Mrejesho muhimu: Madhara ya dawa za kupunguza uzito

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
23,036
2,000
Kwanza napenda sana kuwashukuru wote ambao huwa mnanitia moyo katika safari yangu ya kupunguza uzito. Katika shauri nilizopata kuna mdau alikuja PM akaniambia nichemshe giligilani ninywe kila asubuhi na wakati wa kulala ndani ya siku moja nitapungua kilo tano.

Kweli nilifanya hivyo siku ya kwanza kweli nilipungua kilo moja siku ya pili kilo moja. Usiku wake sasa nikaanza sana kuumwa na tumbo na kichwa .tumbo lenyewe likawa linauma kama la period. Hazikuwa tarehe zangu ilikuwa kama bado week moja hivi kwahiyo nikajua labda ni ovulation
asubuhi nikakuta hali sio hali yaani duka la always limehamia kwenye pochi yangu jamani nitaishiwa damu mimi nifanyeje.

Nawashauri wajawazito wakae mbali na hili jani ndo lililoniletea majanga

upload_2017-6-19_13-10-55.jpeg
 
Sakayo

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
56,561
2,000
Jaribu kuwa na nidhamu ya ulaji wa chakula,pia epuka vitu vya baridi sana.Zingatia mazoezi na maji moto glasi moja asubuhi yenye ndimu nzima na jioni glass moja
Kama anaweza kutumia glass mbili asubuhi ingekuwa poa zaidi maana anakuwa hajala chochote, inasaidia kuyeyusha mafuta kwa urahisi zaidi
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,691
2,000
Kama anaweza kutumia glass mbili asubuhi ingekuwa poa zaidi maana anakuwa hajala chochote, inasaidia kuyeyusha mafuta kwa urahisi zaidi
Asante mkuu kwa kuongezea zaidi.Aachane na hayo madawa sio mazuri
 
Salmah99

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
308
500
binzari nyembamba(cumin water) ndo zinapunguza uzito
zinauzwa madukani au kwenye masoko
 
mkabasia

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
2,032
2,000
Mungu wangu hilo jani ndo lina madhara hayo.Mpaka nimeogopa suku moja kilo.Kwa iyo una over bleed au nini .
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
6,340
2,000
Kwanza napenda sana kuwashukuru wote ambao huwa mnanitia moyo katika safari yangu ya kupunguza uzito. Katika shauri nilizopata kuna mdau alikuja PM akaniambia nichemshe giligilani ninywe kila asubuhi na wakati wa kulala ndani ya siku moja nitapungua kilo tano.

Kweli nilifanya hivyo siku ya kwanza kweli nilipungua kilo moja siku ya pili kilo moja. Usiku wake sasa nikaanza sana kuumwa na tumbo na kichwa .tumbo lenyewe likawa linauma kama la period. Hazikuwa tarehe zangu ilikuwa kama bado week moja hivi kwahiyo nikajua labda ni ovulation
asubuhi nikakuta hali sio hali yaani duka la always limehamia kwenye pochi yangu jamani nitaishiwa damu mimi nifanyeje.

Nawashauri wajawazito wakae mbali na hili jani ndo lililoniletea majanga

View attachment 526945

inapatikana wapi hiyo giligilani mkuu,hakuna namna lazima hiki kitambi nikiondoe,kinanikera kweli
 
Sakayo

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
56,561
2,000
Pole sana mkuu
Kama unata kupunguza uzito kwanza kuwa mtu wa mazoezi hata ukiwa home kwako ruka walau kamba....

Asubuhi Jitahidi upate maji glass mbili ya uvuguvugu yenye limao au ndimu..

Mchana Jitahidi kula chakula cha wastani na mboga mboga nyiiiiingi..

Jioni waweza pata mchanganyiko wa matunda hasa tikiti, tango na papai...

Kama wala yai hakikisha liko na pilipili hoho husaidia saana kupunguza uzito...

Pole mwaya!!!!
 
asante sana yaani cha moto nakiona . hadi kichwa kinauma
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom