Mrejesho,.. Nilimpa mtihani mdogo ulimshinda akaamua kumtukana mke wangu

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Nafaham wengi wenu mliwahi kuona uzi wangu wenye mada iliyopo hapo juu.
Ishu ni kwamba yule mwanamke bado amekaa siku nenda siku rudi kaamua kurudi tena lakini mimi bado msimamo wangu ni ule ule narudia msimamo wangu ni ule ule simtaki tena na namchukia.

Juzi kati alikuja na mbwembwe nyingi,.. "Mimi kwasasa sina tena mda wa kukufata tena maana nimepata mtu mwengine, ananijali sana tena sana na yupo South Africa".

Sasa nikajaribu kumwambia kwamba wewe utaishia kulaliwa kama kuku lakini hautakuja kuolewa abadan, akawa ananiambia namtia gubu.
Nilizidi kumshambulia na kumwambia, nafasi uliyoipoteza kwangu hautaipata tena kwa mwengine. Na kama huamini huyo unaeniambia anakupenda na anakuja likizo, ukikubali kukulala tu umekwisha.

Nikamwambia sikwambii kwasababu ya wivu,.. Hapana, nakupendelea mema... Kama unataka kuolewa olewa ila ukilala nae umekwisha jeuri yako.
Tulikata mawasiliano kitambo... Juzi nikaona friend request kupitia account mpya ila jina lile lile... Mmmh ,.. Nikabaki kujiuliza huyu kafata nini tena kwangu?

Basi nikamkubalia urafiki wetu ukaendelea wa kwenye mtandao... Ikabidi aniulize kwamba bado nina hasira ila katika story zote akanambia lakini kwasasa amepata mtu mwengine na anampa kampan zake sana masuala ya biashara na huyo mtu ni mwanajeshi na yupo mission kwasasa.

Sasa nikamuuliza, inamaana kuja kuniomba urafiriki ni kuja kunitambulisha kwamba umepata mwanajeshi? Akanijibu, "hapana ni story tu kama umekasirika nisamehe" nikamjibu sijakasirika bali kuna swali langu naomba nikuulize, akanijibu sawa uliza.

Nikamuuliza,..

Mimi: Yule jamaa wa South imekuaje?

Yeye: Yule niliamua kuachana nae maana hatuendani umri wake ni mkubwa.

Mimi: Wakati unaanzisha mahusiano na yeye ulikua umefungwa kitambaa usoni?

Yeye: Hapana, tatizo ni kwamba yule mtu anaishi huko na mke wake, sasa nimeona itanichukua mda mrefu kumsubiri yeye kuja huku.

Mimi nikaacha kama yalivyo...
Nikamwambia hapo nilikwambia kwa ushenzi ulionao hautafanikiwa. Akanijibu kwasasa tuachane na yaliyopita, akanambia amemiss vituko vyangu anatamani tuwe marafiki tu ili akumbuke vile viburubani nilivokua nikimpa kwenye sim wakati nipo mbali nae.

Mimi nikataka kujua huyu mwanamke ana msimamo kama anavojinasibu?
Nikamwambia siwezi kuwa na urafiki labda urafiki wetu nikule ila huyo jamaa yako nitakuachia kama kawaida...
Alikubali ombi langu,.. Nikagundua hapa hamna kitu maana hana msimamo thabiti wa kile anachokisimamia..

Nilimtafutia sababu nikamfanyia visa tukaanzisha ugomvi. Hadi leo ni siku ya nne hatujaulizana chochote,... Ifahamike huyo mwanamke sijawahi kufanya nae mapenzi kwakuwa siko tayari.
 
Shida na Raha... Kwann usichague upande wa Raha na mkeo.

Badala yake Hisia zinajaribu kukuchagulisha upande wa Shida na Mchepuko.?? .

Mkuu, Nje ya Mkeo , mwanamke yoyote kwako Nisawa na Simba wa Porin , huwinda kwa polepole , na kuridhika....

Usimpe nafasi Simba huyo.... ivi unawezaje kua namahusiano na mchepuko?( Mwanamke aloshindwa ) aaaahhhhh Mpende mke wako mkuuu!! Achana na huyo Mshindwaji, utakapomkubalia, ataitafuta ndoa kwa lazima.yale yaleee utaendewa kwa Mganga, Kisha utamsahau Mke wako, watoto wako kisa limbwata la Demu aloshindikana.
 
