sabuwanka
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 690
- 751
Mwaka 2016 mfumo wa maisha ulibadilika baada ya Serikali mpya kuingia madarakani! Vijana wengi tulijikita katika kilimo na ufugaji baada ya motivational speaker kutuhakikishia tutapata utajiri bila kutoa jasho
Nami nikaanza na nguruwe wenye mimba 3. Mwanzoni hakukuwa na changamoto sana ila shida ilianza walipozaa! Asikwambie mtu kulisha nguruwe ni kipawa toka mbinguni
Walikuwa wanakula nikanunua gunia 150 za pumba! Walikula mpaka zikaisha kukua hawakui ipasavyo, huku nimeaminishwa nguruwe wa miezi 6 anafikisha kilo 100! Motivational speaker Mungu anawaona
Nilikuja kugundua ndani ya miezi 6 nguruwe wana kilo 30-40! Bei ya walanguzi uchwara ni laki hadi laki na nusu! Ukitaka faida uchinje uuze nyama! Ilifikia gunia la pumba 2017 linauzwa elfu 10 na linaliwa siku 1
Yaani kwa mwezi nguruwe wanakula laki 3! God forbid!!! Nikagundua nimekuwa mzalishaji mkubwa wa mbolea badala ya nguruwe! Nikaamua kupunguza cost za vyakula kwa kuanza kilimo cha matikiti ili nikiuza yanayobaki madogo madogo nilishie nguruwe
Hiyo nayo ikawa biashara kichaa, unalima unaivisha vizuri walanguzi wanakuja na bei ya 700- 1000 shambani, unakuwa unarudisha tu mtaji na wakati mwingine mtaji haurudi
Nikaona nitembelee masoko ya stereo Dar, Buguruni, Mwanza, Kahama na Dodoma! Huko nako nikaamua kupeleka mzigo mwenyewe, madalali Mungu anawaona
Kila tikiti ukiuza dalali anakula 200! Matikiti mazuri yakiisha inabidi umwachie dalali auze taratibu na ili kupunguza gharama na kuokoa muda umamwachia mzigo
Utaambiwa yalioza, yalishuka bei!! Bla bla nyingi. Nikaona ujinga biashara ya tikiti na ufugaji wa nguruwe haina uwiano kama tunavyoaminishwa kwenye makaratasi na forum kibao
Nikahamia ufugaji wa ng'ombe wa maziwa! Mwanzoni kabla ya kuzaa changamoto za kulipa mshahara mfanyakazi, chakula nk. Lakini baada ya kuzaa! Nakamua siku 300 na kwa kweli ng'ombe wameniweka mjini na ninawaheshimu! Wakianza kukamuliwa ile asubuhi au jioni mlio wa maziwa kwenye ndoo kwangu ni Bora kuliko mlio wa ATM ikiwa inatoa pesa
Nikiwa maumwa pesa inaingia, nikiwa mzima pesa inaingia. Changamoto kubwa ni ma bwana mifugo, utunzaji wa nyasi na wanahitaji eneo kubwa! Ila nguruwe na matikiti pasua kichwa