Mrejesho kwenu MMU, ushauri wenu umenisaidia sana

Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
296
500
Wasalaaam!

Sifa na utukufu kwa muumba wa mbingu na nchi, wote tuseme Amen!

Kwa wenye changamoto hajatuacha yuko nasi jana, leo na kesho.

Wakuu huu ni mrejesho kutoka kwenye thread yangu iliyokuwa na kichwa "AMENIAMBIA " hujanijua vizuri eee" niliyo ileta hapa week kadhaa zilizo pita.

Ni uzi ulio eleza safari ya maisha yangu na huyu binti naekaa nae kama mke na mme, ukweli ni kuwa ninefaidika na ushauri wenu mlio wengi hongereni sana.

Sikutaka kuja kuishi na mwanamke kibabe, sikutaka mimi na mke wangu tununiane nuniane lakini inanibidi,nimezaliwa na upendo mwingi ila wife napiga teke bahati hii sasa anaona kabisa inapotea taratibu.

Zaidi binti alikuwa jeuri, dharau, maneno yasiyo kuwa na heshima n.k mwanzo nilipata shida kujua ana tatizo gani,kumbe mimi ndiye niliekuwa nimekosea kwake kw a kujikita kwenye mahaba ya kihindi aisee! japo naamini nilionyesha upendo na ndivyo inavyotakiwa,

Nilimsaidia kazi anapokuwa tight kazini kwake maana yeye ana office yake binafsi lakini nimesitisha, sihitaji tena excuse hata awe na dharura akichelewa kutimiza majukumu yake juu yangu namuwakia balaa.

Kuna wengi walinishauri nimuache na wengine wakashauri nisitishe kutoa mahari ila niendelee kumwangalia na wengine wakasema atakuja kuniuwa wengine wakasema nimpe kichapo na wengine wakasema mimi ni bwege wengine wakasema nampenda sana ndo maana wengine wakasema nisitishe kumsaidia wala nisijihusishe na maisha yake tukae kigumu na mengine mengi.

Kiufupi niliwekeza nguvu kujibadilisha mimi, tangu siku hiyo naandika uzi hadi naleta huu uzi leo nimebadilika na kusitisha issues na mfumo wote wa maisha niliyomzoeza.

Kwa sasa nimevaa moyo nusu huruma nusu ukatiri japo napo apply ugumu nakuwa na huruma ndani ya moyo ila simuonyeshi kiasi kwamba amebadilika na kuanza kukosa raha muda mwingine.

Mahari sijapeleka na wala sijamwambia bila shaka anajionea mwenyewe kuwa hali niliyonayo kwa sasa sio salama kwa future yake na mimi, kuna siku aliongea na mama ake akamuuliza kuhusu mimi kupeleka mahari, alivoniuliza nikamjibu *SIJAKUJUA VIZURI NGOJA SIKU NIKIKUJUA NITAAMUA KUPELEKA AU NISIPELEKE* sasa hivi mimi ni mwendo wa u-serious na kujari mambo yangu. Nahakikisha tu anakula na kulala bila bugudha.

Nilikuwa nampa pesa za matumizi kwa mwezi mzima huku nimenunua kila kitu ndani but this time nimenunua mazaga ndani sijampa kitita cha mfukoni kwake kama zamani amebaki kushangaa tu.

Mke wangu ameanza kuniita kwa heshima, kunihudumia kama Mme wake, sauti yake imebadilika na kuwa ya unyeyekevu, amekuwa mtu wa kunishauri kuhusu life la baadae, amebadili muda wa kutoka kazini kwake anawahi kuja home na kuhakikisha anaweka mambo sawa, sasa hivi nikisema au kumkanya kitu anaomba msamaha na hatoi mdomo wala habishani tena,kiufupi namuona mwelekeo wake sio mbaya najiona mimi mme sasa.

Wanaume tuna roho ya upendo sana lakini wenzetu wakipendwa wanatafasiri upendo kwa kulipa dharau, kejeri, kiburi, n.k

Pamoja na hayo kuna mengi sana ambayo nayaona mazuri kutoka kwake mke wangu, one day dada ake akatutembelea home ghafla kiukweli alinikuta niko tofauti na siku zote na issue nzima ya mdogo wake anaijua maana nilishawahi kumdokeza ili aongee nae, so aliondoka akiwa hana raha yule shemeji yangu niliamua makusudi kumuonyesha uhalisia jinsi navoishi na mdogo wake japo sio kwa shari.

Najiona kwa sasa na baadae nitakuwa baba au babu mwenye kumshauri mjukuu au mwanangu wa kiume kuhusu mwanamke, nime experience uhalisia hivo naweza kuja kuwa mshauri mzuri kwa watoto wangu.

Ni hayo kwa kifupi wakuu.
 

Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
720
1,000
Usibadilike tabia yako mpya kuwa hivo kwa kitambo kidogo kwa maana atakunogesha hapo danganya Toto mwisho wa siku utaenda kuleleka mahari alafu arudie tabia take ya zamani............ sijui utaambia Nini watu
 

Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
296
500
Usibadilike tabia yako mpya kuwa hivo kwa kitambo kidogo kwa maana atakunogesha hapo danganya Toto mwisho wa siku utaenda kuleleka mahari alafu arudie tabia take ya zamani............ sijui utaambia Nini watu
Nakaza mkuu mana hivi ndo tunaenda vziri so siwezi kurudi kule
 

ni ngumu

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
3,792
2,000
Mwanamke ukiishi nae siku zote atakujaribu na vimitihani flani flani na kikubwa atapima msimamo wako...

Hivyo ni muhimu mwanamke ajue wazi kabisa Kila kizuri unachofanya kwake ni kwa sababu yeye ni muhimu kwako na unafanya sababu una mthamini Ila sio kwamba ni lazima ufanye na usipofanya Ana lolote la kukufanya.


Mi naweza kucheka na mke wangu hata miezi mitatu mfululuzo bila kumfokea wala kumletea ukauzu lakini Kuna vitu anajua akifanya hata dk moja sichukui nambadilikia hapo hapo...

Tunaishi sababu anajua Kuna mstari atakiwi kuvuka na hapo ndo heshima inapokuwepo..Nitakujali kadri ya uwezo wangu, nitakuheshimu kadri ya uwezo wangu Ila mstari flani usithubutu kuvuka.Nitakubadilikia mpaka ushangae mwenyewe.

Ukiweza kuwa na msimamo wako na kuweka mstari flani kwenye mahusiano yako basi Mambo mengine mwache afanye we tena puuzia kabisa ila Mambo ambayo ni ya msingi pale usicheke nae kabisaaaaa maana akijua Kila kitu anaweza fanya na huna utakachofanya ndo na dharau zinaanza maana unapoteza mvuto wako km mwanaume.

Mwanaume kuwa kama pilipili ,pilipili ukiiletea mazoea sana inakunyoosha,ukiiheshimu inakupa ladha
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,635
2,000
wanawake wengi wapo hivo mkuu, ukimuoa hua wanaanzisha majaribio ya kukutawala, nikuibie siri katika ndoa hakuna kitu mwanamke anapenda kama kumtawala mume maana hua wanaamin akimtawala mume atakua huru na mamlaka ya kufanya atakacho,

hongera kwa kuushinda mtihan mgum na kuirudisha heshima ya uanaume wako, nadhan kwa sasa kashakujua u wa aina gani hivo mtaishi vyema sana.
 

Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
296
500
Kweli mkuu naanza kuona mabadiliko makubwa sana. Na mimi siachii Clutch
wanawake wengi wapo hivo mkuu, ukimuoa hua wanaanzisha majaribio ya kukutawala, nikuibie siri katika ndoa hakuna kitu mwanamke anapenda kama kumtawala mume maana hua wanaamin akimtawala mume atakua huru na mamlaka ya kufanya atakacho,

hongera kwa kuushinda mtihan mgum na kuirudisha heshima ya uanaume wako, nadhan kwa sasa kashakujua u wa aina gani hivo mtaishi vyema sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom