Mrejesho: Yule Dada mwenye mume aliyepanga na kajamaa

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
3,454
8,227
Mambo yamekua sio mambo asubuhi ya Leo tarehe 5 nikiwa nakunywa chai nasikia makelele kwa jirani na sauti za kuomba msaada. Basi Kama ilivyo ada ya watanzania tukaenda na wife kuangalia Kuna Nini kwa jirani maana mama mwenye nyumba alikua ndio anapiga kelele kuwa msiuliane humu ndani nendeni nje, msiuliane humu nendeni nje, majiraniiii!

Kumbe bana kale kajamaa kaliko kuwa kanakula yule mke wa mtu mwenye watoto watatu ambaye uzi wake niliwaletea humu kama mnaukumbuka yule mwanamke aliekuwa anaondoka kwa mumewe asubuhi na kuja kushinda kwa kajamaa hadi jioni.

Kumbe kale kajamaa roho ilikasuta kaka amua kumtafuta mwenye mke na kumpigia na kumuelekeza kila kitu hadi sehemu aliopo huyo mke wake na kweli jamaa kafuata ramani Hadi kamfuma mkewe alipo na ngumi ndipo zilipo anzia baada ya kuona mke anajibu jeuri. Bad enough kufika pale eneo la tukio nakutana na mjomba wangu macho kwa macho na kuniita jinaa langu na kumsalimia kumbe mjomba ndio mwenye mke

Sema kutokana na maisha ya mjini yalivyo ni ngumu kufahamiana na watu wa muunganiko wa familia yote ndio maana hata huyu shangazi yangu sikumtambua. Ila kwa Sababu damu ni nzito kuliko maji aisee ndio maana nilijikuta nafanya umbea humu jf kuwa wa kusemelea kuwa mwenye mke anamegewa nikatoa na muonekano wa mwanamke kumbe huyu mwanamke ni shangazi yangu kweli damu nzito jamani.

Hadi naenda kazini niliacha bado wanazozana na mjomba hataki kwenda police kwa msaada wanakasubiria kajamaa kanako mpa jeuri mwanamke kaje kamfukuze kwenye kila chumba huku mwanamke nae hataki kuondoka nikaona mambo yasiwe mengi hii shughuli Haina chakula Wala vinywaji ngoja niende kuusaka mkate wangu na familia yangu na kuwaacha wakiendelea na Mambo yao.

Bad enough kwa summary kumbe hela za geto alikua analipa mjomba, pamba baadhi zilizo kuwa zimeanikwa nje zilikua za mjomba vyombo na masufuria yote vya nyumbani kwa mjomba , mjomba mwenyewe hata kuongea anashindwa anatokwa na jasho tu na kujilaumu kuwa huyu mwanamke ndio Alie nilazimisha nimuoe leo kanizalia watoto watatu alafu bado wadogo eti ananiachia Sasa Mimi nawaleaje hao watoto wadogo

Nilicho jifunza

Wanaume tuishi maisha yetu na tupange tunataka Nini na tufanye Nini kwa wakati gani ukutegemea akili za Hawa viumbe lazima uliwe kichwa.

Wanaume tuwape hela wake zetu lkn kubwa kuliko hakikisha unajua kwa undani hizo hela zimefanya Nini na wapi ukijifanya najua sana unaweza ukakuta kumbe ndio hela za kuchongea jeneza lako unajilipia mwenyewe

Wanaume tunapo zaa watoto tujue kabisa Hawa watoto bila mama yao wataishi vipi na wapi hii iwe akilini mwako ukijifanya unaakili Sana utaliwa kichwa

Mengine mtajaza wenyewe msipende kutafuniwa kila kitu

Mjomba pole
 
Kila mtu na changamoto zake....Hakutawahi kuwepo na namna moja sahihi ya kutatua hizo changamoto.
 
Screenshot_20220105-093138_Chrome.jpg
 
Mambo yamekua sio mambo asubuhi ya Leo tarehe 5 nikiwa nakunywa chai nasikia makelele kwa jirani na sauti za kuomba msaada . Basi Kama ilivyo ada ya watanzania tukaenda na wife kuangalia Kuna Nini kwa jirani maana mama mwenye nyumba alikua ndio anapiga kelele kuwa msiuliane humu ndani nendeni nje ......msiuliane humu nendeni nje ....majiraniiii.....!
Achaumbea
 
Mjombaaa alimpaaa kilaaa ktuu lakini bado kaachwaa tuu,daaaaaa wanawakeee
Cha ajabu zaidi mwanamke ndio alimlazimisha amuoe kamzalia watoto eti ndio anamkimbia na kumuacha na watoto watatu alafu yeye anaenda kuanza upya maisha na kajamaa fresher .huu si ukuda huu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom