Mrejesho wangu wa tangazo la kutafuta mume humu

Mnamo mwaka jana mwezi wa 8 nliweka tangazo la kutafuta mume humu ndani nikarudia tena February mwaka huu, nilipata pm nyingi nyingi tu na nlizijibu kadri ya uwezo wangu.

Nilibahatika kuonana na wakaka wa wawili, hawa ni watu wazima kidogo miaka yao kuanzia 35 na kuendelea wa kwanza tulikutana Magomeni tukaongea kupeana basic intro, wa pili tulionana alikuja mitaa ya nyumbani.

Ila hao wote nikiri tu walikuwa wanasisitiza ngono, muingiliano kimwili hata hatujajuana kivile na baadhi ya vitu hatujafahamiana wala kujuana tukaishia hewani.

Kwa kifupi ni kuwa humu kutafuta mume huwezi pata zaidi ya sex partner wanaume ni kama vile wanakuwa wanawinda wanawake, anyway kibongo bongo online dating bado sana, najiandaa kesho kwenda equity bank kufungua akaunti na kujiunga na online transactions nilipie dating sites za mambele huko naamini nitapata mume na nitaleta mrejesho humu.

Nadhani mtajiuliza wht online si mnajua tena single maza ubusy na nini na nini.
Kwa hiyi ulikuwa unataka mtu ambae mtaenda kutangaza ndoa bila kugegedana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom