Mrejesho: Watoto wa mstaafu baada ya kupewa mitaji na baba yao

Matajiri wanawekeza elimu kwa watoto wao na wanawaandaa sana ili wazidi kuwa matajiri Zaidi ya wao. Hapa kosa ni kutowapa elimu bora watoto ambapo mwisho wa siku wanakuja kula mafao yako ya uzeeni na matokeo yake hapo ni lawama tu baadae kuwa nilikusaidia na wewe unisaidie wakati hilo lilitakiwa lije automatic
upo sawa kiongozi lakini elimu yetu inamuandaa mtu kuja kuajiriwa kama unavyojua ajira siku hizi ni tabu wasomi wengi sio kama miaka ile yani kusoma uje uajiriwe kumeshapitwa na wakati na akijaribu kujiajiri tatizo linakuja kwenye mtaji apo mzee katatua tatizo la ukosefu wa mitaji kwa wanawe. anachotakiwa kufanya ni kuwa na asilimia za umiliki kwenye iyo miradi ili iwe kama amewekeza sio amegawa tuu.
 
Hivi ukistaafu unawapa mafao yako watoto wako au unayahifadhi na kuwekeza yakusaidie siku za usoni? binafsi nawekeza sana kwenye elimu ya wanangu na kuwafundisha kujitegemea. Mafao nitayatumia na mama yao nikija staafu inshallah
Kuna kanuni maalum ya kutumia pension mkuu?
 
Mtaji wa mtoto ni elimu;
kama alichezea shule yake shauri zake;
Mafao yangu ni yangu,
umehangaika na hao watoto miaka yote ya kazi
tena wanakuja kupora kifuta jacho chako;
Hao wote labda walionunua mashamba,
lakini hakuna cha hoteli wa kufuga kuku;
maisha siyo rahisi kama wanavyowaza;
 
Kumbe wachoyo wengi ukianza kutoka udenda uzeeni sikupi hata chai
 
Na hiyo mzee aliwa nyima elimu ndipo alipokosea
Aliwanyima elimu au walikuwa hawana akili ya kusoma. Wakati mwingine wazazi wanasingiziwa hawakuwapa elimu kumbe kichwa kilikuwa hakina akili.
Sema family nyingi zinatakiwa kuwafundisha family ujasiliamali katika ngazi ya family kama kilimo, ufugaji, ushonaji, ufundi wa umeme/magari na nyingine na kitu cha mwisho ni kumfundisha mtoto kuwa na pesa yake ya ziada
 
Hivi ukistaafu unawapa mafao yako watoto wako au unayahifadhi na kuwekeza yakusaidie siku za usoni? binafsi nawekeza sana kwenye elimu ya wanangu na kuwafundisha kujitegemea. Mafao nitayatumia na mama yao nikija staafu inshallah
maisha hayana jibu moja
inawezekekana kwa wakati ule fursa za kuwaendeleza hukweza kuwa nazo au hawakuona umakini kwa wakati ule au uliwaendeleza lakini bado wakakosa ajira hivyo ni bora ukawapa mtaji fedha ili upunguze stress za kuwaona wamekaa kama nyanya zinazosubiri mnunuzi.
kwa kufanya hivyo unakuwa umewakopesha kwa staili nyingine wao watakuwa na deni la kukulipa kwa kuangalia afya yako na mahitaji yako muhimu.
 
Hi great thinkers baada ya juzi mwalimu mstaafu kuwapa mitaji wanae pesa zimeanza kutumika kama ifutavyo:

Watoto wa kike wawili wamenunua shamba ekari tano wameshanunua miche ya michungwa wanajiandaa kuipanda.

Wawili wa kike kila mmoja wamenunua vifaa vyote muhimu vya kufungua migahawa ikiwemo meza viti mapoti makubwa chupa za chai sahani wanaendeleza na kuboresha migahawa walikuwa wakifannya hivyo awali.

Mwalimu kanunua machine ya kutotolesha vifaranga anaboresha banda lake la kuku na bata pia mbuzi.Mdogo wao wa mwisho wamempeleka Veta Tanga kusomea mechanics.Nitaendelea kuwapa updates.
kampuni ya ushauri au benki zinatakiwa ziwekeze kwa watu kama hawa ikiwa ni pamoja na kufanya documentary ya kila hatua na kuwashauri vizuri jinsi ya kusimamia biashara na shughuli zao ili jamii ijifunze na kuwa na maisha mazuri siku zijazo.
 
maisha hayana jibu moja
inawezekekana kwa wakati ule fursa za kuwaendeleza hukweza kuwa nazo au hawakuona umakini kwa wakati ule au uliwaendeleza lakini bado wakakosa ajira hivyo ni bora ukawapa mtaji fedha ili upunguze stress za kuwaona wamekaa kama nyanya zinazosubiri mnunuzi.
kwa kufanya hivyo unakuwa umewakopesha kwa staili nyingine wao watakuwa na deni la kukulipa kwa kuangalia afya yako na mahitaji yako muhimu.
kwa style hiyo kama wakifilisika na mzee afya haiku poa na fedha hana inakula kwake
 
Hi great thinkers baada ya juzi mwalimu mstaafu kuwapa mitaji wanae pesa zimeanza kutumika kama ifutavyo:

Watoto wa kike wawili wamenunua shamba ekari tano wameshanunua miche ya michungwa wanajiandaa kuipanda.

Wawili wa kike kila mmoja wamenunua vifaa vyote muhimu vya kufungua migahawa ikiwemo meza viti mapoti makubwa chupa za chai sahani wanaendeleza na kuboresha migahawa walikuwa wakifannya hivyo awali.

Mwalimu kanunua machine ya kutotolesha vifaranga anaboresha banda lake la kuku na bata pia mbuzi.Mdogo wao wa mwisho wamempeleka Veta Tanga kusomea mechanics.Nitaendelea kuwapa updates.
 
sasa kama kuna eneo alikosea kwa kuwekeza kwa watoto wafanyaje
 
Back
Top Bottom