Wakuu habarini za majukumu! Ni karibu miezi 2 sasa toka nilipotoka Dar na kujielekeza Morogoro eneo la Kisaki kutafuta riziki ya familia kwenye Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Umeme.
Wakuu huu mradi ni mkubwa sana ila utaratibu wa kuchukua wafanyakazi hasa get la Kisaki ni mbovu sana.
Wajumbe na viongozi wa kijiji hiki ndio wanaoamua nani achukuliwe na nani aachwe. Hivyo kama hauna ile kitu inaitwa Rupia basi utaendelea kuchina huku watu unaona wanaingia tu.
Mimi kwa kuwa ni maskini sina kitu, nimeamua nirudi nyumbani angalau labda nikiwa huko naweza kupata hata kibarua cha kumsaidia Fundi familia ikapata riziki kuliko kukaa huku bila ramani yoyote huku watoto wakifa njaa.
Wakuu Mimi ni Fundi Chuma (steel fixer) ila kama kuna mtu ana kibarua chochote basi anipe nipate riziki ya watoto.
Asanteni
Nitoe tahadhali kama huna mipango ya chini chini usipoteze nauli yako