Mrejesho na ufafanuzi: Yatokanayo na tiba ya chumvi

Mkuu Mshana Jr tupo pamoja kuhusu matumizi ya kuogea maji yenye chumvi.
Je, yapi ni matumizi sahihi ya kutumia chumvi kama zindiko kulinda shamba na nyumba.
Naomba ufafanuzi kaka
Mwagia kavu au ukiwa umechanganya na maji katikati na kwenda pembe zote za shamba ama kiwanja au nyumba... Pia unaweza kumwagia kwa kuzunguka
 
Tiba Pekee ni Jina la Yesu Kristo wa Nazareth
Hakuna sehemu ambayo Yesu alitumia Chumvi Kuponya au kutakasa watu!!

Hata Mitume walioachwa wale 11 na Paulo
Hakuna mahali ambapo,waliombea watu au walitakasa watu kwa kupitia Chumvi!!

Matumzii ya Chumvi ni USHIRIKINA
Msinishangae niko macho muda huu... Huu ndio wakati pekee naweza kufanya kitu kwa kutulia, hakuna kelele na akili imerelax (hata watoto wanaotafutwa muda huu huwa makini sana) wanaotafutwa saa sita mchana mmh
Kwenye mada yetu ya tiba ya chumvi kumekuwa na maswali mengi huko kwa waziri mkuu... Kwa faida ya wengi nimeona baadhi ya majibu niyatoe hapa upenuni jukwaani

1. Kwanini baada ya kuogea chumvi mtu hupata/hulala usingizi mzito sana?
Jibu: chumvi ni kinga hasa huko kwenye ulimwengu wa roho, unapoitumia chumvi hukuletea kinga ambayo huzuia roho zote za mahangaiko na kuacha mwili ukiwa katika hali yake ya asili... Si kila unapokosa usingizi ni mawazo na stress sometimes ni roho zinazotangatanga ndio zunakukosesha usingizi

2. Je ni lazima kufuata formula ya siku 7, 14, 21,.....?
Jibu : hapana hii ni tiba huru isiyomfunga mtu na taratibu za kidunia, formula ya 7, 14, 21 ni jinsi tu ya kuweza kuweka kumbukumbu na utaratibu wa kawaida usioathiri nguvu husika kama usipofuatwa.. Unaweza kufanya mara nyingi na randomly kadiri uwezavyo

3. Je ni chumvi gani hufaa zaidi?
Jibu: Chumvi zote zinafaa lakini kipaumbele ni chumvi ya mabonge ya bahari na ya kuchimba kienyeji (hizi zina nguvu zaidi) tofauti na za viwandani ambazo kwa kiasi zimepoteza uasili

4. Je naweza kufanya ibada na kutumia chumvi?
Jibu: ndio kwa kuwa chumvi haina mahusiano na uchawi labda uchanganye mwenyewe na vingine

5. Je napaswa kunuia nini?
Jibu: Yale utakayo, kwa remedy ya kawaida huna haja ya kutamka chochote lakini kwenye shida nuia na kunia mema, huku ukizifukuza na kuziseta nguvu zote hasi, hakuna maneno rasmi kwenye hili

Haya ndio baadhi ya maswali yaliyoulizwa sana, nitajibu mengine yatakayojitokeza hapa na kule
1aad027bb7ed5cac2fffd5fba36de4bf.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tiba Pekee ni Jina la Yesu Kristo wa Nazareth
Hakuna sehemu ambayo Yesu alitumia Chumvi Kuponya au kutakasa watu!!

Hata Mitume walioachwa wale 11 na Paulo
Hakuna mahali ambapo,waliombea watu au walitakasa watu kwa kupitia Chumvi!!

Matumzii ya Chumvi ni USHIRIKINA
Mathayo 5;12-13,Marko 9:49-50,Mambo ya walawi 2;13,Waamuzi 9:45,2Wafalme 2:20-21 na vngne vingi!!tusiambiwe ambiwe tu na hawa "mitume" na "manabii" wenye sauti nzito nzito,tusome biblia & Quran (waislam) majibu yote yamo humo
 
nimeanzisha mada ili iwasaidie wengine. Kuacha kujibu ni kukimbia wajibu na kutotenda haki

Jr
Kaka Mshana, kwanza asante kwa mada yako nzuri na kwa kujitolea kusaidia watu. mm naomba kufahamu zaidi ni namna gani chumvi inaweza kutumika kuzuia watu wabaya wasiharibu mazao shambani. Na je hiyo chumvi unaitumia wakati ukiwa umepanda tayari au bado ukiwa hujapanda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itumie nyakati zote na inasaidia sana kwenye ishu za KUKOPEA mazao... Unalima wewe wanavuna wengine
Kaka Mshana, kwanza asante kwa mada yako nzuri na kwa kujitolea kusaidia watu. mm naomba kufahamu zaidi ni namna gani chumvi inaweza kutumika kuzuia watu wabaya wasiharibu mazao shambani. Na je hiyo chumvi unaitumia wakati ukiwa umepanda tayari au bado ukiwa hujapanda?

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Although salt is powerful in historical and metaphorical terms, its spiritual power often goes unnoticed. Spiritually speaking, salt is considered the great neutraliser. It can help cleanse, heal and balance energy, while repelling negative vibrations. ... Rock salt helps in clearing up this residue to a great deal.

Wewe dingi nimetumia hiyo chumvi mwezi sasa mambo sio mabaya ila mvuto umeongezeka daaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mathayo 5;12-13,Marko 9:49-50,Mambo ya walawi 2;13,Waamuzi 9:45,2Wafalme 2:20-21 na vngne vingi!!tusiambiwe ambiwe tu na hawa "mitume" na "manabii" wenye sauti nzito nzito,tusome biblia & Quran (waislam) majibu yote yamo humo
Sasa sisi ambao hatuamini biblia wala Quran unataka tusitumie pia. Kama wewe huamini hayo ni matatizo yako usitake kupangia watu nini cha kufanya hapa mjini wewe pambana na hali yako tu vifungu vyako hivyo.
 
Tiba Pekee ni Jina la Yesu Kristo wa Nazareth
Hakuna sehemu ambayo Yesu alitumia Chumvi Kuponya au kutakasa watu!!

Hata Mitume walioachwa wale 11 na Paulo
Hakuna mahali ambapo,waliombea watu au walitakasa watu kwa kupitia Chumvi!!

Matumzii ya Chumvi ni USHIRIKINA
Sasa ikiwa mtu ni mgeni hajawahi kuja huko Nazareth anafanyeje?
Au utupie hapa namba za simu za huyo mganga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom