MREJESHO: Makubaliano na Gazeti la Kisiwa kuhusu simulizi ya 'GERANIMO E.K.I.A'

Habari Wakuu,

Juzi niliandika thread hapa nikitoa malalamiko kwa gazeti la Kisiwa kwa kutumia makala yangu yenye kichwa cha habari 'Geranimo E.K.I.A: kutoka makao makuu ya CIA Langley, Oparesheni ya kukamatwa Osama Bin Laden' katika gazeti lao la tarehe 14 Octoba (Toleo Namba 463) pasipo ruhusa yangu.

Malalamiko yangu makubwa yalikuwa ni mawili, Mosi; kushindwa kwao kutoa 'credit' kuhusu muandishi halisi wa makala hiyo na pili kutokuwepo kwa makubaliano yoyote ya kimaslahi kati yangu na wao.

Nashukuru kwa uungwana wa Gazeti la Kisiwa kwani licha ya 'misunderstanding' iliyotokea lakini tumewasiliana na tumefikia makubaliano kuhusu sehemu ya makala waliyoitumia na sehemu iliyobaki ambayo itachapwa wiki hii tarehe 21 octoba, 2016.

Niwashukuru wanaJF wote walionipa ushauri kuhusu hili jambo lakini pia niwashukuru wanaJF wachache ambao kana kwamba 'wamekula kiapo' kukatisha wengine tamaa na wale walionishutumu nimenakili makala ile kutoka kwa muandishi huko Facebook anaitwa Josephat Nyambea.

Lakini binafsi nimshukuru Bw. Nyambea kwa uungwana wake kwani baada ya kuiweka makala hii huko Facebook hakutaka kupretend kuwa ni makala yake ndio maana mwisho wa Bandiko lake akaandika "Source: Jamii Intelligence". Huu ndio uungwana tofauti na "bwana yule" anayechukuaga makala hapa na kuzipeleka Facebook na kudai yeye ndiye muandishi.

Bw. Joseph Nyambea umeonyesha weledi na uungwana.

Mwisho kabisa nirudie shukrani zangu kwa Gazeti la Kisiwa kwa kukubali kulizungumza hili suala na kufikia makubaliano na pia kwa dhati kabisa nawashukuru The Boss, Kiranga, Nifah, oyaya karanga, magnifico, SANCTUS ANACLETUS, wambeke, gwankaja na wote mnaosoma thread zangu kwa ushauri adhimu na encouragement..

Asante.

The Bold
Hongera mkuu.. Wakatishaji tamaa wapo kila mahali, ila ukiona watu wanacopy kazi yako ujue una kitu cha ziada ambacho inabidi ukifanyie kazi!

Ila inaudhi sana, mimi huwa naandika makala za uchambuzi wa muziki hasa bongo flava kule fb ila mara kibao nimekuta makala zangu kwenye blog mbali mbali huku wakiwa hawajasema chochote kuhusu mwandishi wa makala husika!!
 
Hongera mkuu.. Wakatishaji tamaa wapo kila mahali, ila ukiona watu wanacopy kazi yako ujue una kitu cha ziada ambacho inabidi ukifanyie kazi!

Ila inaudhi sana, mimi huwa naandika makala za uchambuzi wa muziki hasa bongo flava kule fb ila mara kibao nimekuta makala zangu kwenye blog mbali mbali huku wakiwa hawajasema chochote kuhusu mwandishi wa makala husika!!
Nashukuru sana Mkuu!
Tanzania bado sana watu wanapuuza masuala ya 'intellectual property'.. Mtu akiona kitu kimemvutia akakopi na kutumia atakavyo! This has to stop
 
Ila usituuzie na sisi huku mkuu! Maana wakisha kuchukua kule lazima watakuambia usiwe unaandika huku ili watu tununue gazet. Tukumbuke na sisi mkuu
 
Keep up the good work. Tuletee kisa cha ugomvi wa marekani na Japan iliyopelekea bomu za nyuklia pamoja na aftermath yake
 
Back
Top Bottom