Mrejesho: Ufugaji wa nguruwe, kilimo cha matikiti maji na ufugaji ng'ombe wa maziwa

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Mwaka 2016 mfumo wa maisha ulibadilika baada ya Serikali mpya kuingia madarakani! Vijana wengi tulijikita katika kilimo na ufugaji baada ya motivational speaker kutuhakikishia tutapata utajiri bila kutoa jasho

Nami nikaanza na nguruwe wenye mimba 3. Mwanzoni hakukuwa na changamoto sana ila shida ilianza walipozaa! Asikwambie mtu kulisha nguruwe ni kipawa toka mbinguni

Walikuwa wanakula nikanunua gunia 150 za pumba! Walikula mpaka zikaisha kukua hawakui ipasavyo, huku nimeaminishwa nguruwe wa miezi 6 anafikisha kilo 100! Motivational speaker Mungu anawaona

Nilikuja kugundua ndani ya miezi 6 nguruwe wana kilo 30-40! Bei ya walanguzi uchwara ni laki hadi laki na nusu! Ukitaka faida uchinje uuze nyama! Ilifikia gunia la pumba 2017 linauzwa elfu 10 na linaliwa siku 1

Yaani kwa mwezi nguruwe wanakula laki 3! God forbid!!! Nikagundua nimekuwa mzalishaji mkubwa wa mbolea badala ya nguruwe! Nikaamua kupunguza cost za vyakula kwa kuanza kilimo cha matikiti ili nikiuza yanayobaki madogo madogo nilishie nguruwe

Hiyo nayo ikawa biashara kichaa, unalima unaivisha vizuri walanguzi wanakuja na bei ya 700- 1000 shambani, unakuwa unarudisha tu mtaji na wakati mwingine mtaji haurudi

Nikaona nitembelee masoko ya stereo Dar, Buguruni, Mwanza, Kahama na Dodoma! Huko nako nikaamua kupeleka mzigo mwenyewe, madalali Mungu anawaona

Kila tikiti ukiuza dalali anakula 200! Matikiti mazuri yakiisha inabidi umwachie dalali auze taratibu na ili kupunguza gharama na kuokoa muda umamwachia mzigo

Utaambiwa yalioza, yalishuka bei!! Bla bla nyingi. Nikaona ujinga biashara ya tikiti na ufugaji wa nguruwe haina uwiano kama tunavyoaminishwa kwenye makaratasi na forum kibao

Nikahamia ufugaji wa ng'ombe wa maziwa! Mwanzoni kabla ya kuzaa changamoto za kulipa mshahara mfanyakazi, chakula nk. Lakini baada ya kuzaa! Nakamua siku 300 na kwa kweli ng'ombe wameniweka mjini na ninawaheshimu! Wakianza kukamuliwa ile asubuhi au jioni mlio wa maziwa kwenye ndoo kwangu ni Bora kuliko mlio wa ATM ikiwa inatoa pesa

Nikiwa maumwa pesa inaingia, nikiwa mzima pesa inaingia. Changamoto kubwa ni ma bwana mifugo, utunzaji wa nyasi na wanahitaji eneo kubwa! Ila nguruwe na matikiti pasua kichwa
 
Asante sana umeeleza kwa ufasaha kabisa kutokana na uzoefu! Mimi hayo yoote yaliwahi kunitokea! Motivational speakers Mungu anawaona! Hawa jamaa wanaenda kwenye mitandao wanatafuta notice zinazohusu ufugaji wa wanyama lengwa na ulimaji wa mazao lengwa lengo lao ni kutangaza seminar (training) ili wapige hela kwa kila kichwa cha washiriki.

Akitarget washiriki let say 100 na kila mshiriki akilipa (mara nyingi au kwa wastani wa wengi) 30,000 atapata million 3 akiondoa gharama za ukumbi na makarablasha mengine hakosi million 2 ndani ya siku mbili au tatu.

Jamani tushtuke! Kwa nchi zetu za kiafrika Tanzania ikiwemo kinatochoturudisha nyuma ni soko ulia ambalo halijadhibitiwa kibiashara ambapo baada ya kuvuna mazao au wanyama ukipeleka sokoni unakuta limejaa bidhaa hiyo na kukosa wateja kupelekea kuuza kwa hasara!

Nchi za mfumo wa ubepari unaingia mkataba na mnunuzi kabla ya kulima au kufuga ili kujihakikishia kurudisha gharama za uzalishaji! Hata hivyo inabidi uweke dhamana kwa mnunuzi kama utashindwa kusupply. Hii ndo njia pekee itakayowafanya wajasiriamali wa kilimo na ufugaji kutoka.
 
Hongera sana ndugu yangu kwa kujikwamua kimaisha kwa ufugaji, hii fursa ni nzuri sana iwe kijijini iwe mjini umakini tu ndo unahitajika, katika changamoto yako ya chakula vp hujawai jifunza mbinu ya kutumia hydroponic fodder, nasikia hizi zinapunguza sana gharama ya chakula kwa mifugo.
 
Mwaka 2016 mfumo wa maisha ulibadilika baada ya Serikali mpya kuingia madarakani! Vijana wengi tulijikita katika kilimo na ufugaji baada ya motivational speaker kutuhakikishia tutapata utajiri bila kutoa jasho!