Mbona mkuu maelezo yanajitoshelezaa.. Ukweli ni kwamba mimi simtaki kabisaa,.. Nakama nilikua namtaka ningekua tayari nishamaliza kila kitu.
 
Mbona mkuu maelezo yanajitoshelezaa.. Ukweli ni kwamba mimi simtaki kabisaa,.. Nakama nilikua namtaka ningekua tayari nishamaliza kila kitu.
Achana naye, huo muda woteeee unaotumia naye kimawasiliano , Nenda umpe Mke wako , kamfanye mwanamke wako afurahi tuu acheke cheke basi siku zisonge mbele.

Ivo videmu huwa vinawatega ivo ivo... sikia ,ukweli nihuu, Km mchepuko ? Au mke wapili ?? Hawa huwa wanakuaga chanzo cha mwanamme kufa !!

Unajua kwann?? Wanajua wee umeoa..kwaiyo atajaribu either akuachanishe na mkeo , au akukamate mzima mzima ,nahayo yote anayafanya huku nayeye akiwa na jamaa ake mwingine ambaye Hajaoa.

Sasa nn huja kutokea?? ukizijua nyakati ulizopo, nyakat zijazo hazitokupa shida.
 
Mkuu nimekusoma ila ukweli ni kwamba yeye ndo anapoteza mda wake sana.
 
Mkuu nimekusoma ila ukweli ni kwamba yeye ndo anapoteza mda wake sana.
Hahaa sawasawa mkuu km umelijua ilo,,, jambo dogo la mwisho nihili..kuna mtu anaweza kukutafuta kwa simu meseji kila saa nakila siku, kimahesab ukajua Anakupenda sana, kumbe mwenzako usikute Hana kazi yakufanya au kajiunga vifurushi nasasa anahisi kifurushi kitaisha buree bureee.

Ila km anakutafuta kwa kina na uzito kweli anapotez muda wake LAKIN usije kaa ukahisi Anania njemaa,,, Kwakua km angekua na njia njema asingeForce sana kua naww ..... Hapo target yake niww kusex naye, mpige picha, kisha azitumie kumuumiza mwanamke wako ....

ACHANA NAKO, NIKAJINGA KAMA WAJINGA WENGINE...yaan anafanana na Mdada wamakamo ya 20-28 alafu anatembea na Mzee mwenye mke na watoto ,anadate nayeee weeeeee mwisho wanaachana akiwa na miaka 33 alafu anaanza kulia Y me ?? Y me?? Hiii hiiiiiii haaaa uwiiiiiii hiiiiii y me sipati mume
 
Shida na Raha... Kwann usichague upande wa Raha na mkeo.

Badala yake Hisia zinajaribu kukuchagulisha upande wa Shida na Mchepuko.?? .

Mkuu, Nje ya Mkeo , mwanamke yoyote kwako Nisawa na Simba wa Porin , huwinda kwa polepole , na kuridhika....

Usimpe nafasi Simba huyo.... ivi unawezaje kua namahusiano na mchepuko?( Mwanamke aloshindwa ) aaaahhhhh Mpende mke wako mkuuu!! Achana na huyo Mshindwaji, utakapomkubalia, ataitafuta ndoa kwa lazima.yale yaleee utaendewa kwa Mganga, Kisha utamsahau Mke wako, watoto wako kisa limbwata la Demu aloshindikana.
Asipo kuelewa anahitaji maombi
 
Hata ww huna msimamo km huyo mwanamke.... akikuhitaji kwa namna nyngne atafanikiwa
 
Kuwasiliana na mpenzi wa zamani ni kuugeuza muwa kuwa mkongojo.. Utaula tu.
 
Nanusa harufu ya lose ball , mkuu nipasie huo mpira unaodunda dunda nitie kitu nyavuni refa alete gozi kati...
 
Sijui kupangilia uandishi wangu binafsi ila nawe mkuu uandishi wa aina hii lazima huyo mdada atakupelekesha tu maana hueleweki na utakuwa huna msimamo kwenye mambo yako kama gentleman
 
Back
Top Bottom