Mrejesho: Nipo Morogoro, maisha yanazidi kunichakata haswaaa! Natafuta kazi yoyote halali

Merchante

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,291
2,679
Wanabodi!

Kheri ya sikukuu ya Eid (Eid Mubarak).

Ni matumaini yangu wengi wetu tuko salama na kwa wale wenye matatizo mbalimbali kwa imani yako utapata kupona.
Wakuu yeyote mwenye connections ya kazi yoyote halali naomba anisaidie. Maisha yanazidi kuninyoosha kisawa sawa! Mitihani ni mingi sana,ila natambua kuwa "GOD PULLS US BACK TO SHOOT US FORWARD".

Kwa suala la elimu nina Shahada (Degree), pia nina uzoefu katika Data collection & management, Data analysis kwa (SPSS, STATA n.k). Kwa kifup ni kuwa niko vizuri katika suala zima la kufanya RESEARCH.

Zaidi, nina mafunzo ya kusimamia miradi mbalimbali ya serikali na binafsi, mfano: Miradi ya ujenzi wa Mabweni, Madarasa, Zahanati, Mabwawa, Barabara za jamij n.k).

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Mkuu endelea kupambana wahitaji zaidi yako ni wengi kuliko unavoweza kuzani kuna wenye kazi wana mikopo madeni majukumu na wanapitia mengi na wanamisongo ya mawazo wanatamani waache kuajiriwa na hawajui watafikia vipi ndoto

endeleza tu mapambano utapata fursa tambua muda ndio jawabu la hitaji la mtu yape muda matamanio ya moyo wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiwanda cha sukari cha mtibwa pale turiani, kinatafuta vijana kwa ajili ya msimu mpya wa mavuno ya miwa. Kama unaweza kufanya kwa muda nenda hapo kiwandani kwao chap ukiwa na kitambulisho cha taifa au mpiga kura. Malipo ni sh 6000 kwa siku, chakula, malazi na vingine ni bure. Wahi mzee ujishikize kwa muda huku ukiwaza nini cha kufanya
 
Shukrani sana mkuu.

Asante sana mkuu, nakwenda nakachukue hiyo fursa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nitakuwa nje ya mada kidogo lakini Nafikiri haya Mawazo yatakusaidia kuna kitu kinaitwa kusudi(purpose) kwenye maisha yaani kila mtu aliyepo duniani ana kusudi lake

Sasa basi kwenye maisha haya bila kujua kusudi lako ni nini utashika kila mahali na bado utateleza lakini Utakuta katika kila mahali unaposhika panateleza wengine ndio walipo fanikiwa hapo

Ninapokuwa naongelea kuhusu kusudi naongelea ninamaanisha ni kuna kitu ambacho unaweza kukifanya kwa masukumo mkubwa wa ndani bila kusukumwa na mtu na bado ukajisikia raha lakini ukiwa ukifanya hicho bado unalipwa mfano uimbaji wa diamond yeye anajisikia raha kufanya vile na bado analipwa lakini ndio kusudi lake ,Ronaldo anacheza Mpira kwa kuwa hilo ndio kusudi lake naanaishi kusudi lake na bado analipwa

Sasa basi tafuta kusudi lako ambalo utalifanya na ukagusa maisha ya watu Hakika Naamini utalipwa maana utagusa maisha ya watu

Na uzuri wa kusudi Unakuwa unauwezo nacho hicho natural yaani huitaji kusukumwa ufanye kwa ubora lakini natural
 