!

Ukisikia ujinga ndio huu, kwa hiyo na wewe kwa akili yako finyu ukaamini unaweza kulima na kufuga bila kutoa jasho?
 
Pole na hongera sana kwa kulifanyia jambo kazi, maana wengi tunaongea sana kutekeleza hakuna....

Mi ninachoweza kusema ni kuwa, Ukifocus ktk kitu kimoja ni rahisi kutoka kuliko kubadilibadili biashara, utaconcentrate Sana na utajua utatue vipi changamoto zitakazokukabili kwa kusoma zaidi, kuulizia waliokwishanya, kuona nk nk..ninachoona hapa Katika mradi wako wa nguruwe cha kwanza hukufanyia utafiti wa kutosha ni kuhusiana na mbegu bora ya kufuga, eneo ulipo mjini VS Kijinini nk, njia za jinsi ya kupunguza gharama za ulishaji.

Aina ya ujenzi WA banda pia ni factor muhimu mno no mno..Kuna vitu ulimiss, baba yangu huu ni mwaka WA 35 anafuga nguruwe na anauza Sana tu na kupata pesa za kumtosha, zamani ilikua kama wewe six months kg 30, sasa hivi kaimprove Sana tu! Hadi Kuna kipindi alikua anauzia wachina laki 3 nguruwe WA miezi mi2, alikua anawaambia siuzi nguruwe mtoto wakawa wanambembeleza akasema bila Laki 3 siuzi, aliuza Sana hicho kipindi...

MOTIVATIONAL SPEAKERS hukupa mwanga sasa wewe kama wewe inapasa kuingia chimbo zaidi, unajiongeza na wewe mwenyewe pia kuona kama kuna ukweli ama lah, all in all Mi nawapenda coz wanahamasisha...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika suala la nguruwe siyo kwamba ndio kila mtu akianza kufuga atapata effects kama ulivyopata wew, nguruwe siyo kwamba anahitaji hayo2 ili akue, kuna mahitaj mengine ambayo ulikuw huyatimizi, ikiwemo ratio ya msosi kwa siku,

Ungejarib kupata utaalam zaid kwa wazoefu & ma expert wa kilimo, dawa zina participate pakubwa sana katika ukuaji wa nguruwe, n.k
 
Katka suala la nguruwe siyo kwamba ndo kila mtu akianza kufuga atapata effects kama ulivyopata wew, nguruwe siyo kwamba anahitaji hayo2 ili akue, kuna mahitaj mengine ambayo ulikuw huyatimizi, ikiwemo ratio ya msosi kwa siku,

Ungejarib kupata utaalam zaid kwa wazoefu & ma expert wa kilimo, dawa zina participate pakubwa sana katika ukuaji wa nguruwe, n.k
Ng'ombe wa Maziwa ndiyo mpango mzima.Una mnunua Leo,muda huohuo anaanza kukurudishia hela yako
 
Pole sana mkuu,yaliyokukuta kwenye nguruwe
yaliwahi kunikuta.Ila kuna mfugaji ameniambia
kuwa nilikosea,nguruwe mmoja anatakiwa kula kilo moja
ya pumba kwa siku.muda wote uliobakia anatakiwa apewe maji ya kutosha.

Na ikitokea akawa mzembe wa kula,jitahidi uondoe hayo masalia
ili asizoee kula kila wakati.Hayo mabaki kama unafuga bata au kuku wawekee hayo mabaki
na nguruwe mpe maji tu mpaka kesho yake utakapompa haki yaki ya kilo moja ya pumba.
Hii inasaidia kwamba kesho yake ukimuwekea hiyo kilo moja atakula na kumaliza
maana atakuwa na njaa ya jana.
pia epuka mtindo wa kuwawekea nguruwe vitu mbalimbali kama vile mabaki ya vyakula
au makabichi n.k.ukifanya hivyo unamzoesha kula kila mara bila mpangilio
ambao utakughalimu,maana wakihisi njaa watakupigia kelele na kukukosesha amani.

Natarajia kufuga tena kwa kufuata maelekezo hayo,nione kama nitaweza
kupata faida.Hayo maelezo hapo juu nilipewa na mdau anayefuga
ambaye nilimtembelea nikaona mabanda yake ndo akanipa siri hiyo.
 
Sawa, lakin siyo kwamba nguruwe ndo inatia hasara kila wakati, kuna watu wamefanikiwa pakubwa sana kwa ufugaji wa nguruwe, lifespan ya nguruwe mpaka anafikia mda wa kuzaabn miezi6-7 anakuwa tyr kwa kubeba mimba na anazaa watoto weng kama unavyojua, nkiwa field nmetembelea wafugaj weng sana ikiwa wengine ni mixer, ukifanikisha management vzuri, walalipa sema wako more susceptible na magonjwa mengi na wanahitaj routine flan hiv ya kuwapa dawa that's why sometimes hawalet ile expected outcomes
Ng'ombe wa Maziwa ndiyo mpango mzima.Una mnunua Leo,muda huohuo anaanza kukurudishia hela yako

Sent using Jamii Forums mobile app
A
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom