MREJESHO: Nimeendesha Uber na Taxify kwa gari yangu ndani ya miezi mitatu

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,036
49,640
Wakuu habari.
Kama kichwa kinavyojieleza hapo naomba nilete experience yangu ya kuwa Uber/Taxify Driver kwa kutumia gari binafsi.

Gari ni cc1500 Corolla, na niliifanya kama part-time job sio full time. Mara nyingi nilikuwa naendesha kuanzia Ijumaa to Jumapili, saa 2 usiku hadi saa 12 Asubuhi. Ingawa sio kila weekends but most of them. Na nimefanya kwa muda wa kama miezi mitatu, tokea mwaka jana November/December. Na nilikuwa na Apps zote mbili, Uber na Taxify.

Kwa siku faida nikitoa mafuta na kula mimi, nilikuwa na save kati ya 60,000 hadi 100,000 mambo yakiwa mazuri. Hapo ikiwemo ile hela ya kamisheni (25% kwa Uber) nnayotakiwa ipeleka kwa Uber. Mimi sijawahi kuwapa kusema kweli.

Guys hii biashara ni kuzeesha gari, kujichosha, stress za kuwaza ratings na faida ni kwa ajili ya kupata hela ya kuspend tu siku 2 au 3.

Kwa maana hako ka faida ulikokapata kesho utataka ukasafishe gari (20,000 Car Wash), ununue marashi mazuri ya kwenye gari kuwavutia wateja wakupe high ratings, ununue MB za kutosha maana muda wote laziwa uwe online so unakuta unabakiwa na hela ya chakula tu.

Kwa muda huo wa masaa 10 niliopo online muda mwingi, karibia masaa 7, nakuwa gari inatembea tu. Hapo milage zinaongezeka sana na gari inachakaa sana ukichukulia Watanzania wengi hatukai sehemu rafiki, ila mabondeni sana ambako ukipeleka gari lolote linaweza kutokea. Mfano, nimeshachana Bumper na kusababisha gharama kulitengeneza na kupaka rangi ya Tsh 180,000.

Usiku unakuta wateja ni madogo walevi, miguu juu ya viti na maviatu yao machafu, gari inanuka pombe, halafu wanakutreat cheap sana, yaani kisa wanatoa hela basi ni kero.

Pia Uber maximum ni watu wanne, sasa unakuta kila trip wewe unapakiza watu 3 to wa 4. Gari inakula sana mzigo. Unaichosha sana na wanakaa maporini huko Kimara mabondeni.

Kwa hitimisho, sio biashara mbaya ila ukiwa na gari dedicated kwa hii biashara na sio gari binafsi. Pia, mitaa yako iwe Posta, na uzunguni ambapo pings zinakuwa nyingi so muda wa kuzurura bila abiria unakua mdogo na kazi iwe full time (uwe na dereva wako), na gari zuri liwe na cc ndogo 1300 IST na Vitz, Passo na nyingine za cc990 ni nzuri.

Ila kwa upande wangu, hii kitu sio kwa ajili ya barabara za Tanzania. Inakula sana kwa dereva.
 
Hahaa nimecheka hilo la madogo walevi, na kwel maana haya mambo ya mtandao ma wazee wapi na wapi! Hapo nimekubali ww ni uber member.
 
Ni kweli siyo biashara nzuri, ila siyo mbaya, kwamba wewe na familia mnakula na watoto wanasoma, hata kodi waweza kulipa, jaribu kuacha kusafisha gari kwa 20,000/=, kwanini usisafishe mwenyewe, mazoezi mazuri mno, tena wewe ndio utalisafisha vizuri zaidi..
Hahaaa mkuu umenikumbusha siku nimepewa hela nikaoshe gari

Nikaamua tu nioshe mwenyewe jamaa akanikuta nikamwambia nafanya mazoezi. Mara moja moja siyo mbaya.
 
Ni ujinga kwenda kusafisha gari 20
Kabisa, tena huwa nawaona wanavyosafisha, maji yao mara nyingi machafu, kifagio na kizoleo kimechoka, au wanatumia matambara tu, matambara ya kuoshea gari hujuwi lipi la kioo lipi la matairi, swala la usalama wa vitu vyako ndani ya gari wawa mdogo sana, kuzoena na hao jamaa hapana kabisa, wanaweza hata kukuliza gari siku...kifupi siwaamini, ni heri gari liwe chafu mpaka ukipata muda mkuu..
 
Aisee ulitakiwa uwe na limit yako aisee ikifika 50000 upumzike ukishindana na rizki sana unajiumiza mwenyewe

Mkuu wazo zuri. Ila nakaa nyumba ya kupanga. Ikifika saa 4 wanafunga geti. Na mimi sina mtu ambae ninaweza mpigia simu au mgongea dirishani afungue geti kwa ndani niingie. So kwakua nilikua nimeamua hivo, nikawa kama popo, nalala mchana, usiku nakesha.
 
60,000×30×3= 5,400,000/= net profit(minimum) na bado unalalamika...

Hiyo corrolla yako ulinunua bei gan?

Brother. Sifanyi siku zote za wiki. Nafanya siku 3 tu weekends,. Na sio kila weekends. Nilikua nafanya katika mwezi kama weekends 2 au 3.

Ishu inakuja kwenye service mzee. Leo bampa limechanika, kesho muda wa kuchange oil, keshokutwa lingine tena. Hela haiji kubwa kama hesabu ulizoandika hapo.
 
Back
Top Bottom