GEMO
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 250
- 277
Zabibu imekosa soko wakulima wanalia! Hizi ni changamoto katika uzalishaji muhimu kuchunguza soko Kabla ya kuwekeza!Kuacha kazi ili ujiajili unahitaji uwe na akili maalumu, watu wana Mahindi yanaozea ndani hayana soko, nimeshuhudia Songea mwaka Jana mamia ya heka za mbaazi Wakulima wamegoma kuvuna, sababu gharama za kuvuna ni kubwa kuliko bei ya mbaazi.
Kuna Dada yangu aliacha kazi eti anaenda kulima matikiti, kilio alichonacho sasa....
Tuwe tunafuatilia siasa kidogo, wengine alipoingia tu Mtukufu kwa kauli zake za mwanzo tuliona ana mtazamo mbaya na secta binafsi, na ndio kinachotokea.
Soko limeyumba sana
Soko Soko Soko......