kiwanda cha sukari cha mtibwa pale turiani, kinatafuta vijana kwa ajili ya msimu mpya wa mavuno ya miwa. Kama unaweza kufanya kwa muda nenda hapo kiwandani kwao chap ukiwa na kitambulisho cha taifa au mpiga kura. Malipo ni sh 6000 kwa siku, chakula, malazi na vingine ni bure. Wahi mzee ujishikize kwa muda huku ukiwaza nini cha kufanya
Elf 6000 af inapitia CRDB mkuu bora aendelee kupambana. Kimsingi biashara zote hazikuwa nzuri kipindi hiki cha kuanzia mwezi wa 3 hadi sasa kutokana na janga la korona lilopelekea mdororo wa kiuchumi na shighuli nyingi za uzalishaji kusitishwa kwa muda ila kwa sasa hali itatengamaa kutokana na kufunguliwa kwa shughuli za kimichezo, na vyuo vikuu. Kama wateja wako walikuwa wanachuo basi utarudi kwenye mstaru chap kwa haraka kuliko kwenda kuwa MIGRANT LABOR huko mtibwa.
Huo ni mtazamo wangu. Sijapinga hoja yoyote iliyonitangulia wala zitakazoendelea kutolewa na wana jamvi.
Naomba kuwasilisha.
 
Sure aende pale nimepita juzi nimekuta pia kilombero Wana vuna miwa na wafanyakazi kazi yao ni kukata na kukusanya miwa
 
T
Mimi nitakuwa nje ya mada kidogo lakini Nafikiri haya Mawazo yatakusaidia kuna kitu kinaitwa kusudi(purpose) kwenye maisha yaani kila mtu aliyepo duniani ana kusudi lake

Sasa basi kwenye maisha haya bila kujua kusudi lako ni nini utashika kila mahali na bado utateleza lakini Utakuta katika kila mahali unaposhika panateleza wengine ndio walipo fanikiwa hapo

Ninapokuwa naongelea kuhusu kusudi naongelea ninamaanisha ni kuna kitu ambacho unaweza kukifanya kwa masukumo mkubwa wa ndani bila kusukumwa na mtu na bado ukajisikia raha lakini ukiwa ukifanya hicho bado unalipwa mfano uimbaji wa diamond yeye anajisikia raha kufanya vile na bado analipwa lakini ndio kusudi lake ,Ronaldo anacheza Mpira kwa kuwa hilo ndio kusudi lake naanaishi kusudi lake na bado analipwa

Sasa basi tafuta kusudi lako ambalo utalifanya na ukagusa maisha ya watu Hakika Naamini utalipwa maana utagusa maisha ya watu

Na uzuri wa kusudi Unakuwa unauwezo nacho hicho natural yaani huitaji kusukumwa ufanye kwa ubora lakini natural
The purpose works most on talent i bet, lkn pasi na kipaji cha kimichezo ama muziki ni changamoto sana kukitambua na kuki-utilize kwa mazingira yetu, lets say ana kipaji cha biashara, ili aweze kukitumia kimlipe changamoto ni lukuki
 
Mtu umeacha dar sababu ya changamoto ya maisha kuwa juu,haya sawa....Unaenda mkoa au sehemu ambayo target ya soko lako inategemea kundi moja tu(kwako ni wanachuo)....Kwa nini usiende mikoa iliyochangamka kibiashara kama Mwanza au Mbeya hivi ukapiga mishe zako? Nina rafiki yangu hivi anauza CD maeneo ya dampo,pale movement ni 24/7 na hajawahi kuniomba nimpige Tafu.. Mwingine anapaka rangi kucha za wadada na kusugua miguu yao pale makoroboi,naye shida ndogondogo hana!!! Mnasubir sehemu hadi maisha yapande sana gemu iwe taiti ndo muifikirie!! Ngoja Wanyarwanda wawasaidie!!!
 
