MREJESHO: Nimeendesha Uber na Taxify kwa gari yangu ndani ya miezi mitatu

Wewe ni jipu nimetembelea vijiwe vingi vya taxi madereva wazee mpaka vijana wako very positive na uber na inavyowasaidi...
Umetembelea vijiwe vingapi vya taxi? Hao na wa pale airport ndo wanalia na UBER maana trip waliokuwa wanatoza 15,000/= UBER wanaenda kwa 3,000/=
 
Brother. Sifanyi siku zote za wiki. Nafanya siku 3 tu weekends,. Na sio kila weekends. Nilikua nafanya katika mwezi kama weekends 2 au 3.

Ishu inakuja kwenye service mzee. Leo bampa limechanika, kesho muda wa kuchange oil, keshokutwa lingine tena. Hela haiji kubwa kama hesabu ulizoandika hapo.
Shida ya watu hawapigi hesabu za net profit wao wanangalia mapato bila expenses zingine
 
Naunga mkono hoja. Gari binafsi ukiipandisha abiria ni matatizo tu, Hasa Ukiwa mtu unayependa usafi kwenye gari (kama mimi).

Abiria wanachafua sana gari, hasa kwenye carpets na seats.
Wanatupa vitu walivyotumia(eg chupa) humohumo.

Kama mtu unaipenda gari yako kweli (private car), then Make it YOURS.... Biashara fanya na gari lingine .
 
Uber taxi mbweni-kariakoo = 11,000/= hapo utoe 2,500 (25%) ya Uber, mafuta, bundle, airtime.
 
Kawe-Airport =10,000/= uber 25%=2,500 tsh....mafuta, bundle, airtime, pesa ya tajiri=****???
 
Nilikua nafanya weekend tu. Kwakua weekdays nina kazi nyingine sikutaka kuchanganya mambo.
Nikianza Ijumaa labda saa 2 au 3 (Huu muda foreni inakua low kidogo) basi naenda maeneo kama UDSM, Mabibo Hostels, Mlimani City na Ubungo Bus terminal kwakua kuna Pings nyingi. Hafu napiga hadi saa 12 asubuhi ndio naenda kulala. Ijumaa, uta save kama 60 hivi nikitoa mafuta kwakua Ijumaa sio siku nzuri sana.

Jumamosi na Jumapili kidogo nzuri. kwanza foreni zinawahi kuisha jioni. kuanzia saa 3 barabara ni nyeupe. Pia watu wengi sana wanaenda out. So ukiwa unavijua viwanja sana hukosi pings kila baada ya dakika chache.

Kwahiyo kwa mwezi nikifanya weekends 3 hivi, kale ka hela ulikokapata, unakuta unakatumia kwa matumizi ya kawaida tu, huwezi save. Unavoanza Uber/Taxify jioni gari yako inakua safi tu, Ila kufika asubuhi gari inakua chafu sana, ndani na nje.

Kuosha mwenyewe wazo zuri, ila kumbuka AC ilikua ON muda mwingi, so kunakua na vumbi sana kwenye Airclear ya AC lazima ikapulizwe, pia ndani lazima ipitishwe vacuum cleaner maan wale abiria wengi sio wastaarabu wale wa usiku.

Kuna abiria wanajielewa sana. Akifika karibu na kwake anasema ishia hapa hapa kule barabara haipitiki mimi nitatembea. Au anakuachia hadi Tip.

IlA nilichojifunza ni kua mstaarabu sana kwenye gari la mtu, ata kama nalipia hela au nimepewa lift, roho inakua inakuuma sana kuona mtu ana panda na bia au chakula kwenye gari lako, ila ndio hivo huwezi mfukuza abiria.
Biashara ipo hivyo lazima pawe na depreciation kwenye assets. Huwezi kufanya biashara ya taxi halafu gari lako lisichafuke, mileage isiwe juu, isihitaje frequent services na usikutane mteja mkorofi. Kitu pekee kinachomake sense labda ni hiyo rate ya uber and taxify wangewapunguzia.
 
Back
Top Bottom