rosho
Mkyasi
Kimororoni
Ngangu
KILEMA KUSINI
Vijiji:
Marawe Kyura
Masaera

KIRUA VUNJO MASHARIKI
Vijiji:
Nganjoni
Mrumeni
Kileuwo
Mero

KIRUA VUNJO MANGHARIBI
Vijiji:
Nduweni
Kwamare
Iwa
Kanji
Manu
Kanango
Marua
KIRUA VUNJO KUSINI
Vijiji:
Yam Makaa
Yam
Mparo
Uchira
Koresa
KAHE MASHARIKI
Vijiji:
Soko
Kyomu
Ghona
Kochakindo
Kiterini
Mikameni

KAHE MAGHARIBI
Vijiji:
Ngasinyi
Mwangaria
Kisangesangeni
Oria
Rau River
Mawala
Miwaleni
MARANGU MAGHARIBI
Vijiji:
Mbahe
Komalyangoye
Kiraracha
Kitowo
Kyala
MARANGU MASHARIKI
Vijiji:
Lyamrakana
Sembeti
Rauya
Lyasongoro
Samanga
Arisi

MAMBA KASKAZINI
Vijiji:
Kokirie
Kotela
Komakundi
Mboni
MAMBA KUSINI
Vijiji:
Mkolowoni
Lekula
Kiria
Kimbogno
Kimanga
MAKUYUNI
Vijiji:
Mieresini A
Mieresini B
Nyawenda
Furaha
Miembeni
Mbuyuni
Zilipendwa
Kiriche
Sindina
Kitula
Saghana
Msufini
Kisimani



Naomba uchaguzi huu usifanyike kwa sababu fomu zetu hazikupokelewa tutakuwa hatujatendewa haki.

TLP, Uhai wa Mtanzania
Wako,



DKT. AUGUSTINE LYATONGA MREMA
MWENYEKITI TLP TAIFA

Nakala kwa: Waziri wa TAMISEMI
Katibu Mkuu CCM
Afisa Utumishi Moshi

Mkuu Wa Mkoa Anna MGwira Amjibu .....

Nafuatilia sababu zilizotolewa na Mkurugenzi wa Moshi...kukicha nitakuja huko. Inaonekana kuna njama zinapangwa kuvuruga uchaguzi. Kwa hiyo imeleta baadhi ya vituo kutofunguliwa..hata hivyo nitafuatilia leo wkt wa urejeshaji wa form
images%20(3).jpeg
 
Hivi TLP zaidi ya Mrema Kuna mwanachama mwingine yeyote? Kama yumo humu anyooshe mkono juu
 
Unamtoaje rais katika hiki kinachoendelea wakati walioko chini yake ni bendera fuata upepo, upepo unakoelekea wao hawana ubishi zaidi ya kulalia kule ambako upepo unawasukumizia.
 
angekuwa ndiye Rais wa awamu ya Tatu Dr A.L.Mrema

hata hivyo huwezi ukapata vyote...hivi sasa ni Rais wa TLP
 
Mrema acha alinywe,alilikoroga mwenyewe,alifuga nyoka ndani sasa nyoka ameanza kumlamba,soon atangatwa.asilalamike
 
Kuna shoga moja humu linasema eti Tundu Lissu ndiye ameratibu mpango huu wa watendaji kuzikimbia ofisi zao kwa ina ya kuwakwepa wapinzi ili kuichafua Serikali.
 
angekuwa ndiye Rais wa awamu ya Tatu Dr A.L.Mrema

hata hivyo huwezi ukapata vyote...hivi sasa ni Rais wa TLP
Aliyotamka Mwalimu Nyerere mwaka 1995 ni bahati mbaya yakajitokeza 2015.
Alisema hivi "I'll not let my country go to the dogs"
Wengi walisema mwalimu katukana, lakini wasomi walitafsiri vizuri maana ya msemo huo. Ila kwa vile baada ya yeye kuondoka hakukuwa na mtu mwenye ubavu wa kuonya taifa 2015 yakatukuta ya kutukuta, na onyo halikuwepo tena
 
Back
Top Bottom