Mimi nitakuwa nje ya mada kidogo lakini Nafikiri haya Mawazo yatakusaidia kuna kitu kinaitwa kusudi(purpose) kwenye maisha yaani kila mtu aliyepo duniani ana kusudi lake

Sasa basi kwenye maisha haya bila kujua kusudi lako ni nini utashika kila mahali na bado utateleza lakini Utakuta katika kila mahali unaposhika panateleza wengine ndio walipo fanikiwa hapo

Ninapokuwa naongelea kuhusu kusudi naongelea ninamaanisha ni kuna kitu ambacho unaweza kukifanya kwa masukumo mkubwa wa ndani bila kusukumwa na mtu na bado ukajisikia raha lakini ukiwa ukifanya hicho bado unalipwa mfano uimbaji wa diamond yeye anajisikia raha kufanya vile na bado analipwa lakini ndio kusudi lake ,Ronaldo anacheza Mpira kwa kuwa hilo ndio kusudi lake naanaishi kusudi lake na bado analipwa

Sasa basi tafuta kusudi lako ambalo utalifanya na ukagusa maisha ya watu Hakika Naamini utalipwa maana utagusa maisha ya watu

Na uzuri wa kusudi Unakuwa unauwezo nacho hicho natural yaani huitaji kusukumwa ufanye kwa ubora lakini natural
Asante sana mkuu kwa ushauri wako, nafikiri ushauri wako una manufaa si kwangu peke yangu bali hata msomaji au wachangiaji wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elf 6000 af inapitia CRDB mkuu bora aendelee kupambana. Kimsingi biashara zote hazikuwa nzuri kipindi hiki cha kuanzia mwezi wa 3 hadi sasa kutokana na janga la korona lilopelekea mdororo wa kiuchumi na shighuli nyingi za uzalishaji kusitishwa kwa muda ila kwa sasa hali itatengamaa kutokana na kufunguliwa kwa shughuli za kimichezo, na vyuo vikuu. Kama wateja wako walikuwa wanachuo basi utarudi kwenye mstaru chap kwa haraka kuliko kwenda kuwa MIGRANT LABOR huko mtibwa.
Huo ni mtazamo wangu. Sijapinga hoja yoyote iliyonitangulia wala zitakazoendelea kutolewa na wana jamvi.
Naomba kuwasilisha.
Uko sahihi mkuu,yani hiyo 6000 per day unamaanisha ni 180,000 kwa mwezi. Nalipa Kodi,maji na umeme,bado ile michango midogo midogo ya usafi,n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwa hizo changamoto unazopitia. Nina imani Mwenyezi Mungu anakupa hiyo mitihani ili uimarike zaidi. Hata sisi baadhi yetu humu tumepambana kweli kweli mpaka kufikia hapa tulipo! Usikate tamaa.

Wapo wadau humu ambao wataguswa zaidi na changamoto zako. Inshallah wanaweza wakakusaidia.
 
kiwanda cha sukari cha mtibwa pale turiani, kinatafuta vijana kwa ajili ya msimu mpya wa mavuno ya miwa. Kama unaweza kufanya kwa muda nenda hapo kiwandani kwao chap ukiwa na kitambulisho cha taifa au mpiga kura. Malipo ni sh 6000 kwa siku, chakula, malazi na vingine ni bure. Wahi mzee ujishikize kwa muda huku ukiwaza nini cha kufanya
Hiyo kazi unaifahamu vizuri lakini?
 
Elf 6000 af inapitia CRDB mkuu bora aendelee kupambana. Kimsingi biashara zote hazikuwa nzuri kipindi hiki cha kuanzia mwezi wa 3 hadi sasa kutokana na janga la korona lilopelekea mdororo wa kiuchumi na shighuli nyingi za uzalishaji kusitishwa kwa muda ila kwa sasa hali itatengamaa kutokana na kufunguliwa kwa shughuli za kimichezo, na vyuo vikuu. Kama wateja wako walikuwa wanachuo basi utarudi kwenye mstaru chap kwa haraka kuliko kwenda kuwa MIGRANT LABOR huko mtibwa.
Huo ni mtazamo wangu. Sijapinga hoja yoyote iliyonitangulia wala zitakazoendelea kutolewa na wana jamvi.
Naomba kuwasilisha.
upo sahihi...lakini ni bora ajishkize huko kwenye mavuno kwa mudahuku akicheki ramani nyingine. Pia naamini atapata connection za kutosha akiwa na wadau huko shamba
 
Back
Top Bottom