Mrejesho: Nafanyiwa sexual harassment na msichana wangu wa kazi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,799
Siku kadhaa nyuma nilileta uzi unaoelezea jinsi msichana wangu wa kazi anavyonifanyia vituko. Baada ya Yule binti kulewa na kulala kwenye kochi, nikampeleka chumbani kwake nikamlaza kitandani.

Kesho yake asubuhi nikamwita sebuleni na kumkanya vikali juu ya mwenendo wake. Sikuishia hapo, nikampigia simu mke wangu na huyo binti akiwepo, nikaweka loud speaker, nikamweleza mke wangu yoooote. Mke wangu alikuwa kimya akisikiliza.

Ndipo Yule binti kwenye huo mkutano akasema ni mke wangu ndio anamtuma. Akasema huwa anatumia simu za wale Mabinti wawili wadogo waliopo nyumbani kuwasiliana, na huo ulikuwa Ni mpango mahsusi kunipima kiwango changu Cha uaminifu.

Baadae mke wangu akanipigia simu na kuniomba msamaha kwa mbinu zake za kipumbavu. Wanandoa, hasa kina mama. Msiwawekee vishawishi waume wenu viwezavyo kuvunja ndoa zenu.

Vipi ningetembea na Yule binti kisha akashika mimba, nani ambaye angekuwa analia kama sio mke wangu mwenyewe ambaye ametasababisha hayo yote?

Kuweni waungwana
 
Back
Top Bottom