Mrejesho: Ninadaiwa kodi ya nyumba na sina kazi kwa sasa, msamaria mwema nisaidie

MKONGORO

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
325
263
Habarini za wakati Huu Wana JF!

Jana tar 17/12/2015 Niliweka Uzi Hapa Nikiomba Msaada Kwenu Wasamaria Wema Kunichangia Fedha Ili Niweze Kulipa Kodi Ya Nyumba Au Nichangiwe Bati 12 Ili Nifunike Chumba Kimoja Katika Nyumba Yangu Ya Vyumba 2 Nihamie Kutokana Na Matatizo yaliyonikuta Hadi Kushindwa Kulipa Kodi. Matokeo Ni Kama Ifuatavyo:-

Akaunti Ya Tigo Mpaka Sasa ina Tshs 40,000/=
Akaunti Ya Mpesa Ina Tshs 44,000/=

Western Union Tshs 122,000/=
Moneygram Tshs 120,000/=
Ahadi Watu 3,

Hapa Sitalipa Kodi Tena Ila Naezeka Vyumba Vyote 2 Nihamie Kwangu Mambo Ya Milango Na Madirisha Yatajijua Yenyewe!

Kwa Niaba Yangu Mwenyewe Na Kwa Niaba Ya Familia Yangu Tunasema Asanteni Sana Wana JF kwa msaada wenu mkubwa hakika mmetuepusha na aibu kubwa! Hatuna cha kuwalipa ila MUNGU mwenyewe ndie atakae walipa, wenu Gershom S. Mbanga 0765544791

Asanteni.
 
Mabati ulienda kuchukua?? Maana hapo hujasema kama uliyafuata ama vipi
 
Mabati ulienda kuchukua?? Maana hapo hujasema kama uliyafuata ama vipi

Yeah, kuna mdau wa Kimara aliahidi kumpa bati 12 kuukuu, na mwingine akaahidi kuzifikisha Tegeta maana ana route ya kwenda wazo kuchukua kifusi. Hizo bati siyo za kuacha poti, zitapigwa chumba cha watoto na kuzibwa vizuri tu.
 
Ubarikiwe sana kwa moyo wa shukurani ulio nao!

Pia wabarikiwe wana JF wote.

Nashauri ianzishwe '' JF Fund Board'' kwa ajili kusaidia wenye matatizo. Maana shida haina mwenyewe, leo kwangu kesho kwa mwingine!
 
Mkuu sijaelewa hapo kwenye western union hiyo ni milioni moja na laki mbili au laki moja na ishirini maake huo mkato sijaelewa hapo ulipouweka.

But MSHUKURU MUNGU KWA UPENDO ULIONYESHWA NA HAYA MAMBO YANAPATIKANA TANZANIA AMBAPO MTU ANAEZA KUMSAIDIA MTU ASIE MJUA ..... ASANTEE SANA
 
Mungu awabariki sana wote mliotoa na kuahidi pia nawe kwa kutambua asante kitu cha maana sana.
 
Mungu mkubwa na awazidishie na kuwabariki waliokuchangia.
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom