Mrejesho:Ndoto ya kupanda mlima Kilimanjaro,kuendesha gari n.k

maharage ya ukweni

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
1,091
2,000
Asalaam aleykum!
Wanajamvi Kama mnavyojua JF ni jukwaa ambalo watu wanajadiliana na kupeana ushauri wa mambo mbali mbali ya kiuchumi,kisayansi,siasa na kijamii.Hii ni kutokana na ukweli kwamba JF ni jukwaa la kweli ya Great thinkers.
Kwanza ningependa kukumbuahia baadhi ya ndoto ambazo nilisimulia humu na kupata tafasiri zake.1:niliota napanda mti kwa shida Sana na chini yangu kulikua na mtu ananivuta ili nidondoke lakini nilimshinda nguvu na kupanda ule mti mpaka juu lakini kwa bahati mbaya nilivyofika juu mti uliinama hivyo nikalazimika kushuka lakini kabla ya kushuka mbele yangu niliona njia ndefu sana yenye kona nyingi na mbele yake kukawa na mlima Kilimanjaro.Nilijitahidi kupita ile njia kwa shida sana na nilifanikiwa kuupanda mlima,nilivyofika juu ya mlima nilikuta watu wanahangaika kutafuta madini kwenye Mchanga lakini mimi nilivyoingiza tu mkono kwenye ule mchanga nikachomoa Tanzanite na Dhahabu lakini nikawa nazificha ili wenzangu wasipole maana Tanzanite na dhahabu zilikua zinang'aa Sana na kutoa mwanga mkali.Watu walikua wanafanya mambo machafu ya kumchukiza mungu lakini mimi nikawa najitenga nao.
2:Niliota kuna watu wawili wameshuka kwenye gari na kunikabidhi niendeshe lakini sikujua kuendesha ila nilikua najua gia ilipo na breki.Siku nyingine nikaota nimekabidhiwa gari niendeshe lakini bahati nzuri awamu ya pili nikaweza kuendesha na kuingiza gari barabarani.Mwisho siku nyingine nikaota tupo kwenye gari lenye miskani miwili mwenzangu yupo kulia mimi niko kushoto wote tunaendesha gari moja lenye miskani miwili tena mwenzangu kuna mda akataka kugonga gari mbele yetu lakini nilizungusha msikani upande wangu nikaepusha ajari ya kuligonga lile gari mbele yetu .
3:Niliota rais kanichagua kua waziri wa nishati na madini lakini alivyoniita mbele akaniapishe wanachama wa CCM walikasirika sana kwani mimi sikuwahi kua hata mjumbe wa nyumba kumi wala kua mwanachama wa CCM.Watu walikasirika sana na wakawa wananitazama kwa macho ya husda.
Hizo ni baadhi ya ndoto ambazo niliota na kuzisimulia hapa jukwaani na kupewa tafasiri na ushauri wa nini cha kufanya hasa hasa kua karibu sana na mwenyezi mungu kwani inaonyesha mungu anampango wa kipekee na katika maisha yangu.Pia ndoto zote zilionyesha ntapitia kipindi kigumu sana lakini baadae ntafanikiwa kimaisha tena naweza kuja kua kiongozi hapo baadae.Ushauri wangu ni kwamba tusikate tamaa tunapopata mitihani migumu ya kimaisha bali kuzidishe kumuomba mungu kwani hakuna zaidi ya mungu anayeweza kukufungulia milango ya riziki .Nilifukuzwa kazi katika mazingira ya kutatanisha lakini nilizidisha kumuomba mungu na wala sikuwahi kwenda kwa mganga bali nilizidisha swala na kua na subra.Nilikua bila kazi kwa kipindi kifupi sana lakini mateso niliyopitia ni balaa maana kila biashara niliyofanya ikawa ngumu msingi wote ukakata nikaanza tena moja na kusaidiwa na ndugu.
NB:Kwasasa nashukuru mungu nimepata kazi tena yenye maslahi zaidi ya ile ya kwanza nakula AC safi tena kwa hasira naweka namba 16 TURBO MODE,Mods tafadhali nawaomba msiufute wala kuunganisha huu uzi
 

maharage ya ukweni

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
1,091
2,000
Maisha ni mitihani so inabidi kupambana sana na kumuomba mungu maana mda mwingine kila unalofanya linagoma mpaka ndugu wanakuona huna akili.watu wanakudharau hata JF hupati LIKES hata kama ukikomenti mara mia800 yaani full majanga.
 

maharage ya ukweni

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
1,091
2,000
Hakuna kitu kizuri kama kumtegemea mungu na kujenga mahusiano mazuri na muumba mbingu na ardhi maana atakuokoa sehemu ambayo wewe unaona haiwezekani.
Sometimes watu wakupeleka kwenye kheri bila ya wao kujua kwakukufanyia fitina
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom