Mrema aandaa mkutano wa kujitangaza

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Daniel Mjema,Moshi

MBUNGE Mteule Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP),Agustino Mrema,
Jumamosi wiki hii atafanya mkutano mkubwa wa hadhara kutangaza mambo atakayowafanyia wananchi
wake ndani ya siku 100.

Mkutano huo utakakaofanyika katika mji mdogo wa Himo kuanzia saa 4:00 asubuhi,
utatanguliwa na maandamano makubwa yatakayohusisha magari, waendesha pikipiki
na wananchi kutoka kata zote za Jimbo hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mrema alisema angefurahi sana kama waliokuwa wapinzani
wake katika kinyang’anyo cha Ubunge nao watahudhuria mkutano huo kwa kuwa nao ni wakazi wa Jimbo hilo.

“Ningefurahi sana kumuona rafiki yangu na mtoto wangu Chrispin Meela na
John Mrema waje tu wasione soo (aibu) kuja kumsikiliza Mbunge wao atawafanyia nini
ndani ya siku 100 madarakani kwa sababu siasa si uhasama”alisema.

Katika kinyang’anyiro hicho,Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa
Taifa wa TLP alipata kura 38,010 akifuatiwa na mgombea wa
Chrispin Meela kura 23,870 huku John Mrema wa Chadema akipata kura 6,316.

Mrema alisema alisema matumaini ya Wananchi wa Jimbo hilo kwake ni makubwa sana
hivyo anataka atumie mkutano wa Jumamosi kuwashukuru kwa kumchagua na pia
nini atawafanyia ndani ya siku 100.

SOURCE: Gazeti la Mwananchi
 
Daniel Mjema,Moshi

MBUNGE Mteule Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP),Agustino Mrema,
Jumamosi wiki hii atafanya mkutano mkubwa wa hadhara kutangaza mambo atakayowafanyia wananchi
wake ndani ya siku 100.

Mkutano huo utakakaofanyika katika mji mdogo wa Himo kuanzia saa 4:00 asubuhi,
utatanguliwa na maandamano makubwa yatakayohusisha magari, waendesha pikipiki
na wananchi kutoka kata zote za Jimbo hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mrema alisema angefurahi sana kama waliokuwa wapinzani
wake katika kinyang'anyo cha Ubunge nao watahudhuria mkutano huo kwa kuwa nao ni wakazi wa Jimbo hilo.

"Ningefurahi sana kumuona rafiki yangu na mtoto wangu Chrispin Meela na
John Mrema waje tu wasione soo (aibu) kuja kumsikiliza Mbunge wao atawafanyia nini
ndani ya siku 100 madarakani kwa sababu siasa si uhasama"alisema.

Katika kinyang'anyiro hicho,Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa
Taifa wa TLP alipata kura 38,010 akifuatiwa na mgombea wa
Chrispin Meela kura 23,870 huku John Mrema wa Chadema akipata kura 6,316.

Mrema alisema alisema matumaini ya Wananchi wa Jimbo hilo kwake ni makubwa sana
hivyo anataka atumie mkutano wa Jumamosi kuwashukuru kwa kumchagua na pia
nini atawafanyia ndani ya siku 100.

SOURCE: Gazeti la Mwananchi

Good!
 
safii; he knows the game very well, shukrani na action plan ni muhimu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom