KABAKA28
Senior Member
- Jun 18, 2014
- 197
- 188
Habari wana Jf, natumai mu wazima.
Leo naomba kuuliza wataalam walio wahi kumiliki/Kutengeneza gari aina ya Honda Fit, naomba kujua yafuatayo:
1. Ustahimilovu wa miundombinu (Barabara za Tanzania).
2. Ulaji wa mafuta (Compared to IST, VITZ, RAUM-JAMII YA TOYOTA)
3. Upatikanaji wa spare zake na gharama za spea.
4. Kwanini sio nyingi mjini.
5. Je inafaa kufanyia biashara ya UBER?
Asante, naomba kuwasilisha.
MAONI NA MICHANGO YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
Kwa ufahamu wangu kuhusu hzo gari, nitakuelezea kama ifuatavyo
Declaration of interest;
- Nazipenda sana gari za Honda bila kujalisha ni aina gani. Na natumai ipo siku ntaacha kutumia Toyota na kuhamia Honda.
Maelezo kuhusu Honda fit kulingana na ufahamu wangu;
1)Honda ni moja ya gari ngumu sana zinazotengenezwa japan, hvyo ustahimilivu wa barabara zetu ni mkubwa sana.
2) Honda Fit ulaji wake ni mdogo sana kutegemeana na engines, wana engines za: 1.2L, 1.3L, 1.4L , 1.5L nimeweka kwenye hzo groups kuondoa confusion kwa maana zipo za 1198 cc, 1297cc, 1246cc na zote zinaangukia kwenye 1.2L. hvyohvyo kwa za 1.3, 1.4 na 1.5 .
Lakini nyingi za bongo zinaangukia kwenye 1.3L(1330cc na 1310cc).
Hvyo kwenye suala LA ulaji wa mafuta ni kidogo sana na haitatofautiana na IST au Vitz zenye 1.3L.
3) Upatikanaji wa spares ni mkubwa wala isihofi, na pia soku hizi mambo yamerahisishwa sana waweza kuagiza moja kwa moja.
4) Honda Fit ni nyingi ila inategemea unalinganisha na gari gani.
5) Unaweza kutumia kwa biashara, Honda fit zipo kwenye generations 3 kama ifuatavyo:
I. 2001 - 2008,
hizi ni kama kusema toleo kwanza na ndo zipo nyingi bongo.
II. 2009 - 2014,
hizi zipo chache na zinamuonekano mzuri sana waweza sema sio Honda fit, kama BMW
III. 2014 to present,
Kwa matoleo hayo ukichukua latest inaweza kupigia biashara na mteja wako akahisi kama upo kwenye Lamborghini au Maybach, kwa lugha nyepesi INAFAA KUFANYIA BIASHARA
Mrejesho
Habari za asubuhi wakuu??
Kama mwezi mmoja ulopita niliandika kuhusu kuomba uzoefu kuhusu Honda Fit ("UZOEFU KUHUSU HONDA FIT" Hii ndo ilikia title ya thread yangu)
Nashukuru sana wadau walijitokeza na kushare (you can reffer).
Lile gari nili liagiza kupitia SBT Gharama zake zilikua kama ifuatavyo.
Bei ya kununua $ 1,390
Bank Charges $ 60
Total CIF1,450
TRA 3,882,566
Bandarini 640,000
Agent fee 200,000
Approx. Total 7.9 Mill
Mchakato wote ulikua vizuri bila shida yoyote (Nawapongeza SBT kwa huduma yao bora)
Gari nimelichukua jana nikaenda nalo kwa fundi wangu, nikamwambia fundi nimeandaa kama 1.5 mill kwa ajiri ya kurekebisha hili gari, naomba uliendeshe uniambie lina tatizo gani kabla sijaingia nalo mtaani.
Fundi ali test gari akazunguka nayo ile mitaa ya kwa kakobe mwenge, alivyorudi akaniambia kaka, gari halina shida yoyote isipokua kufanya service tu.
Tutamwaga oili na kubadirisha filter na kufanya air cleaner. Akanishauri nibadiri matairi niweke makubwa kidogo au nilipandishe juu kidogo.
Gari linasoma limetembea km 46,000. Kwakweli nime wafurahia honda japo ndo kwanza leo siku ya tatu toka naliendeaha, sijajuta.
Mafuta nimeweka full tank, but bado sijafika katikati na unajua ukiwa na gari jipya unavyo washwa washwa kutembea nalo.
Naomba nimalize kwa kusema hivi
ASANTENI KWA USHAURI WENU NIMEPATA GARI ZURI KWA BUDGET YANGU NDOGO.
ASANTE JF.
Karibuni.
PIA SOMA:
- Naomba uzoefu kuhusu honda fit