Mrejesho: Mke mwenye wivu, nawashukuru wana JF kwa msaada wenu

Ndugu zangu naomba nilete mrejesho wa ushauri wenu,

Ni majuzi nilifungu uzi hapa, unaosema hivi Mke mwenye wivu uliopitiliza nilipitia kila coment ya mtu wengi walinambia huyo atakua anakusaliti hivyo anajikinga.

Mimi ni muoga sana sipendagi kumfatilia hata simu yake sitakagi kushika, nilimwambia mke wangu nimeulizia kwa watalaamu wa mahusiano wameniambia wewe utakua ndo mchepukaji.

Alistuka sana mpaka nikahisi kuna kitu, juzi tumezinguana kidogo, zimepita siku tatu maelewano hakuna kabisa mpaka leo asubuhi nimeamka nikashika simu yake sikuamini macho yangu, nimekuta SMS anachat na jamaa ambaye ni mpangaji mwenzetu sehemu nilipomfungulia ofisi kwakweli nimeumia sana nilichofanya ni kumnyang'anya funguo za ofisi kuna mdogo wangu ndo kaenda kufungua, mimi mwenyewe nimeshindwa kufanya kazi nimerudi nyumbani tupo tunaangaliana tu sina cha kumfanya.

Naombeni ushauri mwingine
Mfanyee tu mkuu
 
Nisaidieni maana mpaka sasa sjajua cha kufanya nmeondoka nyumbani kuja ofsin lkn sijisikii vzr kabisa nimemtumia sms nisimkute hom akasema anamsubiri mtoto atoke shule ili andoke naye na anajua mi ninavyompenda watoto wangu nimemwambia aondoke na mdogo nibaki na mkubwa anasema hawezi kuhacha mtoto labda afe
Sasa huyo hakupendi... hivi na wewe unaogopa kuhusu watoto waachae aende nao wakimshindwa atawarudisha
 
Kila ndoa watu wangekuwa wanaachana hivyo. Pple zingebaki single nyingi

Kaa angalia ukimuacha na kuto muacha faida na hasara ipo wapi

Wakati mwingine ushauri mzuri ila ndoa nyingi zinavunjika sababu ya ushauri wa watu kutoka nje, kaa alone jiulize maswali unakosea wapi, ila mpe adhabu ya kuto muuliza, ukiona hasira zimeisha na maamuz yanatoka ndani ya moyo.wako utaamua kumuacha au kumsamehe na kumpa onyo.

Nyumba zinaficha mengi, paa linasikia mengi, kuta, ardhi, milango na madirisha na mbingu zinasikia mengi, lakin huyakuti nje. Tumia hekima na busara vzr
Ndoa sio ya watu weengi au ya group ndoa ni yako na mkeo hivyo amua kama wewe na mkeo

Ushauri unaweza jenga na pia kubomoa kuwa makini na ushauri pia.
 
Nisaidieni maana mpaka sasa sjajua cha kufanya nmeondoka nyumbani kuja ofsin lkn sijisikii vzr kabisa nimemtumia sms nisimkute hom akasema anamsubiri mtoto atoke shule ili andoke naye na anajua mi ninavyompenda watoto wangu nimemwambia aondoke na mdogo nibaki na mkubwa anasema hawezi kuhacha mtoto labda afe

Duuh huyo kakuchoka aisee yaani anajibu kana kwamba hakijatokea kitu
 
Kila ndoa watu wangekuwa wanaachana hivyo. Pple zingebaki single nyingi

Kaa angalia ukimuacha na kuto muacha faida na hasara ipo wapi

Wakati mwingine ushauri mzuri ila ndoa nyingi zinavunjika sababu ya ushauri wa watu kutoka nje, kaa alone jiulize maswali unakosea wapi, ila mpe adhabu ya kuto muuliza, ukiona hasira zimeisha na maamuz yanatoka ndani ya moyo.wako utaamua kumuacha au kumsamehe na kumpa onyo.

Nyumba zinaficha mengi, paa linasikia mengi, kuta, ardhi, milango na madirisha na mbingu zinasikia mengi, lakin huyakuti nje. Tumia hekima na busara vzr
Ndoa sio ya watu weengi au ya group ndoa ni yako na mkeo hivyo amua kama wewe na mkeo

Ushauri unaweza jenga na pia kubomoa kuwa makini na ushauri pia.
Nimependa ushauri wako
 
Natoa ushauri mdogo tu,Mke kuchepuka kuna vitu viwili na zaidi vinasababisha 1,UPENDO kudhoofu.2,Mume kuwa bussy kupitiliza,3.Tabia ya Asili.Sasa katika vitu hivi lazima kuna mojawapo inampelekesha mkeo.Nini kifanyike,1.Muombe sana Mungu amfungue macho ya ndani aone jinsi mabinti wanavyoangaika kutafuta waume wa kuwaoa,2.Msamehe kutoka Rohoni na umwonyeshe Upendo wa hali ya juu,3 3.Zungumza naye kwa upole atakuelewa.
NB:UPENDO USTIRI WINGI WA DHAMBI.
 
boss bado upo na huyo mwanamke? inaonesha kuna nguvu flani za ziada mwanamke anazo, huwezi kuchukua maamuzi juu yake.
 
Pole sana ndugu yangu. Mambo mengi yanaumiza dunia hii. Mchukue mke wako mwende kwa mchungaji kama kanakubali mkaombewe na kama atakiri kuachana na huyo mtu basi muendelee. Kitu kigumu ni kusahau. Inabidi Mungu akusaidie kusaahau.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom