Mrejesho: Namshukuru Mungu tumeachana kwa amani

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Nawashukuru wadau wa Jamii Forums hasa wale waliotoa ushauri kwa nia njema kabisa kabisa uzi wangu >> Niko ukweni leo usiku nitadhihirisha kila kitu mbele ya wakwe na mwenyewe akiwepo. Nimempa taarifa ya kumwacha mke wangu siku ya Alhamis. Alishtuka sana na kulifikisha jambo lile kwa wazazi wake bila kuniuliza kwanini namwacha.

Waliitisha kikao cha familia ambacho kingekusanya ndugu zangu na ndugu zake, ambacho kingefanyika kesho Jumapili, lakini nikawaomba nifanye kikao na familia yake kwanza kabla ya hicho kikao cha Jumla. Nilihitaji awepo Baba na shangazi tu, hata hivyo aliongezeka na Kaka (Mtoto wa baba mkubwa wa Mke wangu ambaye ni mwanasheria) Tumekaa kuanzia saa 3.30 mpaka saa 5.07

Nimetoa sababu zangu kwanini namwacha, Miongoni mwa maswali ambayo niliulizwa na shangazi ni kwanini siku ambayo mke wangu Wikori alikuwa guest sikutaka kufumania ili upatikane ushahidi wa kweli ambao hauna Shaka? Nilichomjibu ni kuwa namuheshimu sana Mzee Wambura, fumanizi lolote ambalo ningelifanya lisingemdhalilisha mtoto wao tu bali angedhalilika pia mpaka baba na familia mzima kwa ujumla.

Kidogo yule kaka yake ambaye ni mwanasheria alinijia juu kwa madai kuwa nililolifanya ni kosa kisheria (Udukuzi) hivyo swala langu inabidi pia lisikilizwe kimahakama. Hapo baba mtu alikuja juu na kusema hataki hilo jambo lifike mahakamani kwani kile tulichokikwepa ndicho kitakachotokea. "Tunaweza kushinda mahakamani lakini hatutaweza kuishinda aibu ya mtaani", alifoka mzee huyo na kuomba hata hicho kikao cha kesho kisifanyike tena.

MAMBO YALIKUWA MENGI LAKINI HOJA KUBWA ILIYOBAKI MEZANI NI KWANINI PESA WALIZOKUWA WANATUMA VINYAGO WA MKE WANGU ZILIKUWA ZINAPITIA KWENYE SIMU YA MAMA MKWE? Hilo halinihusu watamalizana wenyewe.

Mpaka naandika uzi huu naambiwa hali ya aliyekuwa mke wangu si mzuri amekimbizwa Hospitali. Sijui nini kimejiri.
 
Kwa nini umefikiria hivyo?
Uliyemwacha alishakuwa halali yako pekee! Wengine walikuwa wanaiba kidooogo tu! Sasa itakupasa umsake mwanamke mwingine ukipitia majaribu kibao ikiwemo kumtenga kwa ushawishi awakatae wapendwa/wapenzi wake wa awali, during this process mtakuwa mnachangia saaana na masela kabla ya ndoa na haiyumkini hata baada ya ndoa.
NI SULUHISHO LA MUDAMUDA, MAUMIVU YANATARAJIWA KUENDELEA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom